Kwanini mkiwa wajawazito mnakuwa hivi?

Kwanini mkiwa wajawazito mnakuwa hivi?

pole sister
kutafuna barafu au kumumusa/kunyonya?
mm wangu alinitesa sana kwa mtoto wa pili nilifua kila kitu na kupika (msiniulize nilifua nini)
Kutafuna yaani nagandisha maji natafuna yakishaganda

Najisikia vizuuuri

Pole na hongera
Mie kuna kipindi nilishindwa kupika tulikula sana kwa mama ntilie[emoji16][emoji16]
 
Igiza wewe kama ni rahisi
Aaah hata mwenyewe mimba nshabeba ila sikufanya upuuzi huo,na kuna mda unatakiwa ujikaze siyo kujiendekeza we barafu sa nane za usiku ndo nini,mwenzio hata kutapika unaweza usijue kama huwa natapika kwa jinsi navojiweka na kazi nyingi nafanya mwenyewe
 
Nadhani mtakuwa wanawake mnatofautiana japo bado haijawa sababu ya kutomuondoa akajifungulie kwao
Mmh we dictator,au utakuwa na mchepuko wa kudumuu,ila mi sikubali yaani m nihangaike we umelala tu hapana lazima tuishi wote ili mara moja moja ujue uchungu wa mimba,maramoja moja nikuamshe hata sa saba za usiku wee
 
Kina mama nauliza,kwani ujauzito ni maradhi??
 
Mmh we dictator,au utakuwa na mchepuko wa kudumuu,ila mi sikubali yaani m nihangaike we umelala tu hapana lazima tuishi wote ili mara moja moja ujue uchungu wa mimba,maramoja moja nikuamshe hata sa saba za usiku wee
Nijue uchungu wa nini wakati wewe ndo umebeba hio mimba ni maumbile yenu yanataka iwe hivyo .acheni kutumia mimba kama kigezo cha kutuadhibu

Yaani lazima niondoe mtu kinguvu siwezi kubali ujinga
 
Nimeona kimfuko kimejaa limau za kutosha,kila mboga itakayopikwa lazima limao liwepo
 
Nijue uchungu wa nini wakati wewe ndo umebeba hio mimba ni maumbile yenu yanataka iwe hivyo .acheni kutumia mimba kama kigezo cha kutuadhibu

Yaani lazima niondoe mtu kinguvu siwezi kubali ujinga
Sasa anakuwa na tofauti gani na mtu alobebea mimba kwao yaan mimba haina mwenye nayo(tena mke kabisa m nsingeenda)
 
  • Thanks
Reactions: Cyb
Kwakweli hapa jibu halipo la moja Kwa moja.Kuna wengine kweli mimba zinawapelekea kutamani vitu flan flan,au vyakula flan haijalishi yupo wapi.Si tulikua na msichana alipata ujauzito akawa ananunua chipsi Kwa kujificha karibu kila siku.

Wapo ambao mimba hata haziwapekekeshi mwanzo mwisho.Kuna wale mimba zinwafanya watamani kula aina flani ya chakula Tu.Na sio kwamba mtu anajifanya inatokea Tu.Binafsi sikuwai kuwa mpenzi wa pepsi kabla ya mimba yangu ya Kwanza.Nilishangaa Tu siku moja nimeenda mahali kula nkakuta mtu anakunywa pepsi nikaitamani mpaka Leo.Soda yangu ilikua Fanta passion niliichukia hii soda siinywii tena mpaka Leo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Baadhi ya wanawake wakiwa wajawazito wanabadilika.Wife ujauzito wa kwanza alikua anataka mda mwingi anione.Kwa sasa ana ingine ila ananiponda mpaka namwambia au hiyo siyo yangu?hata niogeje utasikia unanuka.Kunipa misosi ameongeza kipimo cha kunijali.Hivi nyie kina mama mnaigizaga au mnayofanya mnamaanisha???
Afadhali ya wewe.....kaka yangu alihama kwake baada ya shemeji kuwa mjamzito kwa mara ya kwanza tu. Shemeji kila akimuona kaka alikuwa anamkimbiza na kisu eti alitaka kumuua kwa kumtesa na ujauzito. Sasa mtoto ana miaka 7 nyumba iko shwari kabisa, kama na shemeji wako na raha zao.
 
Kuishi na mke akiwa mjamzito Ni kazi sana
Wakwangu kila siku mara naumwa hiki mara kile
Mara na hamu na nyama choma ukileta anadonoa anacha
Mara sijisiki kufanya chochote
Mara nikifua naumwa
Nakisugue miguu sifikii
Mara we mbishi
Nipikie nkipika Mimi sitamani kula
Kila saa kunywa fruto
pole mkuu ila hapo anapotamani chakula fulani au kinywaji fulani hiyo ni hali ya kawaida kwa kinamama wajawazito ili kwa hivyo vingine naweza sema anaigiza au asiingize hiyo pia inachangiwa na wewe mwanaume wenda unamdekeza sana, ila naomba akihitaji kitu cha kula kama unauwezo umpatie lakn kama huna huwezo hata kiumbe kilichopo ndani anaona na mungu pia anaona lakn hayo mengine niwewe tu kupenda fanya maana nimeona wanawake wengi wakiwa wajawazito huwa wanapenda kuwajaribu waumezao kuona utafanyaje
 
Na hili nimelifuatilia kwa makini nimegundua kila kipindi na vituko vyake mfano mwanzo na Sasa Ni tofauti
Zamani (mimba changa )alikua akikosa samaki nazi machozi yanalenga
 
Kuishi na mke akiwa mjamzito Ni kazi sana
Wakwangu kila siku mara naumwa hiki mara kile
Mara na hamu na nyama choma ukileta anadonoa anacha
Mara sijisiki kufanya chochote
Mara nikifua naumwa
Mara Nikisugua miguu sifikii
Mara we mbishi
Mara leta mkono mtoto kacheza Sasa ivi
Mara Nipikie nkipika Mimi sitamani kula
Mara Kila saa kunywa fruto
N.K...............

😂😂😂
 
Back
Top Bottom