Kwanini Mbezi beach imepoteza umaarufu wake iliyokuwa nao miaka ya nyuma?

Ni kama ilivyokuwa Sinza, sasa hivi Tabata ndio inakimbiza na Kinyerezi yake.
 
Nafikiri huko ndio tunapoelekea πŸ˜€
 
Hata Bagamoyo ya Mapinga kilikuwa kijiji cha Wamakonde.

Wale Jamaal Wana utamaduni wa kutotaka kuchanganyika na jamii nyingine, sehemu wakianza kuingia jamii nyingine wanauza wanasepa.
Wamakonde nao walikuja kutoka Mtwara wakajimilikisha maeneo mengi ya wilaya ya Kinondoni ambayo kiasili yalikuwa ni maeneo ya wazaramo. Ila waliyanunua na kujimilikisha wao, alaf baadae na wao wakayauza na kutafuta maeneo mengine.

Ni kama wamanyema walivyotoka Kigoma wakaja kujimilikisha maeneo mengi ya Kariakoo, na ndio walioungana na wenyeji halisi wazaramo na wazee wengine wa kiswahili kuleta songombingo la kupigania uhuru nk.

Baadae wazee wa Kimanyema walipofariki watoto wao wakaanza kuyauza maeneo yale kwa watu wengine kutoka mikoa mingine, alaf wao (wamanyema) wakatokomea na kusambaa katika maeneo mengine ya Sinza, Kinondoni nk.

Wazaramo, wandengereko, Wamakonde, wamanyema na makabila mengine yaliowahi kufika Dar es salaam na kumiliki maeneo ya mijini, kama wangekuwa wana elimu na uwezo wa kuona mbali, basi wao ndio wangekuwa madon wanaomiliki maeneo yote ya maana mjini hapa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…