Kwanini Mohammed Said hakupewa nafasi kwenye msiba wa Ally Sykes?

Sooth,
Njoo na ushahidi kwa hizi tuhuma.

Historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika ilivurugwa kwa makusudi kwa hofu
ya bure kuhusu Uislam na Waislam.

Nimeiandika historia hii na kkitabu kimechapwa.

Nimefanya na mihadhara ndani na nje ya Tanzania kwa mialiko ya wanaotaka
kujua ukweli.

Mada nilizowasilisha ndani na nje ya nchi zipo na kitabu nilichoandika kipo na
kimeshachapwa matoleo kadhaa.

Sijasikia popote pale kuwa kuna mtu katukanwa kisa kitabu cha Mohamed Said.

Hayo mengine sitakupa jibu mimi majibu watakupa Bergen (1981) na Sivalon
(1992)
 
Sooth,
Njoo na ushahidi kwa hizi tuhuma.
(1992)
Kwan hapa mahakamani? Kama wataka kuyakana maneno yako mwenyewe, hewala. Sisi wengine hatutakubali upotoshe jamii ya kitanzania maana tuna watoto ambao tunapaswa kuwaachia nchi salama kama tulivyoikuta.
 
Sooth,

Hayo mengine sitakupa jibu mimi majibu watakupa Bergen (1981) na Sivalon
(1992)

Mimi niko open-minded, nitavisoma nikipata wasaa. Lakini pia nikutaarifu nimkisoma 'Mwembechai Killings' cha Njozi ambaye nae amemquote sana Sivalon. Pia nimesoma 'The Darkside of Nyerere Legacy' ambacho pia ni kitabu chenu pendwa. Tatizo linakuja pale mnapokuja na 'us vs them strategy', hapo huwa nawapuuza.
 
Mkuu hujawahi kuwahoji wakristo au ha wapagani waliokuwa vinara katika harakati za kudai Uhuru?
 
Kwan hapa mahakamani? Kama wataka kuyakana maneno yako mwenyewe, hewala. Sisi wengine hatutakubali upotoshe jamii ya kitanzania maana tuna watoto ambao tunapaswa kuwaachia nchi salama kama tulivyoikuta.
Sooth,
Nadhani wewe ni mgeni hapa jamvini.

Wengi walianza kama wewe kuwa naandika historia ya uongo kama unavyosema
wewe kuwa napotosha.

Ikiwa wewe hukubali mimi ''kupotosha,'' njia ya kunikabili na uongo wangu si vitisho.
Njia ni wewe kuja na ukweli.

Huo usalama ni jukumu la kila mtu.
Umefanya haraka kuja kutaka kubishana na mimi.

Chukua muda usome kwanza hizo hizo rejea nilizokuwekea.
Kuna mengi utajifunza.

Historia hii haitaki haraka ndugu yangu.
Uliza hapa jamvini utaelezwa.

Kila aliyesimama na mimi katika historia hii amekimbia.

Hii historia niliyoandika na hizo video unazoangalia ndiyo ukweli wa historia ya nchi
yetu.

Ukitaka kujua zaidi msome Njozi (2002).
Yeye alisherehesha yale waliyoandika Bergen na Sivalon.

Nadhani unajua kuwa serikali ilitishika na ukweli katika kitabu cha Njozi na kikapigwa
marufuku.

Haya yote tushajadili sana hapa jamvini ni bahati mbaya wewe hukuwepo.

Katika jamvi hili hatuna kawaida ya kutishana na ndiyo unaniona mimi sijajificha naandika
kwa jina langu halisi sababu ninachosema ni kweli sina sababu ya kuogopa ukweli.
 
Sooth,
Ukitupuuza sawa hakuna wa kukulazimisha.
Hapa hukuitwa na mtu.

Umekuja kwa khiyari yako mwenyewe na utaondoka kwa khiyari yako mwenyewe.
 
Sooth,
Ukitupuuza sawa hakuna wa kukulazimisha.
Hapa hukuitwa na mtu.

Umekuja kwa khiyari yako mwenyewe na utaondoka kwa khiyari yako mwenyewe.
Tatizo la 'us vs them' ndio lililopelekea mgogoro wa nani achinje ng'ombe. Ni dhahiri hakukuwa na mshindi. Ilisaidia kutambua kuwa tunategemeana. Kwahiyo kukupuuza maana yake, sitakuunga mkono ktk unachoshadidia. Nitakupinga kila nitakapopata nafasi.
 
Mohamed Said wewe ni mlalamishi (whiner), hujawahi kuja na suluhisho la masahibu ya watu wako. Kama utakumbuka wakati wa uchaguzi mkuu ulikuwa bize na sideshows na mimi nikakushauri nguvu zako uzielekeze ktk kuhakikisha tunapata viongozi watakaosimamia haki na sheria kwa watu wote. Hukunisikia. Rais anaapisha mawazi ukawa wa kwanza kumpinga Ndalichako. Ungekuwa smart ungefanya kampeni ya kukiondoa hicho chama ulichosema mlikitumia kuleta uhuru ili muwape wengine wanaoweza kusikiliza kero zenu.
 
Mzee wangu mm hua na kuelewa sana, namuomba Allah akupe umri mrefu na mwisho mwema. Ama kweli ukweli mchungu!!
 
Sooth,
Toka awali nilijua hutofika mbali na mimi.
Fungua uzi mwingine In Shaallah nitakuja.

Hii mada mpya uloleta hapa si kwake.
 
Tatizo la 'us vs them' ndio lililopelekea mgogoro wa nani achinje ng'ombe. Ni dhahiri hakukuwa na mshindi. Ilisaidia kutambua kuwa tunategemeana. Kwahiyo kukupuuza maana yake, sitakuunga mkono ktk unachoshadidia. Nitakupinga kila nitakapopata nafasi.
Sooth,
Uwezo wa kupambana na mimi huna.
 
Sooth,
Toka awali nilijua hutofika mbali na mimi.
Fungua uzi mwingine In Shaallah nitakuja.

Hii mada mpya uloleta hapa si kwake.
Katika jamii ya kiislam, wewe kama sheikh Ponda mna influence kubwa sana. Sasa sisi wengine tunashauri hiyo influence inaweza ikatumika kwa mafanikio ya wengi na kutoa suluhisho la kudumu la kile mnacholilia.
 
Sooth,
Uwezo wa kupambana na mimi huna.
Tatizo liko hapo. Unapenda mapambano na watu-hasa wasio wa imani yako. Mimi napambana na umaskini na ujinga. Kama kuna ulazima wa kupambana, mi nitapambana na hoja zako uchwara.
 
Mzee Mohamed naomba siku utuwekee hizo barua za Chief Marealle japo nami niweze kumfahamu kidogo. Ni jirani yangu pale Marangu
 
Mzee Mohamed naomba siku utuwekee hizo barua za Chief Marealle japo nami niweze kumfahamu kidogo. Ni jirani yangu pale Marangu
Kinyungu,
Hizi barua siwezi kueleza, ''content'' ingawa marehemu Ally Sykes alitaka
nieleze katika kitabu cha Abdul Sykes nini Marealle amesema kuhusu watu
fulani.

Lakini leo nikiangalia nyuma yale ambayo Chief Marealle alimuonya rafiki
yake ndiyo yaliyokuja kumfika Ally Sykes na kaka yake baada ya uhuru.

Tosheka na haya.
 
Tatizo liko hapo. Unapenda mapambano na watu-hasa wasio wa imani yako. Mimi napambana na umaskini na ujinga. Kama kuna ulazima wa kupambana, mi nitapambana na hoja zako uchwara.
Sooth,
Mbona sasa unakuja na matusi?

Ikiwa huwezi kustahamili ''contrary views,'' basi na tusitishe
huu mnakasha.

Hapana sababu ya kutukanana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…