Kwanini mtu ukiwa unatekeleza majukumu yako ya kiofisi unaonekana ni mwenye kiherehere?

kyagata

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2016
Posts
13,966
Reaction score
26,220
Kufanya kazi na Watanzania ni changamoto sana kwa kweli.

Labda mnisaidie kuelewa, muda si mrefu nimeingia ofisini hapa kuanza majukumu yangu ya siku.

Nimefika tu, kuna chawa wangu mmoja akaniletea kaumbea kuwa kwenye kikao chao cha idara yao huko, kuna mtu amenizungumzia kuwa nawabana sana na siwapi ushirikiano wa kutosha.

Nikakumbuka, siku chache zilizopita hao wanaosema nawabana na siwapi ushirikiano walikuwa na field trip huko mikoani. Walipewa kiasi kikubwa tu cha pesa za safari, na kama ilivyo kawaida ya kila ofisi ina utaratibu wake. Watu wanapotoka field trip basi lazima wafanye retirement, na sisi hapa ofisini kwetu kila kitu kinafanyika online kwenye system ya taasisi husika. Miongozo iliyopo iko wazi kwamba risiti pekee zinazokubalika wakati wa kufanya retirement ni EFD receipts only. Kama mtu alienda kulala kwa hawara yake na siyo hotelini, basi afanye kila linalowezekana apate EFD receipt.

Sasa, kuna mtu anajifanya ni mkongwe wa taasisi, kwa hiyo baadhi ya mambo anataka tufanye business as usual. Katoka trip, kaja kufanya retirement, kaweka risiti za kuandikwa kwa mkono. Kweli, karne hii kuna hoteli ya hadhi ya nyota tatu inatoa risiti za mkono, wakuu?

Ile retirement yake mimi nimeipiga pini; nimeikataa na nimempa sababu kuwa haijacomply na matakwa ya taasisi. Hivyo nimempa siku tatu mbele aweze kutafuta documents halali. Wenzie wote wamefanya hilo zoezi vizuri, ingawa najua risiti nyingi zimetengenezewa Kariakoo tu hapo, ila nimefumba macho tu. Sasa huyu mmoja aliyeniwekea mirisiti ya kuandikwa kwa mkono ndie ananizungumzia vibaya huko kwa mavikao yao.

Hivi, kwa nini hapa Bongo mtu ukitekeleza majukumu yako unaonekana kama snitch, wakuu?
 
Kufanya kazi na watanzania ni changamoto sana kwa kweli.
Labda mnisaidie kuelewa,muda si mrefu nimeingia ofisini hapa kuanza majukumu yangu ya siku.

Nimefika tu kuna chawa wangu mmoja akaniletea kaumbea kuwa kwenye kikao Chao cha idara yao huko kuna mtu amenizungumzia kuwa nawabana sana na siwapi ushirikiano wa kutosha.

Nikakumbuka siku chache zilizopita hao wanaosema nawabana na siwapi ushirikiano walikua na field trip huko mikoani.walipewa kiasi kikubwa tu cha pesa za safari,na kama ilivyo kawaida ya kila ofisi ina utaratibu wake, watu wanapotoka field trip basi lazima wafanye retirement, na sisi hapa ofisini kwetu kila kitu kinafanyika online kwenye system ya taasisi husika,miongozo iliyopo iko clear kwamba risiti pekee zinazokubalika wakti wa kufanya retirement ni efd receipts only,kama mtu alienda kulala kwa hawara yake na sio hotelin basi afanye kila linalowezekana apate efd receipt.

Sasa kuna mtu yeye anajifanya ni mkongwe wa taasisi kwa hiyo baadhi ya mambo anataka tufanye business as usual,katoka trip kaja kufanya retirement kaweka risiti za kuandikwa na mkono,kweli karne hii kuna hotel ya ya hadhi ya nyota tatu inatoa risiti za mkono wakuu?

Ile retirement yake mimi nimeipiga pini nimeikataa nimempa reasons kuwa haijacomply na matakwa ya taasisi hivyo nimempa siku 3 mbele aweze kutafuta documents halali.wenzie wote wamefanya hilo zoezi vizuri ingawa najua risiti nyingi zimetengenezewa kariakoo tu hapo ila nimefumba macho tu.sasa huyu mmoja aliyeniwekea mirisit ya kuandikwa kwa mkono ndo ananizungumzia mbovu huko kwa mavikao yao.

Hivi kwa nini hapa bongo mtu ukitekeleza majukumu yako unaonekana kama snitch wakuu?​
Uzalendo hamna mtu unapambana hulali uko macho unasema unapambania taifa mwisho wa siku boss anakwambia acha umbea 🥲🥲🥲
 
Hivi kwa nini hapa bongo mtu ukitekeleza majukumu yako unaonekana kama snitch wakuu?
Wewe ndio wale Wahuni wakiwa wanakula bangi zao wakianza kukuzungumzia utasikia unamuongelea yule dogo kyagata yule dogochoko sana, funika kombe mwanaharamu apite mweke chini mpe ABC za jinsi wenzake wamefanya afanye hivyo usikaze tu the extent aanze kukuona wewe km mchawi unamuwangia
 
Kufanya kazi na Watanzania ni changamoto sana kwa kweli.

Labda mnisaidie kuelewa, muda si mrefu nimeingia ofisini hapa kuanza majukumu yangu ya siku.

Nimefika tu, kuna chawa wangu mmoja akaniletea kaumbea kuwa kwenye kikao chao cha idara yao huko, kuna mtu amenizungumzia kuwa nawabana sana na siwapi ushirikiano wa kutosha.

Nikakumbuka, siku chache zilizopita hao wanaosema nawabana na siwapi ushirikiano walikuwa na field trip huko mikoani. Walipewa kiasi kikubwa tu cha pesa za safari, na kama ilivyo kawaida ya kila ofisi ina utaratibu wake. Watu wanapotoka field trip basi lazima wafanye retirement, na sisi hapa ofisini kwetu kila kitu kinafanyika online kwenye system ya taasisi husika. Miongozo iliyopo iko wazi kwamba risiti pekee zinazokubalika wakati wa kufanya retirement ni EFD receipts only. Kama mtu alienda kulala kwa hawara yake na siyo hotelini, basi afanye kila linalowezekana apate EFD receipt.

Sasa, kuna mtu anajifanya ni mkongwe wa taasisi, kwa hiyo baadhi ya mambo anataka tufanye business as usual. Katoka trip, kaja kufanya retirement, kaweka risiti za kuandikwa kwa mkono. Kweli, karne hii kuna hoteli ya hadhi ya nyota tatu inatoa risiti za mkono, wakuu?

Ile retirement yake mimi nimeipiga pini; nimeikataa na nimempa sababu kuwa haijacomply na matakwa ya taasisi. Hivyo nimempa siku tatu mbele aweze kutafuta documents halali. Wenzie wote wamefanya hilo zoezi vizuri, ingawa najua risiti nyingi zimetengenezewa Kariakoo tu hapo, ila nimefumba macho tu. Sasa huyu mmoja aliyeniwekea mirisiti ya kuandikwa kwa mkono ndie ananizungumzia vibaya huko kwa mavikao yao.

Hivi, kwa nini hapa Bongo mtu ukitekeleza majukumu yako unaonekana kama snitch, wakuu?
Naona sasa umeandika vizuri au mods wamekusaidia kuEdit ? maana mwanzo ulibandanisha kama chapati bila hata Aya hadi nikaona uvivu kusoma nikataka nikutukane.
 
Punguza unoko kazini dogo.

Simamia misingi ya kazi yako kweli ila usipanie sana kama unavyofanya inaonekana hata waliokuletea risiti za kariakoo zimekuuma sana.
 
Timiza majukumu yako kwa mujibu wa sheria za taasisi husika,

Issue ya wao kukuongelea vibaya,wewe haikuhusu,tena hata huyo unayemuita chawa wako anayekuletea umbea unatakiwa umpige marufuku kukuletea umbea,

Kama hata wewe una chawa wa kukuletea umbea,basi sioni tofauti yeyote kati yako na hao uliokuja kuwasema hapa.
 
Huyo ni bwege. Ila kingine, nyie wahasibu mna wivu sana na watu wa program mnahisi wanapiga sana ela kuwazidi ndio mana mnakuwaga wanoko wanoko. Mimi ni mtu wa program
 
Ni kweli ni kiherehere maana katika utekelezaji wenu mnakuwa na viherehere, unaweza kutekeleza majukumu yako vizuri tu na taratibu bila kukanyaga mtu
 
Katika kila kazi kaa ukijua hakuna anae weza kuvaa viatu vyako, na kila mtu hua anafanya mambo kurahisisha upande wake.

Sasa we cheka nao, siku likikuibukia Hakuna wa kusimama na WW.
 
Kufanya kazi na Watanzania ni changamoto sana kwa kweli.

Labda mnisaidie kuelewa, muda si mrefu nimeingia ofisini hapa kuanza majukumu yangu ya siku.

Nimefika tu, kuna chawa wangu mmoja akaniletea kaumbea kuwa kwenye kikao chao cha idara yao huko, kuna mtu amenizungumzia kuwa nawabana sana na siwapi ushirikiano wa kutosha.

Nikakumbuka, siku chache zilizopita hao wanaosema nawabana na siwapi ushirikiano walikuwa na field trip huko mikoani. Walipewa kiasi kikubwa tu cha pesa za safari, na kama ilivyo kawaida ya kila ofisi ina utaratibu wake. Watu wanapotoka field trip basi lazima wafanye retirement, na sisi hapa ofisini kwetu kila kitu kinafanyika online kwenye system ya taasisi husika. Miongozo iliyopo iko wazi kwamba risiti pekee zinazokubalika wakati wa kufanya retirement ni EFD receipts only. Kama mtu alienda kulala kwa hawara yake na siyo hotelini, basi afanye kila linalowezekana apate EFD receipt.

Sasa, kuna mtu anajifanya ni mkongwe wa taasisi, kwa hiyo baadhi ya mambo anataka tufanye business as usual. Katoka trip, kaja kufanya retirement, kaweka risiti za kuandikwa kwa mkono. Kweli, karne hii kuna hoteli ya hadhi ya nyota tatu inatoa risiti za mkono, wakuu?

Ile retirement yake mimi nimeipiga pini; nimeikataa na nimempa sababu kuwa haijacomply na matakwa ya taasisi. Hivyo nimempa siku tatu mbele aweze kutafuta documents halali. Wenzie wote wamefanya hilo zoezi vizuri, ingawa najua risiti nyingi zimetengenezewa Kariakoo tu hapo, ila nimefumba macho tu. Sasa huyu mmoja aliyeniwekea mirisiti ya kuandikwa kwa mkono ndie ananizungumzia vibaya huko kwa mavikao yao.

Hivi, kwa nini hapa Bongo mtu ukitekeleza majukumu yako unaonekana kama snitch, wakuu?
Wahasibu na ma HR kusema ukweli mna kauzinguaji fulani muwapo makazini, mnapenda taratibu, sera na sheria za taasisi ila sio well being ya mfanyakazi, mnatska wajibu ila sio haki
 
Maneno yako kwake yangekua machache tu naomba risiti za EFD basi, hayo mawazo ya hata kama wametoa kariakoo sijui wapi wapi sio jambo lako kabisa.
 
Kufanya kazi na Watanzania ni changamoto sana kwa kweli.

Labda mnisaidie kuelewa, muda si mrefu nimeingia ofisini hapa kuanza majukumu yangu ya siku.

Nimefika tu, kuna chawa wangu mmoja akaniletea kaumbea kuwa kwenye kikao chao cha idara yao huko, kuna mtu amenizungumzia kuwa nawabana sana na siwapi ushirikiano wa kutosha.

Nikakumbuka, siku chache zilizopita hao wanaosema nawabana na siwapi ushirikiano walikuwa na field trip huko mikoani. Walipewa kiasi kikubwa tu cha pesa za safari, na kama ilivyo kawaida ya kila ofisi ina utaratibu wake. Watu wanapotoka field trip basi lazima wafanye retirement, na sisi hapa ofisini kwetu kila kitu kinafanyika online kwenye system ya taasisi husika. Miongozo iliyopo iko wazi kwamba risiti pekee zinazokubalika wakati wa kufanya retirement ni EFD receipts only. Kama mtu alienda kulala kwa hawara yake na siyo hotelini, basi afanye kila linalowezekana apate EFD receipt.

Sasa, kuna mtu anajifanya ni mkongwe wa taasisi, kwa hiyo baadhi ya mambo anataka tufanye business as usual. Katoka trip, kaja kufanya retirement, kaweka risiti za kuandikwa kwa mkono. Kweli, karne hii kuna hoteli ya hadhi ya nyota tatu inatoa risiti za mkono, wakuu?

Ile retirement yake mimi nimeipiga pini; nimeikataa na nimempa sababu kuwa haijacomply na matakwa ya taasisi. Hivyo nimempa siku tatu mbele aweze kutafuta documents halali. Wenzie wote wamefanya hilo zoezi vizuri, ingawa najua risiti nyingi zimetengenezewa Kariakoo tu hapo, ila nimefumba macho tu. Sasa huyu mmoja aliyeniwekea mirisiti ya kuandikwa kwa mkono ndie ananizungumzia vibaya huko kwa mavikao yao.

Hivi, kwa nini hapa Bongo mtu ukitekeleza majukumu yako unaonekana kama snitch, wakuu?
Kwa hiyo unataka kusema hakuna watu wenye kiherehere!
 
Acha uboya maCCM yanavyotupiga na kutubagaza hivi bado unabania watu wewe ndo tatizo.
 
Back
Top Bottom