Ngoja niwasaidie wakati mnajiandaa na champions ijayo.
Kwanza Jiulizeni ni kwanini timu zilizofungwa na Simba hapa Dar es Salaam ndizo zilizocheza finali champions?
Kwa akili za kawaida Simba imezifunga timu zote zilizocheza finali basi Simba ndio ingekuwa sahihi kwa fanali na ubingwa. Lakini kwanini imeishia pale ilipoishia?
Majibu yake ni rahisi tu, ambayo ni ama:
1. Simba imecheza na timu dhaifu kwenye ligi ya nyumbani, yaani sio kipimo sahihi kwao. Mfano, kwenye ligi kulikuwa na Yanga ambayo kwa miaka 4 mfululizo ilikuwa inakinga bakuli kupata fedha, wachezaji wanagomea mazoezi na mechi, makocha na wachezaji hawalipwi mishahara yao, makocha na wachezaji wanabadilishwa kila wakati, hivyo Simba kuifunga Yanga ya hivi hakikuwa kipimo sahihi kwa simba iliyo kamili idara zote. Kwenye ligi kulikuwa na IHEFU, Mwadui, Polisi, KMC, Gwambina, Namungo, nk ambazo zisingeweza kutoa ushindani kwa Simba yenye kikosi kipana cha professionals.
2. TFF na marefa na viongozi wakuu wa nchi waliipandisha mabega Simba na kuipa matumaini feki ("false hope") kwa kuwasifu, kuwapangia ratiba na waamuzi rafiki na kutumia fedha za mfadhili dhidi ya wachezaji wa timu nyingine na marefa ambao walikuwa hawalipwi stahiki zao. Hivyo timu ilikuwa inaonekana inashinda kumbe iko juu ya mabega ya watu (unfair competition). Ushahidi wa hili ni Simba kuweza kuwashawishi viongozi wakuu wa nchi kwenda uwanjani kuona mpira biriani dhidi ya timu dhaifu za ligi kama Yanga ya kuungaunga wachezaji na makocha.
3. Inawezekana ndani ya vyumba kubadilishia nguo wageni kwenye viwanja vyetu kulikuwa na "namna" inayotendwa (no evidence), mungu anajuwa, au ni maswala ya muda tu itakuja kufahamika.
4. Kufika kwao rpbo finali ilikuwa fluke tu; chance, good luck, good day. Ndio maana siku nyingine inafungwa na Mwadui, Yanga mbovu, Ruvu, Kagera pamoja na kuwa na fedha, kocha mzuri na wachezaji wazuri relatively.