Ukishasema kuna barua, kama ni muwazi, una wajibu wa kuelezea yaliyomo katika barua hiyo, hususan kama barua ni ya magwiji, inahusu makubwa na ulitakiwa kusema hayo na watu unaowaheshimu waliotangulia.
Usiposema, utakuwa umewakosea heshima.
Pia, utakuwa unatukosea heshima uliotuambia kuna barua halafu hutaki kutuambia imesemaje. Bora usingetuambia kabisa.
Pia, kuna wengine watakuona mzushi tu, kwa sababu kila mtu anaweza kujifaragua "nimepokea barua kutoka kwa Papa Francis wa Wakatoliki leo, jana nilipokea ya Obama, sina hata muda wa kuzijibu".
Kila mzushi anaweza kusema hivyo. Ili ujitenganishe na wazushi hawa, ama usitaje kaabisa kitu ambacho hupo tayari kukijadili kwa kina ama kitaje na kijadili kwa kina.
"Put up or shut up" wanasema Waingereza.