Kwanini mnawahukumu mno single mothers?

Kwanini mnawahukumu mno single mothers?

Pengine anawakilisha tatizo lake. Alafu mkuu, kupata hela hakusababishi mtu aache kufikira matatizo ya wengine, maana bado ataendelea kuishi nao tu.
kama yanagusa moja kwa moja ila ukiwa busy huwezi hata kupoteza muda kufikiria mambo binafsi ya mtu mwingine ambayo hayana impacts kwako. hawa ni kama wale wanakaa vijiweni mtu akipita na gari wanaanza kumjadili
 
kama yanagusa moja kwa moja ila ukiwa busy huwezi hata kupoteza muda kufikiria mambo binafsi ya mtu mwingine ambayo hayana impacts kwako. hawa ni kama wale wanakaa vijiweni mtu akipita na gari wanaanza kumjadili
Kwahio tuwaache single mother wafanye wanavyotaka yaani wasikosolewe?
 
Kuwa single mother sio shida, shida ni kuwa single mother alafu mpumbavu.

Kuna jamaa yangu anamlilia single mother fulani amkubalie, yani anadai akimpata anatoa na mahali fasta apewe mchumba.
 
No comment!

Ila tupunguze kuwalaumu ndugu zangu ukibahatika mbona wapo single mother wanaojielewa sana.
 
Najua ushakataa mimba ya MTU tayari,kalee tu mkuu huwez jua labda atakukumbuka uzeeni
 
Single mother ni matokeo ya mwanamke kuchagua chagua kuwa selective sana mwanamme wakudate nae
 
Mtoa mada , unatakiwa kufahamu ya kuwa wengine wamefiwa na waume zao tena walikuwa ktk ndoa safiiiiiiiiiiiiiiiiiii, na sio unaemuaona ukadhani amemuacha mwanaume kuna wanawake wengi wameachwa na wanaume kwa tamaa za wanaume baaada ya kuona amemzalisha na uwezo wa kuhudumia hana mwanaume anakimbia anabaki mama na mwanae kwa hiyo usimuhukumu kila unaemuona ana mtoto lkn hana mume ua ameachana na baba wa mtoto wake , upo nyonyo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom