Kwanini Mbeya maisha yako nafuu kiasi hiki ukilinganisha na sehemu zingine za nchi yetu?

Kwanini Mbeya maisha yako nafuu kiasi hiki ukilinganisha na sehemu zingine za nchi yetu?

kyagata

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2016
Posts
10,406
Reaction score
19,892
Niko Mbeya nashangaa shangaa
Naona mabucha mengi ya nyama ya ng'ombe yanauza nyama kilo 6,000/=
Kitimoto kilo ni 8000/=
Mchele kilo ni 2000/=
Mafuta ya kupikia lita 5 ni 23,000/=
Maharage kilo ni 2500/=
Ndizi mkungu ni elfu 5 tu.
Matunda yapo ya kila aina,mfano maembe bakuli zima ni jero tu.
Hiki kitu kimenishangaza sana wakuu,hawa jamaa wana serikali yao tofauti na hii ya ndugu Samia?
 
Kama kweli hizo ndio bei halisi, basi nadhani kuna haja ya kuangalia tena wapi panafaa mtu kuweka makazi yake kwa sasa.

Kwa hali ilivyo sasa, elfu kumi(10,000) ya kitanzania haina thamani hata kidogo ukienda nayo sokoni/dukani.
 
Nilikwenda Mbeya 3 years back nilivutiwa sana na life simple kweli kweli
 
Ukilinganisha na Dar huko kuna nafuu, sijui mzunguko wa pesa ukoje ila bidhaa walau ziko chini kidogo, kuna sehemu hapa dar mchele ni 3,500, nyama 9,000, maharage 4,000 nk. Kifupi maisha yapo juu sana.
Of course, huwezi kulinganisha Dar na Mbeya.

Mbeya wanazalisha, na bidhaa nyingine ndio zinapelekwa Dar.
 
Back
Top Bottom