Kwanini Mungu aliita kwamba "Adamu uko wapi?"". Hii ina maanisha kwamba ukijificha Mungu hawezi kukuona?

deblabant

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2022
Posts
2,650
Reaction score
4,065
Kwa nini Mungu aliita kwamba "Adamu uko wapi?"". Hii ina maanisha kwamba ukijificha mungu hawezi kukuona?

Naombeni jibu
 
Hapana. Ni kinyume chake. Ukijificha, wewe ndiwe huwezi kumwona Mungu.

Mungu alimwita Adamu ili kumzindua arudi katika utimamu wake wa akili, ajue kwamba hitaji lake ni Mungu na si kinginecho, ama awe nuruni au gizani.

Kwa hiyo Mungu alichukua hatua ya kumwita Adamu kwa niaba yake Adamu mwenyewe.

Alimfanyia kile ambacho Adamu angepaswa kufanya mwenyewe baada ya kwenda kinyume na Mungu.

Majifunzo hapa ni kwamba usijifiche na kujitosa gizani zaidi unapomkosea Mungu. Mwite, ataitika na kukusaidia kabisa.

Kama Mungu yu radhi kuchukua hatua ya kwanza ili kukurejesha alipo, nini sasa kikuzuie usiunyoshe mkono wako ili akuinue na kukuokoa?

Adamu alijificha kwa kutukusa (entertain) dhana potofu kwamba pengine Mungu amemchukia na kwamba hali yake isingeponyeka.

Mungu alimwita Adamu ili kumthibitishia vinginevyo kwamba mawazo anayowaza sasa dhidi ya Mungu wake ni potofu na hayana msingi wowote.

Mungu alimwita Adamu ili kumwonesha kwamba bado Muumbaji wake angali upande wake, na kamwe asingemwacha bila uamuzi wa Adamu mwenyewe.
 
Naombeni jibu
Adamu alijificha sababu aliona 'aibu' baada ya kujijua yupo 'uchi'....

Mungu alimuita Adamu ila asikie jibu kutoka kwa Adamu kwanini alijificha..
 
Mkuu nimependa jibu lako...
 
Adamu alijificha sababu aliona 'aibu' baada ya kujijua yupo 'uchi'....

Mungu alimuita Adamu ila asikie jibu kutoka kwa Adamu kwanini alijificha..
Hii ni tafsiri yako au? Sasa mi nikija na tafsiri yangu na yule akaja na tafsiti yake itakuwaje. Kumbuka hakuna mwenye umiriki wa tafsiri
 
Adamu alijificha sababu aliona 'aibu' baada ya kujijua yupo 'uchi'....

Mungu alimuita Adamu ila asikie jibu kutoka kwa Adamu kwanini alijificha..
Kwahiyo Mungu alikuwa hajui kwanini Adam amejificha?
 
Hii ni tafsiri yako au? Sasa mi nikija na tafsiri yangu na yule akaja na tafsiti yake itakuwaje. Kumbuka hakuna mwenye umiriki wa tafsiri
Ni kweli, Kila hatuwezi kulingana tafsiri na huwezi kukwepa hilo.
 
Acha ukorofi Mkuu.

KaziKweliKweli/JobTrueTrue
 
Ni kweli, Kila hatuwezi kulingana tafsiri na huwezi kukwepa hilo.
Kivipo nisikwepe wakati ni tafsiri yako wala Mungu hajashuka akasema kwamba alimaanisha nini
 
Kitabu gani hakieleweki kila kukicha ni editing tu. Naskia hata sala ya baba yetu papa anataka ku iedit kwamba mungu hawezi kututia majaribuni
Kwanini unahangaika na kitu ambacho hakieleweki soma unacho elewa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…