Ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Ila
Rebeca 83 mpenzi, najua utakuwa na elimu na una upeo, hebu basi tumia hiyo elimu na upeo kuwa reasonably right....
Sasa wewe hayo maneno ya Bible yanalenga single mothers au?!
Widow ni neno la English lenye maana ya mjane....
Kwa kiswahili mjane ni mwanamke aliyefiwa na mume wake halali wa ndoa takatifu. Hao ndio vitabu vya MUNGU huwa vinawalinda, maana sio sehemu ya dhambi ya uzinzi wao na watoto wao.
Mwanamke anapoolewa kwa ndoa takatifu akiwa na bikra yake huwa anapata ulinzi wa ki MUNGU yeye pamoja na uzao wake wa watoto na vijukuu....
Ukitaka kuprove hili tazama familia za zamani ambazo Baba anafariki na kumuacha mama analea watoto wake mwenyewe. Na hawa watoto wakaja kuwa wakubwa wakafunga ndoa vema tu kwa kuoa na kuolewa bila mushkeri na wakakuza familia imara ambazo nazo zikaja kupata watoto wenye hekima na uzao wa kushika maagizo ya MUNGU. Hiyo ni baraka ya ulinzi wa MUNGU katika maisha ya mjane na uzao wake...
Na ndio maana hata sheria za kiserikali na za kidini wakati wa mirathi humlinda mjane wa ndoa takatifu na watoto wake halali wa hiyo ndoa sio wa nje......
Sasa turudi kwenye neno single mothers....... Hili neno kama unavyoliona ni kitu kimesimama chenyewe, yaani ni mother kwa maana mwanamke aliyezaa watoto na ni single kwa maana ya ambaye hayupo katika mahusiano rasmi yaani ya ndoa... So aidha hana mahusiano ya wazi au analala na watu tofauti au ana mtu ila hajamhalalisha.
Single mother ilianza kutumia huko marekani kwenye jamii ya watu weusi (Black American) baada ya sheria za JIM CROW (Nenda kagoogle hili neno halafu soma maana yake, ilitokea 19th century huko na nadhani ilizimwa miaka ya 1965) kupitishwa na kuanza kuleta madhara especially kwa watu weusi ambao hizi sheria kwao hazikuwa na faida bali majanga.
Mojawapo ya majanga ni wanaume wa jamii ya watu weusi kuwekwa jera kwa sababu za kiuonevu bila kupewa nafasi ya kujitetea.
Hii ikazaa kizazi cha wanawake waliokuwa wanalala na kuzaa wanaume nje kipindi wanaume zao wakiwa jela, na mara wanaume wanapotoka nakukuta mke ana watoto ambao waliwachunguza tu na kugundua si wa kwao au waliwalea tu kishingo upande maana atadanganywa mtoto ni wako wengi wa hawa wanaume walitelekeza hawa wanawake na watoto na kuanza maisha mengine huko kando.
Hii ikazaa pandemic mpya kwa jamii ya watu weusi ya wanawake ambao mwanzo waliwaita single female parents ila baadae wataalamu wakasema mwanamke hawezi kuwa single parent kama mwenzake yupo hai na hawaishi pamoja bali huyo anakuwa ni single mother.
Pia wataalamu wa child welfare walihoji sana kuita wanawake wa kundi hilo kwa neno "single-female parents" ile hali wanawaacha watoto kulelewa na bibi zao au Nannies(yaya) au babysitters haitakuwa sawa na itakuwa ni degradation ya value ya wanawake wanaolea watoto wao wenyewe baada ya wanaume zao kufariki dunia.
So kutokea hapo hiyo term single mothers ikashika hatamu na kutumika kwa wanawake ambao kutokana na maamuzi yao ya kimazingira (sababu tofauti) waliamua kupata watoto wanaume zao wakiwa mbali.
Hiki swala likaja kuwa issue serikalini sababu kundi hili la wanawake waliokuwa wakizaa na wanaume tofauti wanaume zao wakiwa jela likaanza dai na kuomba kupewa msaada na kutoka serikalini unaoitwa "Welfare" support,(kwa hapa Tanzania tunaweza fanisha na TASAF) ambayo iliwasaidia kupata coupons special za kupata discount ya bei za chakula na mahitaji ya watoto kwenye masupermarket na hata kupewa coupon yenye thamani ya pesa ili aweze kuitumia kulipia mahitaji mbali mbali huko supermarket.
Hii ikaja kuongezewa na kitu kingine kinaitwa "child Support" ambayo kwasasa inatumika kuwawajibisha wanaume wote wenye watoto kulea watoto wao kwa kutoa pesa ya matunzo kwa lazima na asipotoa anakwenda jela kama felony convict.
Sasa hizi vitu zilipokuja ndipo zikazaa wave ya modern single mothers ambao kwa makusudi walizaa na wanaume kisha wanakwenda kuclaim "welfare" pamoja na childsupport mahakamani. Unakuta binti wa miaka 23 anawatoto 6 maana wanaanza kuzaa as early as 13 years younger kwa baadhi but most wakiwa 16 tayari unakuwa wanawatoto wawili au watatu na wataendelea.
Na watazaa na wanaume wa hovyo ili wapate sababu ya kuwashindwana nao na kuwanyima custody ya mtoto na kisha wanakwenda mahakamani kudai child support. Akiwa na watoto 5, then ni amount yake times watoto 5 anatumia ya katoto kamoja then ya watoto waliobakia anafanyia mambo yake kama kuvaa, kunua gari simu ya bei, kutokea out na kadhalika.
Hao ndo single mothers as how they are described by their definition. Sasa unapokuwa proud na hilo neno jiulize unajua asilia yake kimatumizi.....