Kwanini Mo 'hatamuweza'Manara

Kwanini Mo 'hatamuweza'Manara

Kuna mambo nayafikiria, yananifanya nisiamini kuwa Manara amekosea ktk hili sakata.

Je ile tume sijui shirikisho la ushindani wa kimasoko/hisa lilikosea kuhoji uwekezaji wa Mo? Walikosea kuuliza Mo amekuwaje Mwenyekiti wa Simba? Yote yale waliyozungumza walikosea?

Tuachane na ile tume, vipi kuhusu Kigwangala? Aliwahi kuhoji mengi mno kuhusu uwekezaji wa Mo Simba.

Twende mbele turudi nyuma, tuweke shahada zetu na stashahada zetu mifukoni, tujadili hili. Simba imeperfom vyema michuano ya kimataifa na ndani pia. Ni kweli Simba imeendeshwa kwa hasara?

Yanga ambayo haina makombe, haijacheza michuano ya nje n.k imeweza tengeneza faida, sembuse Simba ambayo inapeak sana muda huu kuliko timu yoyote East Afrika?

Wakuu embu tuwekeni ushabiki pembeni na tuwe wawazi na wakweli ktk hili.
Mkuu umeuliza maswali manitowoc sana ila humu kuna watu kama akina GENTAMYCINE washapewa mrungula kutwa kucha wanakesha wanatetea utapeli wa Mo
 
Matajiri wanawababaisha watu wanaotoka shamba..
Ukiona mtoto wa mjini anaitisha Press Conference na anamshambulia tajiri wazi wazi bila woga na jina anamtaja ujue tayari
Tajiri kaingia kuminane .

Huyo Manara Mbona analia alindwe na serikali? Kayachezea anaogopa kuyaoga
 
Tukubali Manara kuna level alishafika huwezi kummaliza kirahisirahisi bila kupasua club. Kudeal na mtu kama Manara ni rahisi sana ila si kwa kumuundia skendo mbuzi.

Kitakachotokea ni kuvurugana na kutoaminiana na hapo mwisho wake ni MO kujitoa.

Kwa ufupi bila suluhu Simba haitobakia kama ilivyokuwa maana MO mwenyewe hana ngozi ngumu! Kama viongozi wa Simba wangeweza kufocus kwenye malengo yao na kuachana na kelele za Manara tungetoboa lakini sio hilo likitokea zaidi ya malumbano ambayo Haji atashinda tu.
Atashinda kwa lipi?
 
Mo a.k.a Mwamedi, kaifanya Simba klabu ya ukoo wake
Nasikia eti anataka kujiudhuru!!kwani watu hawaoni mazuri anayoyafanya!!yaani huyu ni mtu wa ajabu akitokea tu mtu, kusema kuwa kuna mambo hayako sawa, yeye anakimbilia kutishia kujiudhuru?!!
 
Yan hii ina matangazo ya mo hadi jina mchezaji ulioni halafu anadai anapata hasara!

Screenshot_20210804-145224_Instagram.jpg
 
Yan hii ina matangazo ya mo hadi jina mchezaji ulioni halafu anadai anapata hasara!

View attachment 1880274
Hahaaaaa!!!na ktk hesabu zake anazotoa ni kama simba haina chanzo cha mapato hata kimoja?!!!ukiuliza sana mashabiki lia lia wanakwambia hata aichuke bure tunachotaka ni furaha tu, hayajui kuwa anaweza akaitumia timu, akishaona tayari anawaachia timu yao!!wanarudi kule kule!!leo nasikia anataka kujiudhuru eti watu hawana shukrani!!!
 
Yaah hata mimi nakiona hicho kitu kwa huyu ndgu. Ukitaka kushindana nae kaa kimya usimjibu anajua kujitea mno atakudhalilisha.
Mo nae yule ni mtu wa kupanick atajibu tu kwa namna moja ama nyingine, alishangaza alivokua anapeana vijembe na kigwangala tusubiri vijembe kwa manara pia.
 
Tena wakijiroga kumjibu ndo wataharibu kila kitu, wakae kimya simba isipoteane
Hakuna wa kumjibu, alianza kabla ya Derby akajibiwa tuko busy na maandalizi ya mechi..

Akapost huko kwenye mitandao baada ya mechi tu jumatatu ataitisha press, labda alitishia akijua ataitwa, akapotezea. Majuzi baada ya Mo kuweka mzigo kapost tena akisifia kitendo cha mzigo kuwekwa, bado akapotezewa.

Ndio leo anakuja na hizo kelele za kitoto na kipuuzi. Kama alitumikishwa miaka yote hiyo bila mkataba kwanini aliendelea na kazi? Jibu ni rahisi, aliendelea na kazi sababu alikuwa anajitengenezea umaarufu na huo umaarufu kupitia Simba ulikuwa unamlipa, nani alikuwa anamjua Haji hapo kabla?? Angekuwa anapata hizo deals za GSM na AZAM kama sio Simba hii ya Dewji?

Wakati Simba inaenda trophy less miaka ile hizi deals anazozipata sasahivi alikuwa akizipata? Hivyo hakukua na sababu yeyote ya yeye kupiga kelele zote hizi anazopiga sasahivi.

Kitu kingine, Mo wala Babra hawana muda wa kujibishana nae, na baada ya muda mchache sana mtaona post zake za huko Mitandaoni zikibaki na comments sita mpaka ishirini. Watanzania ni watu wa zima moto tu, hawachelewi kukusahau upambane na hali yako. Leo Mbowe yupo mwenyewe gerezani hakuna aliyeandamana nae..
 
Mkuu umeuliza maswali manitowoc sana ila humu kuna watu kama akina GENTAMYCINE washapewa mrungula kutwa kucha wanakesha wanatetea utapeli wa Mo
Wewe unaumia nini kwa utapeli wa Mo pale Simba?
 
Back
Top Bottom