Mimi ni mmoja wa watu ninaokubali kabisa kuwa Manara alikuwa 'very unprofessional' mara nyingi sana. Na hata hiyo nafasi nimewahi Shauri Sana atolewe ..yeye na Jerry Muro niliwahi shauri watolewe wote huko nyuma.
Naweza sema Mimi sio mshabiki wa Manara lakini baada ya hili sakata. Nimegundua kitu kwa watu aina ya Manara...
Pascal Mayalla huwa anasema watu aina ya Manara 'wana hidden power'..
Hiki ndo nimekiona kwa Manara na naamini Mo hataweza kabisa kumzima Manara. Ukimtazama Manara anapoongea na historia yake yote utagundua kitu kimoja.
'passion'
Huoni 'Proffesionalism'..
Huoni 'ethics'
Huoni 'unafiki wala woga'
Manara siku zote amekuwa Manara
Anaishi kwa sheria zake ..lakini most important ana enjoy ushabiki wake..
Wanaosema nafasi ile inahitaji mtu more Proffesional wako sahihi lakin wanasahu kitu kimoja Tu..je mangapi hatuyafanyi ki Proffesional?
Wananchi watazoea hiyo Proffesionalism inayozungumzwa?
Utamaduni wetu na timu zetu za Kariakoo
Unaruhusu 'Proffesionalism' hiyo?
Au tunasahau na mashabiki wetu na mpira wetu watu kama Manara ndo haswaa wanazalishwa na kupendwa zaidi..?Pengo la Manara likijitokeza tutawapa nini mashabiki?
Manara alikuwa shabiki mkuu wa Simba zaidi kuliko mfanyakazi wa Simba.
Alikuwa maarufu kuliko yeyote Simba.
Hakupata hiyo kazi kwa kuomba.
Aliombwa.
Why watu wamtarajie aje a behave kama muajiriwa mwingine?
Bado atabaki shabiki mkuu wa Simba kuliko Mo hata kama hana title official hapo Simba.
Watu wenye passion na wako genuine bila kujali risks za kuwa open na genuine na wanayo ongea mara zote hushinda vita.
Manara ukimsikiliza anapoongea utaona.
Anaongea kama mshabiki na sio kama muajiriwa hajali lolote mradi anausikiliza moyo wake..Mo hatamuweza Manara..