Kwanini Mbowe hakwenda kumpokea Tundu Lissu?

Sasa nawe si uwe unatumia akili kidogo -mwenyekiti tena siyo mwenyekiti tu bali pia mwenye chama anawezaje kwenda kumpokea makamu mwenyekiti? itifaki haiko hivyo.
 
hakwenda kwa sababu ni kawaida mbona ulishajibu kwenye aya yako hapo juu, wakati Yohana mbatizaji yuko gerezani aliwatuma wanafunzi wake kwa Yesu kwamba niko kifungoni je ni wewe masihi wa bwana au tumtazamie mwingine,Yesu akawajibu akawaambia mwambieni Yohana vipofu wanapata kuona viwete wanakwenda,viziwi wanasikia waliopooza wanapata afya waliokifungoni wanawekwa huru
 
Vipi mapokezi yamedoda? Unawashwa sana wewe mdada
 
Dah! Mimi ni CCM Damu lakini naona kiitifaki sio sawa Mbowe kumpokea Lissu. Ila Lissu kumpokea Mbowe ni sahihi na lazima. Hata mwenyekiti wa CCM hawezi kwenda kumpokea Makamu Mwenyekiti. Kulamba asali haihusiani na hili tukio la kupokeana.
Ni sahihi mwenyekiti wa CCM kwenda kumpokea makamu mwenyeki Abdulrahiman Kinana kiitifaki imekaaje?hebu tuanzie hapo.
 
Mleta mada hujui itifaki za kitaasisi wewe.
Hata Mhe Samia hawezi kwenda kumpokea Mh Mpango Airport.
" Mwenyekiti (Mbowe)yupo wapi? Si mliniambia atakuwepo? Eeeeh.

 
Kaona aibu kama Adam alivyojifisha kwa Mungu baada ya kula tunda la katikati, kwa hiyo Mbowe na yeye keshalambishwa asali sasa anaona aibu ya kumpokea msaliti wa taifa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…