Kwanini matajiri wengi wakifikisha miaka 60+ huanza kurudi kwenye kilimo?

Kwanini matajiri wengi wakifikisha miaka 60+ huanza kurudi kwenye kilimo?

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2015
Posts
25,030
Reaction score
61,298
kama umegundua Watu wengi wanaofanikiwa kwenye biashara au sekta nyingine mbalimbali, wakifika umri mkubwa hasa miaka 60 na kuendelea, wanaanza kuhamishia nguvu zao kwenye kilimo.

Mfano, Shabiby wa dodoma amefanya sana biashara ya mabasi na siasa, lakini sasa anaonekana kuwekeza kwa ukubwa kwenye kilimo cha mahindi huko Mpanda. kuna Joseph Kusaga, baada ya mafanikio makubwa kwenye media, sasa anawekeza kwa kiwango kikubwa kwenye kilimo cha soya huko Songwe.

Kinachonishangaza ni kwamba kilimo pia si kazi nyepesi hata kidogo. Kina changamoto zake, kinahitaji mtaji, usimamizi, uvumilivu na wakati mwingine hasara pia. Sasa ni nini hasa kinachowasukuma hawa watu kwenda huko?

au ndo tuseme binadamu anavyozeeka na kuona mwisho wa maisha unakaribia ndipo anaanza kurudi kwenye "nature" na kazi za asili kama kilimo na ufugaji? Je, kuna utulivu wa akili ambao haupatikani kwenye biashara nyingine? Au ni kwamba kilimo kina risk ndogo kuliko biashara nyingi walizokuwa wakifanya awali?Au pengine baada ya kutafuta pesa maisha yao yote, wanafika hatua wanaona thamani ya kuzalisha chakula kuliko kuuza bidhaa au huduma nyingine?
 
Kilimo kina risk kubwa, kwakua walisha enjoy maisha ujanani wanaona liwalo na liwe
Nakubaliana na wewe mkuu, ila nadhani kuna kitu kingine. Mzee akifika 60+ kelele za mjini zinaanza kumchosha. Hapo hata akipewa penthouse katikati ya jiji anaweza kuikataa na kukimbilia shamba lake.Asubuhi anaamka anasikia ndege wanalia, si honi za magari. Anavuta hewa safi, hakuna pollution, hakuna vikao vya bodi kila siku. Inawezekana pesa wanakuwa tayari wanazo, sasa wanatafuta amani ya moyo na kurudi karibu na nature kuliko kutafuta utajiri mwingine.
 
Hizo ni biashara ambazo hazina ushindani, Hazihitaji technologia kubwa sana, Ishort ni rahisi kuingia na kutoka.

Tofauti sana na biashara kama ya viwanda n.k.
Kweli mkuu nimekuelewa. kujenga kiwanda leo utasubiri mpaka 2030 hukoo ndo uanze kuona faida.....ila umejilipua shamba huko linaweza kukupa mrejesho fasta.... Mzee wa miaka 65 akianza mradi mpya anataka kuona matokeo akiwa bado ana nguvu za kuufurahia si kusubiri mpaka wajukuu waje kuvuna..
 
Wanaofikia umri huo na kwenda kwenye kilimo ni wastaafu wa serikali ama waliokuwa waajiriwa. Hakuna tajiri muhindi au mfanyabiashara ambaya ana hela akifika umri huo anaenda kulima.
Ukiona analima ujue amekuwa akifanya hivyo kabla hata ya kufika umri huo unaosema
 
Unaweza kuwa bilionea kwenye kilimo bila kufanya marketing. Ukilima mahindi hata ziwe hekari ngapi, unauza. Ukilima mpunga unauza. Ukilima soya unauza. Kasoro mali kuoza ndio zina bahati nasibu.

Population inakua kila siku, na wao wana mtaji hawana njaa hivyo akilima mpunga anaweka store kisha anauza December bei imeishapanda. Hakosi twice the investment ndani ya mwaka. Yaani kaweka 300M January, kavuna May, kaanika na kuweka store June, kauza December anachukua 600M yake kisha anatoa 300M kurudisha shambani.

Sasa jichanganye usome mchanganuo ulivyo rahisi udhanie kulima ni rahisi hivyo bila dedication. Kwanza kupata hizo ekari za kulima kwenye scheme ni vita watoto wadogo hawaiwezi.
 
Shabiby alianzia kwenye kilimo cha mahindi huko Gairo akiwa kijana kabla ya kumiliki mabasi na vituo vya mafuta!

Sumry ndiye kaachana na mabasi na kwenda shamba huko Nkasi.
 
Ila business sio Kwa watu dhaifu, Kuna muda ukipigiwa simu na wafanyakazi roho inaenda mbio balaa😀😀
 
Back
Top Bottom