Kwanini Mbezi beach imepoteza umaarufu wake iliyokuwa nao miaka ya nyuma?

Kwanini Mbezi beach imepoteza umaarufu wake iliyokuwa nao miaka ya nyuma?

Nakataa hii hoja.
Mbezi beach kutaendelea kuwa sehemu maarufu, ghali, yenye mvuto kuliko mbezi ya upande wa pili.
Hata ukitaka nunuwa kiwanja uliza bei uone.
Kweli mbezi beach ina barabara mbovu, kweli madimbwi na mitaa kunuka, hiyo haina tofauti na masaki, mikocheni nk nk
Kama ukisema mbezi ya kimara, Luis na makabe kumejaa wachaga na nini nitakubali, ila status? Bado sana sana sana
Mkuu mimi sizungumzii kwa kujengwa au thamani ya eneo. Nazungumzia umaarufu ilionayo leo Mbezi louis ni mkubwa kuliko umaarufu wa Mbezi beach, na wakati miaka ya 90 asilimia 85 ya wakazi wa Dar na mikoani hawakuwa wanaifahamu Mbezi louis.

Kuna baadhi ya watu mikoani ukisema mbezi beach, wao wanafikiri labda hiyo beach ipo karibu na stand ya Magufuli, hawajui kabisa kama Mbezi beach ni eneo lingine lililo katika wilaya na kata nyingine na inajitegemea.
 
Ila maisha yako tofauti sana, kuna sehemu kiwanja ni milion 100+, wakati hiyo ni bajeti ya kujenga bonge la jumba kwa maeneo mengine
 
Lakini bado karibu sana mjini kwa kutumia daraja...labda bongo idadi ya wenye hela sio kama nigeria au kenya
Ukiona wanaija na wakenya wanavyoshangaa youtube kwa jinsi kulivyopendeza na bei ya nyumba za huko Avic town na kumetelekezwa...
Wanasema ingekuwa kwao, bei ingekuwa mara tatu na zamani kungeshajaa wenye hela zao...
Inategemea na uhaba wa ardhi na culture ya watu. Kwa Tanzania bado watu wana options za kupata sehemu nyingine ambazo zipo karibu na wakajenga nyumba za ndoto zao.
Kiukweli si watanzania wengi wanapenda krishi kwenye gated conmunities
 
Maeneo dar yanashift status tu..masaki to Mikocheni to Mbezi beach now Mbweni ndio habari ya mjini. Still bado mbezi beach status haijapotea sana , sema wenye nyumba wengi walishafariki watoto either hawazijali na wengine wako nje , so tunapoelekea nyumba nyingi Mbezi beach zitakuwa maofisi na makampuni kupanga kama Mikocheni na masaki
 
Habari wana jamii forum?

Kuanzia miaka ya elfu mbili kushuka chini, eneo la Mbezi beach lilikuwa ni kati ya maeneo machache ya jiji la Dar es salaam ambayo yalikuwa na umaarufu mkubwa kama vile ilivyokuwa Masaki, Osterbay, Sinza nk.

Hii ilipelekea watu wengi hasa wa mikoani wakisikia neno Mbezi, basi akili au mawazo yao yanaenda moja kwa moja kwenye Mbezi beach. Japo Mbezi ya Kimara ilikuwepo, lakini watu hawakuwa wakiifahamu kivile kama inavyofahamika leo.

Sasa hali imekuwa ni tofauti, Mbezi ya Kimara imetokea kuwa na umaarufu mkubwa hadi kupelekea Mbezi beach kusahaulika. Leo hii mfano ukiwa mikoani ukazungumzia neno Mbezi bila kuweka hilo neno beach mbele basi kila mtu akili na mawazo yake yataenda kwa Mbezi ya Kimara kama vile mbezi luis, mbezi mwisho, mbezi magufuli nk.

Je, ni nini chanzo cha umaarufu wa mbezi kuibuka ghafla tofauti na hapo zamani?

Nawasilisha
Kwa sasa Mbezi beach ishakuwa chaka
 
Ila maisha yako tofauti sana, kuna sehemu kiwanja ni milion 100+, wakati hiyo ni bajeti ya kujenga bonge la jumba kwa maeneo mengine
Ndo hivyo mkuu. Unakuta kuna mtu anatafuta mchango wa Mil 5 ili mama yake afanyiwe operation fulan ya kuokoa maisha yake bila mafanikio, huku mungine anatumia Mil 5 hiyo kulewea mwezi mmoja inaisha na kupata nyingine.
 
Walijaa sana wamokonde na wapo ununio
Na wamakonde ndiyo watu waliyoweza kuanza kukaa kwenye maeneo mengi ambayo yalikuja kuwa hot...sema walishindwa kudumu huko
Hata msasani peninsula wamakonde kote walijaaa huko

Ova
Hata Bagamoyo ya Mapinga kilikuwa kijiji cha Wamakonde.

Wale Jamaal Wana utamaduni wa kutotaka kuchanganyika na jamii nyingine, sehemu wakianza kuingia jamii nyingine wanauza wanasepa.
 
Back
Top Bottom