kifupi kirefu
JF-Expert Member
- Oct 29, 2018
- 539
- 3,507
UTANGULIZI
Askari wa Usalama barabarani nikiungo Muhimu Sana kati ya wamiliki wa vyombo vya usafiri na sheria zilizotungwa na bunge katika kudhibiti makosa yote ya usalama barabarani na sambamba na kuakikisha vyombe vinavyotembea ni tu vilivyo salama.
JE, NI KWELI ASKARI HAWA WANASIMAMIA USALAMA BARABARANI?
Asilimia kubwa ya watendaji Hawa wa serikali awasimamii usalama barabarani si kwa sababu wasingependa kusimamia usalama huo Bali nikwasababu sheria za barabarani kwa kiasi kikubwa zimewekwa zisimame kwa wanyonge. Wavunjaji wakubwa wa sheria za barabarani Tanzania ni watumishi wa Umma wakiwa na magari binafsi au magari ya serikali na kundi la pili ni watu wenye dhamana ya cheo serikalini, kundi la tatu ni wenye fedha na kundi la mwisho ni ndugu wa makundi matatu yaliyotangulia. Haya makundi ni vigumu kuyadhibiti yasitende makosa ya usalama barabarani si kwa sababu Yana Kinga bali kwa sababu ukipambana nao wanao uwezo na nguvu yakushinda. Hapa ndipo Askari barabarani anapoamua kutafuta zaidi namna ya kuishi kuliko namna ya serikali kuendesha mambo yake.
JE, ASKARI HAWA WANAAKIKISHA VYOMBO VINAVYOTEMBEA NI VYOMBO VILIVYO SALAMA?
Endapo wangeweza japo kwa asilimia 30% kupambana kuviondoa vyombo hatarishi barabarani may be ajali zingepungua lakini pia wenye navyo wangewekeza kuvifanyia maboresho. Ukaguzi unaofanywa na Askari si wakuondoa vyombo vyenye hitilafu barabarani bali niwakuhalalisha faini au pesa ya kung'arisha viatu kama Jamhuri ilivyowahi kuwaelekeza.
JE, KWANINI ASKARI BARABARANI WANASHINDWA KUTEKELEZA WAJIBU WAO?
Ni kwa sababu serikali imeshindwa kutekeleza wajibu wake. Askari wanapenda Sana kuasimamia sheria lakini na wao ni binadamu. Kuliko amtoze 30,000 dreva daladala huku akikaripiwa asimtoze mwenye V8 chocchote na akithubutu anapelekwa benchi basi Bora atengeneze ushirikiano wa kibiashara kati ya wanyonge na yeye, Mnyonge apate haueni kwa makosa yake na viatu ving'ae huku Jamhuri iliyoshimdwa kuwasimamia watu wake ikipata hasara.
Sambamba na hilo hapo juu lengo la Askari barabarani limebadilika Jambo kwenye maandishi ya serikali halijabadilika, leo hii Askari wa barabarani ana makisio ya makusanyo na taarifa zake zinasomwa bungeni hivyo siyo mdhibiti Tena Bali mkusanya mapato. Fomula ya ukusanyaji mapata haiangalii ubora wa huduma inaangalia wingi wa kinachotakiwa kukusanywa. Gari bovu au nzima yote yanatembea na hakuna wakuzuia maana ukiyazuia umezuia mapato.
JE, NI MBINU GANI ASKARI UTUMIA KUSHIRIKIANA NA WAMILIKI WA VYOMBO VYA MOTO KATIKA KAULI MBIU YA NIPE NIKUACHIE?
Zipo mbinu kadhaa lakini naomba nitaje chache kwa ufupi na unaweza kufuatilia uweze kuthibitisha ukweli;
1. Kwa mabasi ya Mikoani mbinu kuu inayotumika nikondakta kufunga kiasi flani Cha fedha kwenye karatasi Kisha kumkabidhi dreva. Mara tu anaposimamishwa upeana ishara na trafiki Kisha kuangusha kile kikaratasi chenye KIWI chini nakupiga honi Kisha kuondelea na safari. Mbinu hii imeonyesha mafanikio makubwa na nivigumu kunaswa na kamera za wanaojidai wazalendo.
2. Mbinu ya pili, vituo vya trafiki barabarani vimeajiri raia wema ambao kazi yao kuu nikumfuata dreva nakuchuku ujira wa mwiha nakurejea kwenye kivuli. Kupitia mbinu hii hata ungejifunga camera mia mwisho wa siku uwezi kumnasa askari akipokea KIWI kutoka kwa dreva.
3. Kwa upande wa daladala, ushirikiano wao na Askari barabarani niwakizembe na usiofaa kufanywa na Askari anayejua thamani ya kazi. Kondakta wa daladala Hana Siri, akisimamishwa lazima apige yowe na baada ya kupiga yowe atamuuliza dreva tumtoe ngapi. Kisha ushuka na kuweka kwenye risiti ya zamani na kukabidhi kwa afande na kurejea kuendelea na safari. Mbinu hafifu Sana hizi na utokana na kutoaminiana kwa dreva na kondakta lakini pia kipato duni.
4. Kwa wale mandata wenye tamaa na wenye roho ya unyang'anyi upiga matukio machache yanayoumiza Kama vile tunavyoambiwa sadaka nzuri Ni ile inayouma. Hapa gari ukamatwa na kupelekwa kituo Kisha kuandikiwa makosa lukuki na ukitaka kulitoa au makosa yapungue unakata mpunga mrefu. Mbinu hii utumiwa Sana na mandata wenye mawe mabegani na ambao awapendi kushiriki sakramenti ya shetani na Askari wa chini. Kundi hili uzalisha Sana viongozi wa Askari barabarani na linabeba wale watu wanaojidai waadilifu.
5. Mwisho, nigusie stahili ya kaa mbali, unakamatwa Kisha unaambiwa nenda pale ukaprintiwe risiti. Hii stahili utumiwa na Askari wenye confidence na ambao wanajiamini kabisa kwamba kwenye mgao hakuna kudhulumiana. Hapa utumika kapu la sadaka na ulindwa na chuma kuepusha macho kuona asisogee eneo la tukio.
JE, KAMA MBINU ZA USHIRIKIANO ZIPO NYINGI HIVI NANI ANAUMIA?
Kwanza serikali inapoteza muda kunaza Askari barabarani kwa ajili ya ukusanyaji mapato, Bora wapunguze Askari wawapangie kazi nyingine.
Pili familia za Askari zinazidi kudidimia kwa kula vitu haramu kutoka kwenye mfumo haramu
Wenye magari wanashindwa kurekebisha vyombo vyao na hivyo kuongeza hatari ya kusababisha madhara kwa watumiaji
NINI KIFANYIKE?
Tuwekeze kwenye taa na camera za barabarani, tuondokane n ufuatailiaji wa binadamu. Tuweke mifumo ya udhibiti itakayorekeodi makosa na Kuandika adhabu ikiwepo kupunguza points kwenye leseni za madreva.
Mwisho niwaombe wananchi kusukuma agenda ya serikali kuondoa trafiki barabarani kwani endapo tutategemea askari hawa huku vyombo tunavyotumia vikiwa haviaminiki tutazidi kuteketea wao wakipeana pesa ya KIWI. Kumbukeni akipokea pesa ya KIWI nakuja kupokea pia pesa yakupima ajali na kuandaa Taarifa ya kwenda bima mara mnapoumia au kuondoka Duniania.
USHIRIKIANO WA ASKARI BARABARANI NA WENYE VYOMBO VYA MOTO UNA TIJA KABLA YA AJALI SI BAADA YA AJALI. TUJILINDE TUFICHUE WALA RUSHWA.

Upvote
2