Kwanini Mo 'hatamuweza'Manara

Kwanini Mo 'hatamuweza'Manara

Sasa Mo ashindane na manara kwa lipi.

Manara yupo nje ya game tayari,labda apeleke vita za kuihujumu klabu kwa kuchukua fedha huko kisha aanze kuhonga wachezaji ama marefa.

Ila kwa mifumo iliyopo sio manara akifanikiwa hata moja.

Labda atulie abaki kama shabiki tu.
 
Wasije kulogwa wakajitokeza kumjibu, wataumbuka, niliona kwa page ya Diamond alipomuunga mkono na kusema kuwa hata yeye Dai alijiunga simba kwa ajili ya amsha amsha za Manara...alivimba balaa[emoji16]
Tukubali Manara kuna level alishafika huwezi kummaliza kirahisirahisi bila kupasua club. Kudeal na mtu kama Manara ni rahisi sana ila si kwa kumuundia skendo mbuzi.

Kitakachotokea ni kuvurugana na kutoaminiana na hapo mwisho wake ni MO kujitoa.

Kwa ufupi bila suluhu Simba haitobakia kama ilivyokuwa maana MO mwenyewe hana ngozi ngumu! Kama viongozi wa Simba wangeweza kufocus kwenye malengo yao na kuachana na kelele za Manara tungetoboa lakini sio hilo likitokea zaidi ya malumbano ambayo Haji atashinda tu.
 
Mimi ni mmoja wa watu ninaokubali kabisa kuwa Manara alikuwa 'very unprofessional' mara nyingi sana..
Na hata hiyo nafasi nimewahi Shauri Sana atolewe ..yeye na Jerry Muro niliwahi shauri watolewe wote huko nyuma..

Naweza sema Mimi sio mshabiki wa Manara ..lakini baada ya hili sakata
Nimegundua kitu kwa watu aina ya Manara...
Pascal Mayalla huwa anasema watu aina ya Manara 'wana hidden power'..

Hiki ndo nimekiona kwa Manara na naamini Mo hataweza kabisa kumzima Manara ..
Ukimtazama Manara anapoongea na historia yake yote utagundua kitu kimoja..
'passion'
Huoni 'Proffesionalism'..
Huoni 'ethics'
Huoni 'unafiki wala woga'
Manara siku zote amekuwa Manara
Anaishi kwa sheria zake ..lakini most important ana enjoy ushabiki wake..

Wanaosema nafasi ile inahitaji mtu more Proffesional wako sahihi lakin wanasahu kitu kimoja Tu..je mangapi hatuyafanyi ki Proffesional?
Wananchi watazoea hiyo Proffesionalism inayozungumzwa?
Utamaduni wetu na timu zetu za Kariakoo
Unaruhusu 'Proffesionalism' hiyo?

Au tunasahau na mashabiki wetu na mpira wetu watu kama Manara ndo haswaa wanazalishwa na kupendwa zaidi..?Pengo la Manara likijitokeza tutawapa nini mashabiki?
Manara alikuwa shabiki mkuu wa Simba zaidi kuliko mfanyakazi wa Simba..
Alikuwa maarufu kuliko yeyote Simba..
Hakupata hiyo kazi kwa kuomba
Aliombwa ...
Why watu wamtarajie aje a behave kama muajiriwa mwingine?..
Bado atabaki shabiki mkuu wa Simba kuliko Mo..hata kama hana title official hapo Simba...
Watu wenye passion na wako genuine bila kujali risks za kuwa open na genuine na wanayo ongea mara zote hushinda vita..
Manara ukimsikiliza anapoongea utaona
Anaongea kama mshabiki na sio kama muajiriwa..hajali lolote mradi anausikiliza moyo wake..Mo hatamuweza Manara..

Umeiweka vema!
 
Wasije kulogwa wakajitokeza kumjibu, wataumbuka, niliona kwa page ya Diamond alipomuunga mkono na kusema kuwa hata yeye Dai alijiunga simba kwa ajili ya amsha amsha za Manara...alivimba balaa[emoji16]

Avimbe tu simba ilikuwepo kabla ya uyo domo na mropokaji kuw maarufu
 
Tukubali Manara kuna level alishafika huwezi kummaliza kirahisirahisi bila kupasua club. Kudeal na mtu kama Manara ni rahisi sana ila si kwa kumuundia skendo mbuzi.

Kitakachotokea ni kuvurugana na kutoaminiana na hapo mwisho wake ni MO kujitoa.

Kwa ufupi bila suluhu Simba haitobakia kama ilivyokuwa maana MO mwenyewe hana ngozi ngumu! Kama viongozi wa Simba wangeweza kufocus kwenye malengo yao na kuachana na kelele za Manara tungetoboa lakini sio hilo likitokea zaidi ya malumbano ambayo Haji atashinda tu.
Stop kidding us, yani Mo aondoke Simba kwa sababu ya Manara?!

Manara aachwe aropoke akichoka atajifia mwenyewe, hana ukubwa wowote mnamkuza bure tu hapa, hana ubavu wa kuiharibu image ya klabu, matokeo uwanjani ndio kila kitu kwa mashabiki.

Vile atakavyoendelea kupiga kelele na hapatakuwepo wa wakumjibu ndio atachokwa haraka na hao wanaomsikiliza, na Simba SC sio wajinga waanze kulumbana na Manara, yule ni kama mtoto wa mtaani tu.
 
Kuna mambo nayafikiria, yananifanya nisiamini kuwa Manara amekosea ktk hili sakata.

Je ile tume sijui shirikisho la ushindani wa kimasoko/hisa lilikosea kuhoji uwekezaji wa Mo? Walikosea kuuliza Mo amekuwaje Mwenyekiti wa Simba? Yote yale waliyozungumza walikosea?

Tuachane na ile tume, vipi kuhusu Kigwangala? Aliwahi kuhoji mengi mno kuhusu uwekezaji wa Mo Simba.

Twende mbele turudi nyuma, tuweke shahada zetu na stashahada zetu mifukoni, tujadili hili. Simba imeperfom vyema michuano ya kimataifa na ndani pia. Ni kweli Simba imeendeshwa kwa hasara?

Yanga ambayo haina makombe, haijacheza michuano ya nje n.k imeweza tengeneza faida, sembuse Simba ambayo inapeak sana muda huu kuliko timu yoyote East Afrika?

Wakuu embu tuwekeni ushabiki pembeni na tuwe wawazi na wakweli ktk hili.
Hiyo report ya faida ya Yanga SC kama unayo tuwekee hapa tafadhali, tusijekuwa tunajadili story za mitaani.
 
Ataishia kupiga kelele mwisho wa siku atachoka na Simba Sc hatarudi.

Aende huko GSM au Azam sasa wakampe usemaji wa Yanga / Azam kwani lazima awe msemaji wa Simba SC

Ukiachwa achika sio kumganda mwenzio kama kupe.
IMG_20210805_005346.jpeg
 
Kuna mambo nayafikiria, yananifanya nisiamini kuwa Manara amekosea ktk hili sakata.

Je ile tume sijui shirikisho la ushindani wa kimasoko/hisa lilikosea kuhoji uwekezaji wa Mo? Walikosea kuuliza Mo amekuwaje Mwenyekiti wa Simba? Yote yale waliyozungumza walikosea?

Tuachane na ile tume, vipi kuhusu Kigwangala? Aliwahi kuhoji mengi mno kuhusu uwekezaji wa Mo Simba.

Twende mbele turudi nyuma, tuweke shahada zetu na stashahada zetu mifukoni, tujadili hili. Simba imeperfom vyema michuano ya kimataifa na ndani pia. Ni kweli Simba imeendeshwa kwa hasara?

Yanga ambayo haina makombe, haijacheza michuano ya nje n.k imeweza tengeneza faida, sembuse Simba ambayo inapeak sana muda huu kuliko timu yoyote East Afrika?

Wakuu embu tuwekeni ushabiki pembeni na tuwe wawazi na wakweli ktk hili.
Kwa vile mashabiki wa Simba ni mbumbumbu huwa hawajishughulishi kuuliza vitu vigumu utawasikia imradi timu inashinda basi wao mashabiki wa Simba wanataka matokeo tu ya uwanjani na Kanji kawawini sana kwa hilo naye anapitia humo humo kutangaza bidhaa zake hawana ubavu wa kuhoji mkataba wowote unaotangaza bidhaa za mo kupitia klabu ya Simba ndio maana Rage hakukukosea kuita mambumbumbu
 
Back
Top Bottom