Umeweka hapa hoja ya msingi sana siyo akienda Azam tu bali hata Simba...huo ndio ukweli na sijui kuna nini, binafsi huwa sielewi pia... historia inaonyesha hivyo...Ezeckiel Greyson ilikuwa hivyo aliwika Yanga miaka ya 70 na alipokwenda Simba ikawa nidyo mwisho wa enzi...wapo wengi tu akina Omari Hussein, Maulid Dilunga, Edibily Lunyamila na kadhalika na kadhalika...Baadhi yao kama akina Omari Hussein, Said Mwamba na Lunyamila na pia Mohammed Hussein walirudi tena Yanga na wakatulia...
Ila mchezaji akitoka Simba na kuja Yanga nyota yake huwaka maradufu...Kama akina Method Mogella, Yondan, Deo Munishi, Ajib na wengine wengi tu...
Ukiona mchezaji ametoka Yanga na kwenda Simba wewe mhurumie tu....ni sawa na wachezaji wa Arsenal wengi wao wakitoka timu hiyo na kwenda timu nyingine hucheza kwa msimu mmoja tu na kupotea...