Kwanini mkiwa wajawazito mnakuwa hivi?

Kwanini mkiwa wajawazito mnakuwa hivi?

Hayo yote ni maigizo ya huko huko mjini, wamekuwa wakifundishana na kupania... sikuwahi kuyasikia vijijini!
Sasa akiniambia anajisikia vile au hivi nitabisha vipi mkuu?
Kazi tuliyobaki nayo Ni kuwatimizia tuuh
 
Sasa akiniambia anajisikia vile au hivi nitabisha vipi mkuu?
Kazi tuliyobaki nayo Ni kuwatimizia tuuh

Kwanini usibishe na kukemea, au ndo mahaba... basi utahenya huku mwenzio akikung’ong’a tu.
 
Kwanini usibishe na kukemea, au ndo mahaba... basi utahenya huku mwenzio akikung’ong’a tu.
Kwani kuna tatizo gani mkeo akikuhenyesha? Kuna kipindi hata wewe huwa unamhenyesha, punguza pride mkuu.

BTW, mwanaume akiweza kuishi na mke mjamzito bila kumchoka atakuwa na uwezo wa kushinda vikwazo vingi sana maishani, wajawazito wana namna yao ambayo sio ninyi wanaume mnawavumilia hata sisi wanawake wenzao tunawavumulia pia sababu tunaelewa, hata akikukwaza kuna muda unamsamehe tu.

Mimi nilirudi kazini nina njaa sana, nikafika home nikamkuta wifi yangu mjamzito, nilirudi na chips maana jioni vyakula home hakuna au vimeshakuwa viporo, ile nimenawa tu huyu hapa akang’ang’ania chips na mbaya zaidi anataka aile pekeake, nikampa nikapasha kiporo cha ugali dagaa na mchicha nikala. Nilimind kichini chini sababu akijua umemmind kisa chips zako anaweza kukuchukia hadi siku unajifungua.

Wajawazito sehemu nyingi sana wanavumiliwa makazini, sehemu zote za public sasa wewe mwenye ujauzito wako “mliofanyana” kwa starehe ukishindwa kumvumilia utakuwa huna utu.
 
binti kiziwi
Umewahi kuwa mjamzito?

Tupe ushuhuda wa kweli, the situation might be real but overrated... maigizo ni mengi kuliko uhalisia.
The situation is real na vingine tunajikaza navyo tu hatusemi, mfano mjamzito usiku anashindwa kulala kabisa we umelala na hakuamshi anakuacha tu ustarehe zako. Wengine hamu ya kufanya mapenzi huisha kabisa lakini hatakunyima miezi yote tisa kuna siku atakupa ikiwa yeye hajisikii chochote, utafanya huku ukimkera mwenzio, Mfano mwingine suala la harufu hapa huwa na balaa kila mjamzito kuna harufu lazima iwe inamsumbua, na harufu zenyewe hazikwepeki maana zinatuzunguka kwenye mazingira yetu, ukitapika sana mbavu zinauma zinabana yaani kila kitu shida. Kuna mengi mkuu.....

Lakini.... wanaowapania kuwatesa wanaume zao ujue huwa hawadekezwi kipindi sio wajawazito na wao wanakuwa wamepata pakuwabania, kama mtu ameshazoea kutreatiwa vizuri siku zingine sidhani kama anaweza kuwa na drama.
 
Ewe binti kiziwi
Maelezo yako ni matamu sana, too sweet words to be true.

Kunyima sex kipindi chote, mimba ni miezi miwili tu (7,8,9)... huwezi kuhesabu kuanzia 0-9 wakati hata shambani unaenda.

Na kwanini zisumbue mijini tu!

Swali la msingi, umewahi kuwa mjamzito?
 
Halafu wengi hutapika sana,cjui kwa nn
 
Ewe binti kiziwi
Maelezo yako ni matamu sana, too sweet words to be true.

Kunyima sex kipindi chote, mimba ni miezi miwili tu (7,8,9)... huwezi kuhesabu kuanzia 0-9 wakati hata shambani unaenda.

Na kwanini zisumbue mijini tu!

Swali la msingi, umewahi kuwa mjamzito?
Ndio mimi nimewahi, Una uhakika gani kuwa wanawake wa vijijini mimba haziwasumbui, Umewahi kuwa mjamzito kijijini? Au umeoa kijijini? Una wake wangapi ambao unaweza kuutumia uwingi wao kuthibitisha kuwa wanawake wa kijijini mimba haziwasumbui eti kwa sababu tu wanaenda shamba, hata wanawake wa mjini wanaenda makazini na kwenye biashara ninini unajaribu kuitengeneza kama hoja hapa?

Mimba ni miezi mingapi? Je umewahi kuwa mjamzito? Nauliza tena, uzoefu wangu unaniambia vipindi vyote vitatu vya ujauzito (trimesters) vina aina yake ya usumbufu, unasemaje kuhusu hilo.

Umeelewa ninavyoweka “exceptional” kwenye maelezo yangu? Nilikueleza kwa utaratibu na nikijaribu kutokujumuisha wanawake wote katika kundi moja. unaonekana huelewi, kwa sasa tunaweza kwenda sawa.
 
Naam binti kiziwi, here we go!

Hatushundani tunaeleweshana, kwa faida ya wengi... asante kwa uzoefu na uchambuzi wako.

Kutaja kwangu kijijini ni sawa tu na wewe ulivyotaja wanawake wa mjini, kama wanaweza kwenda makazini huwezi kutetea kuwa vipindi vyote ni 'mzigo' kwao... hiyo ndo hoja yangu.

Sote tunaelewa masaibu ya ujauzito, inajulikana na inaelezeka kitaalamu... hoja ya OP hapa mezani ni ile kudeka/usumbufu kwa mwanamme wake.

Hapa ndo inakuja tofauti ya uhalisia na maigizo, wengi imekuwa ni mkumbo na kukamia kisa tu ana mimba!

Mimba is nothing special, hata viumbe wengine hubeba mimba na wanapitia hali sawa sawa... lakini hawabagui majani ya kutafuna.
 
Naam binti kiziwi, here we go!

Hatushundani tunaeleweshana, kwa faida ya wengi... asante kwa uzoefu na uchambuzi wako.

Kutaja kwangu kijijini ni sawa tu na wewe ulivyotaja wanawake wa mjini, kama wanaweza kwenda makazini huwezi kutetea kuwa vipindi vyote ni 'mzigo' kwao... hiyo ndo hoja yangu.

Sote tunaelewa masaibu ya ujauzito, inajulikana na inaelezeka kitaalamu... hoja ya OP hapa mezani ni ule usumbufu kwa mwanamme wake.

Hapa ndo inakuja tofauti ya uhalisia na maigizo, wengi imekuwa ni mkumbo na kukamia kisa tu ana mimba!

Mimba is nothing special, hata viumbe wengine hubeba mimba na wanapitia hali sawa sawa... lakini hawabagui majani ya kutafuna.
Unapenda mno kuweka ujumuishi katika maelezo yako na hapo ndipo matatizo yanapoanzia.

Kwa heshima ya binadamu, naomba utengue mstari wako wa mwisho uliouandika, ni kweli mimba sio kitu special “especially ukiwa huibebi wewe” lakini angalau usifananishe hisia za binadamu na za mnyama asiye binadamu.
 
Ujumuishi ndo afya ya mjadala, kumbuka hapa hatujadili mtu mmoja mmoja au kundi fulani tu... hivyo naomba usichukulie kama tatizo.

Pia, binadamu kama wanyama wengine hubeba mimba kwa jinsi yao... haiondoi heshima wala utu wake kumlinganisha nao.

Kutaka tumuone spesho ni ubinafsi tu, lakini kihisia hana tofauti ukiacha kile mnaita 'utashi' sijui!

Naomba nisitengue kauli, labda unipe hoja yenye mashiko.

The fact that kuna wanaosumbua na wasiosumbua, tena wasiosumbua ni wengi kwa idadi... inatosha kuchukulia kuna uwezekano wa hao wasumbufu kutia chumvi. Japo wapo wa ukweli.

Je, hayo masaibu husababishwa na mazingira, mtindo wa maisha au ni genetically?
 
Ujumuishi ndo afya ya mjadala, kumbuka hapa hatujadili mtu mmoja mmoja au kundi fulani tu... hivyo naomba usichukulie kama tatizo.

Pia, binadamu kama wanyama wengine hubeba mimba kwa jinsi yao... haiondoi heshima wala utu wake kumlinganisha nao.

Kutaka tumuone spesho ni ubinafsi tu, lakini kihisia hana tofauti ukiacha kile mnaita 'utashi' sijui! Naomba nisitengue kauli, labda unipe hoja yenye mashiko.

The fact that kuna wanaosumbua na wasiosumbua, tena wasiosumbua ni wengi kwa idadi... inatosha kuchukulia kuna uwezekano wa hao wasumbufu kutia chumvi. Japo wapo wa ukweli.

Je, hayo masaibu husababishwa na mazingira, mtindo wa maisha au ni genetically?
Idadi ya wingi na uchache we unaipataje Kashaulo? Yaani umeipatia wapi? Unajibu kwa uhakika sana hata unanitisha, mimi nimekuwa nikijibu kuwa, wengine ndio wengine hapana hao ninao waita wengine binafsi sifahamu ni wengi au wachache.

Hilo swali la mwisho, Mimi nimezunguzia uzoefu kama mwanamke ambaye ninaishi na kuongea na wanawake wenzangu, swali hilo kwa mimi layman litakuwa gumu maana linahitaji mtaalamu kulijibu.
 
Kwa mtazamo huo huo wa kilayman, idadi sio muhimu sana hapa. Bora yako kuna wanawake umewahi kuongea nao, mimi ni fikira zangu tu.

Mjini vs Kijijini. Huku chips na vinono, kule udongo (pemba). Ile ya kumchukia au kumhitaji mwanamme ipo kote kote.

Kwa nukta hiyo basi, kama umekiri swali hilo ni la kitaalamu na huwezi kulijibu... naomba kuhitimisha kuwa hali hizo hutegemea zaidi MAZINGIRA na mfumo wa maisha.

Cheers [emoji276][emoji1635]
 
Back
Top Bottom