Kwanini Mchezaji akitoka Yanga kwenda Timu Nyingine Lazma Achemshe

Yaani Wawa na Onyango wanamuweka benchi Nondo na Lamine? Muwage serious....
 
Niyonzima ndiye anayenishangaza zaidi! Jamaa walitoa hela ndefu ya kumsajili na anakula bonge la mshahara! Ukiondoka Yanga kwa adabu kama Msuva huwezi shindwa huko uendako
Yanga inauza wachezaji waliochoka, wakati simba unauza wachezaji ambao bado wako kwenye 'form'.
 
Nadhani ni kwa sababu huwa wanajiko la gesi so kuchemsha inakuwa simple
 
Yanga ni Mpili watupu. Wanawaroga wachezaji.
Hii tabia waiache

Sent from my Infinix X612 using JamiiForums mobile app
 
Msuva alichemsha wapi?halafu domayo mbona azam alicheza kwa mafanikio tu
 
Kipimo cha mafanikio ni kipi?
Kibinafsi domayo alifanikiwa sana azam ila kitimu labda unaweza kusema akufanikiwa sababu hajawahi kushinda taji la maana zaidi ya mapinduzi cup,domayo alikiwasha sana azam mpaka mwaka juzi walipomuacha sababu ya kushuka kiwango na umri pia ushaanza kumuacha,kwa msuva alipokua al jadida alikiwasha hadi wydad wakamnunua kwa pesa nyingi wydad ile ilichukua baroka cup na klabu bingwa africa japokua msuva baadae alisusa na kurudi TZ sababu za kimaslahi,upande wa pili kuna chama na mikson nadhani unafahamu kilichowakuta
 
Msuva hakuchukua CAF Champions League na Wydad.

Wydad ya kina Msuva ilitolewa Semi final na Al Ahly na msimu uliofuata ilitolewa na Kaizer chiefs.
 
Sikuwa nafahamu kuwa ni tokea kitambo. Halafu wanamtukana Mayele.

Kweli lisemwalo lipo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…