Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
Sooth,Mohamed Said, nakuheshimu kwa umri wako lakini kwa msimamo wako kuhusu ukristo na wakristo napata shida sana kukuheshimu. Mimi nimekufuatilia maandiko yako mengi hapa Jukwaani, nakuona kama mtu unayetafuta cheche kwenye bwawa la petroli.
Huna nia ya kuwaunganisha watanzania. Huna nia ya kuwaelemisha wasio waislamu masahibu (kama yapo) yanayowakumba waislamu. Usidhani kila asiye muislam ni adui wa uislam. Mimi huko bara nilikokulia sikuwahi kusikia wala kumuona muislamu. Muislam nimekuja kukutana naye shule, tena alipojitambulisha nilidhan uislam ni kabila maana daras zima tulijitambulisha kwa makabila yetu. Hivyo sikulelewa kuuchukia uislam maana sikuufaham. Sasa wewe hili unalisahau, unadhan wasio waislam wote wanaujua uislam na wanauchukia.
Msimamo wangu, kama kuna jamii ya kitanzania inaamini inakandamizwa au kudhulumiwa, basi njia sahihi ya kutatua tatizo ni kuwafanya watu wote waelewe tatizo na washiriki kulipatia ufumbuzi. Siamin ktk 'us against them strategy' ambayo wewe hupenda kuitumia. Pia wewe hauko rational-kuna wakati uliwahi kulalamika wabunge waislamu kuwa wachache ndani ya bunge na ukataka pawepo usawa. Sasa ukitaka usawa wakati kwa asilimia zaid ya 70 wabunge huchaguliwa na wananchi-hawateuliwi na mtu, huwa napata shida sana kukuelewa. Are you after affirmation or revenge?
Njoo na ushahidi kwa hizi tuhuma.
Historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika ilivurugwa kwa makusudi kwa hofu
ya bure kuhusu Uislam na Waislam.
Nimeiandika historia hii na kkitabu kimechapwa.
Nimefanya na mihadhara ndani na nje ya Tanzania kwa mialiko ya wanaotaka
kujua ukweli.
Mada nilizowasilisha ndani na nje ya nchi zipo na kitabu nilichoandika kipo na
kimeshachapwa matoleo kadhaa.
Sijasikia popote pale kuwa kuna mtu katukanwa kisa kitabu cha Mohamed Said.
Hayo mengine sitakupa jibu mimi majibu watakupa Bergen (1981) na Sivalon
(1992)