Kwanini Mbezi beach imepoteza umaarufu wake iliyokuwa nao miaka ya nyuma?

Kwanini Mbezi beach imepoteza umaarufu wake iliyokuwa nao miaka ya nyuma?

Maeneo dar yanashift status tu..masaki to Mikocheni to Mbezi beach now Mbweni ndio habari ya mjini. Still bado mbezi beach status haijapotea sana , sema wenye nyumba wengi walishafariki watoto either hawazijali na wengine wako nje , so tunapoelekea nyumba nyingi Mbezi beach zitakuwa maofisi na makampuni kupanga kama Mikocheni na masaki
Ni kama ilivyokuwa Sinza, sasa hivi Tabata ndio inakimbiza na Kinyerezi yake.
 
Maeneo dar yanashift status tu..masaki to Mikocheni to Mbezi beach now Mbweni ndio habari ya mjini. Still bado mbezi beach status haijapotea sana , sema wenye nyumba wengi walishafariki watoto either hawazijali na wengine wako nje , so tunapoelekea nyumba nyingi Mbezi beach zitakuwa maofisi na makampuni kupanga kama Mikocheni na masaki
Nafikiri huko ndio tunapoelekea 😀
 
Hata Bagamoyo ya Mapinga kilikuwa kijiji cha Wamakonde.

Wale Jamaal Wana utamaduni wa kutotaka kuchanganyika na jamii nyingine, sehemu wakianza kuingia jamii nyingine wanauza wanasepa.
Wamakonde nao walikuja kutoka Mtwara wakajimilikisha maeneo mengi ya wilaya ya Kinondoni ambayo kiasili yalikuwa ni maeneo ya wazaramo. Ila waliyanunua na kujimilikisha wao, alaf baadae na wao wakayauza na kutafuta maeneo mengine.

Ni kama wamanyema walivyotoka Kigoma wakaja kujimilikisha maeneo mengi ya Kariakoo, na ndio walioungana na wenyeji halisi wazaramo na wazee wengine wa kiswahili kuleta songombingo la kupigania uhuru nk.

Baadae wazee wa Kimanyema walipofariki watoto wao wakaanza kuyauza maeneo yale kwa watu wengine kutoka mikoa mingine, alaf wao (wamanyema) wakatokomea na kusambaa katika maeneo mengine ya Sinza, Kinondoni nk.

Wazaramo, wandengereko, Wamakonde, wamanyema na makabila mengine yaliowahi kufika Dar es salaam na kumiliki maeneo ya mijini, kama wangekuwa wana elimu na uwezo wa kuona mbali, basi wao ndio wangekuwa madon wanaomiliki maeneo yote ya maana mjini hapa.
 
Back
Top Bottom