Kwanini Mawaziri wengi awamu ya Tano na sita wanapoingia ofisini uanza kuwachongea wakuu wa taasisi waliowakuta waondolewe?

Kwanini Mawaziri wengi awamu ya Tano na sita wanapoingia ofisini uanza kuwachongea wakuu wa taasisi waliowakuta waondolewe?

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2019
Posts
762
Reaction score
6,984
Akiteuliwa Waziri wa Mambo ya ndani lazima apambane na wakuu wa idara aliowakutwa,akiuliwa Waziri wa ardhi naye Kila anayemkuta ofisni Hana sifa, akiteuliwa Waziri wa sheria naye ana watu wake, kilimo Kila sehemu anataka yeye atawale nk

Je, wanapata wapi nguvu yakufika ofisini na kuanza mikakati ya tumbutumbua na mikakati Hiyo kuidhinishwa na mamlaka ya uteuzi? Kutumbua au kupangua safu kumewahi kuifanya serikali Gani ikafikia malengo? Gharama za utumbuaji upitiwa na mteuaji kabla ya kuanguka wino?

Huko watendaji wanapopelekwa wanakwenda kukaa benchi au wanarejeshwa nyumbani na kusitishiwa mishahara? Kama wanaenda benchi Katibu Mkuu Kiongozi anatakwimu za watumishi waandamizi ambao Awana majukumu rasmi serikalini na wanalipwa posho na mishahara bila kufanya KAZI?

Kwanini Mhe. Rais utaratibu wa kustaafu Kwa maslahi ya umma na kulipwa stahiki usitumike kupunguza nguvu KAZI isiyo na kazi Kwenye kazi za umma? Ukimstaafisha Mtumishi mwandamizi mmoja naamini unapata fedha za kulipa waajiriwa wapya wawili au watatu....kwanini tusijiongoze?
 
Back
Top Bottom