Zanzibar-ASP
JF-Expert Member
- Nov 28, 2013
- 11,550
- 40,697
Kupitia video inayotembea mitandaoni, mkuu wa mkoa wa Dar, ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama, Albert Chalamila amesikika akitoa kauli hizi tatu kwa ujasiri mkubwa;
1. Amekiri, kujitamba, kujivunia na kujipongeza kwa kuua? mtuhumiwa wa wizi aliyeingia nyumbani kwake mkoani Iringa
2. Amewahamisha wananchi kuua mara moja mtuhumiwa yoyote wa wizi wa kuvunja na kuingia ndani ya nyumba.
3. Ametoa amri na maelekezo kwa Polisi kuua mara moja mtuhumiwa yoyote anayevunja nyumba na kuingia ndani kwa dhumuni la kuiba.
Alichokema Chalamila kuhusu wezi soma:
Kwahiyo hapa RC Chalamila alihalalisha watu kuua tena, aagiza Polisi wafanye hilo waziwazi
Sababu za Chalamila kutoa kauli hiyo ni kutokana na kujenga dhana ya kuhisi kuwa dhamira ya mwizi wa namna hiyo huwa ni kutaka kumuua mwenye mali na upande wa pili kuponguza msongamano usiokuwa na sababu magerezani.
Sasa kwa kuwa kauli hiyo iko kinyume cha katiba, sheria na haki za binadamu ambapo mkuu wa mkoa alipaswa kuwa kinara wa kuzilinda na kuzisimamia, kupitia hapa JF tunahoji, kwanini mpaka sasa mkuu wa mkoa wa Dar yupo ofisini, na kwanini vyombo husika vya usalama vimeshindwa kumchukulia hatua za kumkamata na kumhoji?