Kwanini matumizi ya Mbolea za Kisasa katika nchi za Afrika ni lazima ikiwa nchi za Ulaya wanatumia Samadi?

Wacha uongo kiongozi! Hebu soma hapa chini!
 
Si taratibu, zikishatumika mara 1 tu basi hakuna zao lolote litalostawi wala kuota bila ya hizo mbolea artificial na hapo ndipo ujue wapi dunia ilipofikia.

Ubinadamu ni kazi/The humanity is a work.
 
Sio lazima kutumia mbolea za kisasa, unaweza kuendelea kutumia samadi.
 
Acha kuwaonea wataalamu wa kilimo.Ni msomi yupi nchi hii mwenye nguvu kukiko wanasiasa? Nchi hii ujifanya mjuaji na kupinga maamuzi ya wanasiasa utaishia kutekwa. Ndio maana watu wanaangalia tu bora liende
 
Samadi ni kwa wakulima maskini au wale wa hobby tuu, hakuna serious commercial farming inayotumia samadi, bila modern agricultural machineries na mbolea za nitrogen wote mngekuwa mmekufa na njaa nyie, huo mchele mnaokula, ngano, sukari, mafuta etc 90% tunaagiza, mnafikiri vinalimwa na samadi? hata wakulima wetu wakiacha kutumia mbolea za viwandani watu watakufa njaa, Tanzania tunaagiza chakula kuliko mafuta ya petrol na sababu kubwa ni umaskini wa kutumia vitu kama samadi
 
Hawatumii mbolea za kutengeneza maabara, je, kwanini sisi weusi watu wetu wanalazimishwa kutumia mbolea za kutengenezwa kutoka maabara?

Wasomi mnao elewa mambo embu mtupe elimu katika hili, asanteni.
Hata vyakula kwenye mahoteli makubwa wako selective sana, nilishuhudia wakikataa kula kuku na beef wakisema zime tritiwa na madawa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…