Kuna mambo nayafikiria, yananifanya nisiamini kuwa Manara amekosea ktk hili sakata.
Je ile tume sijui shirikisho la ushindani wa kimasoko/hisa lilikosea kuhoji uwekezaji wa Mo? Walikosea kuuliza Mo amekuwaje Mwenyekiti wa Simba? Yote yale waliyozungumza walikosea?
Tuachane na ile tume, vipi kuhusu Kigwangala? Aliwahi kuhoji mengi mno kuhusu uwekezaji wa Mo Simba.
Twende mbele turudi nyuma, tuweke shahada zetu na stashahada zetu mifukoni, tujadili hili. Simba imeperfom vyema michuano ya kimataifa na ndani pia. Ni kweli Simba imeendeshwa kwa hasara?
Yanga ambayo haina makombe, haijacheza michuano ya nje n.k imeweza tengeneza faida, sembuse Simba ambayo inapeak sana muda huu kuliko timu yoyote East Afrika?
Wakuu embu tuwekeni ushabiki pembeni na tuwe wawazi na wakweli ktk hili.