Kwanini matajiri wengi wakifikisha miaka 60+ huanza kurudi kwenye kilimo?

Kwanini matajiri wengi wakifikisha miaka 60+ huanza kurudi kwenye kilimo?

mkuu kilimo ukiwa na mtaji hakina risk yeyote ile ... pawepo na dawa maji mbegu bora mbolea imeisha hiyo hapo sahau hasara.

ila uzoefu au elimu visikosekane.
 
Shabiby alianzia kwenye kilimo cha mahindi huko Gairo akiwa kijana kabla ya kumiliki mabasi na vituo vya mafuta!

Sumry ndiye kaachana na mabasi na kwenda shamba huko Nkasi.
yeah nilitaka kusema sumry sio shabiby
 
kama umegundua Watu wengi wanaofanikiwa kwenye biashara au sekta nyingine mbalimbali, wakifika umri mkubwa hasa miaka 60 na kuendelea, wanaanza kuhamishia nguvu zao kwenye kilimo.

Mfano, Shabiby wa dodoma amefanya sana biashara ya mabasi na siasa, lakini sasa anaonekana kuwekeza kwa ukubwa kwenye kilimo cha mahindi huko Mpanda. kuna Joseph Kusaga, baada ya mafanikio makubwa kwenye media, sasa anawekeza kwa kiwango kikubwa kwenye kilimo cha soya huko Songwe.

Kinachonishangaza ni kwamba kilimo pia si kazi nyepesi hata kidogo. Kina changamoto zake, kinahitaji mtaji, usimamizi, uvumilivu na wakati mwingine hasara pia. Sasa ni nini hasa kinachowasukuma hawa watu kwenda huko?

au ndo tuseme binadamu anavyozeeka na kuona mwisho wa maisha unakaribia ndipo anaanza kurudi kwenye "nature" na kazi za asili kama kilimo na ufugaji? Je, kuna utulivu wa akili ambao haupatikani kwenye biashara nyingine? Au ni kwamba kilimo kina risk ndogo kuliko biashara nyingi walizokuwa wakifanya awali?Au pengine baada ya kutafuta pesa maisha yao yote, wanafika hatua wanaona thamani ya kuzalisha chakula kuliko kuuza bidhaa au huduma nyingine?
Ukiona tajiri ameenda kwenye kilimo ujue ameenda kutakatisha fedha
 
Washaanza kupiga dili haranu nyingi, wanatakatishia pesa huko maana hizi bisahara zao za kila siku zinafahamika.
 
Back
Top Bottom