Kwanini mbuga ya Serengeti haiunufaishi mkoa wa Mara badala yake inainufaisha Arusha

Kwanini mbuga ya Serengeti haiunufaishi mkoa wa Mara badala yake inainufaisha Arusha

Mkoa una Ziwa ila umezubaa kama nini.
 
Mkoa wa Mara uliharibiwa na Mwl Nyerere mwenyewe. Enzi zake hakutaka kufanya jambo lolote kwenye mkoa huo, kwa kigezo cha kuonekana anapendelea kwao. Yaani hata barabara za lami tu hazikuwepo.

Hadi leo mkoa ule ni wa mwisho kwa kila kitu. Jambo litaanzia sehemu zote na Mara ndio itakuwa ya mwisho.
Asomaye na aelewe, natamani mngeiona Butiama.
 
Arusha inayo? Mbwiga
Ninavyokuheshimu hadi nimeduwaa kwa hiyo kauli.
Nikikushukuru nahisi sitapungukiwa kitu pia.
Ndio Arusha iko karibu na kia ni 45km to Arusha cc.
 
,uko serious kabisa na swali lako?

kwani kinachojengwa Dom kina faida gani ikiwa KIA na JNIA hazipati flights za kutosha?
Hakuna kiwanja cha ndege kinachojengwa Dodoma, naishi hapa ingewezekana kushea live location yangu ungeona! twende ukanionyeshe kinapojengwa swahiba

Acha ndoto za mchana huku kuna mvua tu za kipumbavu
 
Ninavyokuheshimu hadi nimeduwaa kwa hiyo kauli.
Nikikushukuru nahisi sitapungukiwa kitu pia.
Ndio Arusha iko karibu na kia ni 45km to Arusha cc.
Shida ni moja clearly ni ngumu kufika Musoma kwa flights ila inachukua masaa machache sana kufika Serengeti ukishafika Musoma!

Arusha kuna makampuni binafsi yenye videge vidogovidogo vingi ndicho kinachofanya watalii wasihangaike na Musoma
 
Nadharia yangu.

Mwl. Nyerere hakupenda kuupendelea Mkoa wa Mara
viongozi wengi waonatokea Mara waliogopa kuupendelea sababu ya mwalimu.
Wengi walishindwa hata kuendeleza Vijiji na nyumbani kwao kwa kumuogopa Mwalimu.
Hii tabia imeendelea hadi leo wana Mara hawapendi kuendeleza kwao/mkoani kwao.

Mwalimu hata familia yake hakuipendelea sembuse mkoa.
 
Sababu Arusha ina advantage, imekaa katikati ya Vivutio vya utalii zaidi ya Vinne.
Hii inafanya ipendelewe kwenye miundombinu sababu "Unaua ndege wengi kwa jiwe moja.
 
Magufuli ndo alikuwa anaenda kuufaidisha mkoa wa mara coz alikuwa na mpango wa kujenga airport kubwa ndani ya mbuka ya serengeti hivo watalii wangekuwa qanatua direct mbugani
 
Shida ni moja clearly ni ngumu kufika Musoma kwa flights ila inachukua masaa machache sana kufika Serengeti ukishafika Musoma!

Arusha kuna makampuni binafsi yenye videge vidogovidogo vingi ndicho kinachofanya watalii wasihangaike na Musoma
Jibu fupi...hakuna miundombinu ya utalii Musoma
 
Mambo mengine ni maamuzi binafsi ya MUNGU
Ujinga huu hakutoka kwa mtu mwingine ulitoka kwa Nyerere!
Hakuna wa kuja kukujengea! Mano mkoa wa morogoro vyuo kibao musoma hata kimoja hamna!
Mwl alifanya mazuri mengi ila alipaswa kufanya vitu vizuri pia nyumbani kwao!
Mpaka anatoka madarakani hospital ya mkoa hakumaliza yaani inasikitisha sana!
JPM ndo kaja kupambania lakini akina Heche wakinyanyuka ni kutukana Magufuli tu!
Pia watu wa Musoma wengi roho mbaya na kutopendana wao kwa wao!
 
Simiyu ni pori la akiba Kijereshi na Arusha hakuna sehemu ndani ya mkoa wa Arusha hifadhi ya Serengeti inafanya coverage na hifadhi ya Serengeti kwa mapana zaidi ipo ndani ya mkoa wa Mara. I stand to be corrected.
Serengeti upande wa Kusini Mashariki inakutana na Ngorongoro creater ambayo ipo ndani ya Arusha. Pia kaskazini Mashariki inakutana na Loliondo game controlled area ambayo nayo ni Arusha. Kwa hiyo Serengeti iko accessible vizuri tu tokea Arusha.
Upande wa Kusini Magharibi ya Serengeti inapakana na Maswa ambayo ni Simiyu na utalii wa wanyama wa Serengeti unafanyika sana huko hata Serikali inaplan kujenga uwanja mkubwa wa Ndege wa Simiyu huko Itilima ambayo ni wilaya mojawapo ya mkoa wa Simiyu inayopakana na Serengeti.

images (1).jpeg
 
Mkoa wa Mara uliharibiwa na Mwl Nyerere mwenyewe. Enzi zake hakutaka kufanya jambo lolote kwenye mkoa huo, kwa kigezo cha kuonekana anapendelea kwao. Yaani hata barabara za lami tu hazikuwepo.

Hadi leo mkoa ule ni wa mwisho kwa kila kitu. Jambo litaanzia sehemu zote na Mara ndio itakuwa ya mwisho.
Lete ushahidi kwamba mkoa wa Mara ni wa mwisho kwa kila kitu. Otherwise you shut up your dirty mouth!
 
Lete ushahidi kwamba mkoa wa Mara ni wa mwisho kwa kila kitu. Otherwise you shut up your dirty mouth!
Ndugu yangu hata kama sio wa mwisho ni mkoa mbovu sana na hakuna anayetamani kwenda kulaa Musoma!
Kwa kanda ya ziwa huwezi kuukuta mtu anahamia Musoma utakuta sanasana ni Mwanza ,kahama na Geita!
 
Wasaalam! Kwa fikra pana sana na hofu ya Mungu iliotukuka ningependa kulileta suala hili mbele yenu tulijadili kwa mapana zaidi bila ya chuki za ukanda wala ukabila.

Kwanini mbuga ya Serengeti haiunufaishi mkoa wa Mara?
Mara akuna hotel za maana za kufikia watali hizo hotel walipaswa wajenge watu binafsi na siyo serikali Arusha wazaliwa wa kanda hiyo wamejenga mahotel ya kifahari mara kutonufaika na mbuga sababu ni Wana mara wenyewe na Arusha kunufaika sababu ni wanaarusha kuona fursa
 
Back
Top Bottom