Kwanini Mungu aliita kwamba "Adamu uko wapi?"". Hii ina maanisha kwamba ukijificha Mungu hawezi kukuona?

Kwanini Mungu aliita kwamba "Adamu uko wapi?"". Hii ina maanisha kwamba ukijificha Mungu hawezi kukuona?

Hapana. Ni kinyume chake. Ukijificha wewe ndiye huwezi kumwona Mungu.

Mungu alimwita Adamu ili arudi katika utimamu wake wa akili, ajue kwamba hitaji lake ni Mungu na si kinginecho, ama awe nuruni au gizani...
Jibu lako limefanya niamin wanaoyachunguza maandiko bado wapo, unasali wapi nikaribie mkuu?
 
Mungu aliimpa "benefit of doubt " ,hata mahakamani wanasema "innocent until proven guilty ".Mungu muweza wa yote anajua kila kitu. Alijua Adam alipo na bado alimuita.
 
Naombeni jibu
Hakuna Mungu na Adam hakuwahi kuwapo.

Hizo habari za Mungu na Adam ni hadithi zilizotungwa na watu tu waliokuwa wanajaribu kutatua matatizo ya jamii zao.

Kwa taarifa zaidi soma kitabu cha Dr. James Kugel "How To Read The Bible: A Guide To Scripture Then And Now".

 
Naombeni jibu
Wanakupa majibu yasiyo sahihi.

Ni hivi, Mungu ana uwezo wa kuona kila kitu, kilichopita na kitakachotokea. Lakini sasa, kumbuka kwamba - ana uwezo, sio kwamba anaona.

Kwa hiyo anapoamua kuangalia kitu ni kama anafungua file na kuona kila kitu, kiwe cha mbele au cha nyuma katika maisha yako. Usidhani kwamba kila sekunde inayopita maisha ya watu bilioni nane duniani yapo wazi mbele yake kama vile anaangalia TV, hapana, bali ana uwezo wa kuangalia akaona, pale inapobidi aangalie. Kama hana sababu ya kuangalia basi hatajua unachofanya kwa wakati huo. Na mara nyingi haangalii mambo tutakayofanya mbeleni, labda iwe tunamsihi sana kwa maombi aangalie.

Kwa hiyo hakumwona Adamu wala Eva akila tunda, bali Adamu alipomwambia wamejificha, immediately akajua wamekula - na akawauliza (bila yeye kuangalia) mmekula tunda? Wakati wakila hakuwaona kwa sababu hakuwa ameelekeza fikra juu yao wakati huo.

Kwa hiyo kuna wakati, by the time anaelekeza fikra kwako anakuta yameshakukuta ya kukukuta - mara nyingine hata umepatwa na janga na kufa. Ndio maana ni muhimu kusali kila wakati, kwamba kila wakati unajaribu kuvuta attention yake kwako ili kama kuna jambo baya mbele yako, ikiwa inakubalika kwake, anakuepusha nalo. Na akiona acha litokee kama sehemu ya kawaida ya maisha ya mwanadamu, litakupata, japo haina maana yeye ndio anapanga likupate. Ndio maana mara nyingine utasali, utaanza safari ya kwenda mkoani, na bado utapiga mzinga na kufa!
 
Hapana. Ni kinyume chake. Ukijificha wewe ndiye huwezi kumwona Mungu.
Kwa hiyo ukiwa sehemu peupe unamwona Mungu? Wewe binafsi umeshamwona mara ngapi, maana mie ninachojua mwanadamu hawezi kumwona Mungu akaishi.
 
Kumbuka hata biblia unayotumia iliandikwa na wakatoliki halafu nyie mkamegewea tu halafu .kajifanya wajanja kufuta baadhi ya vitabu
Ukatoliki umeanza karne ya tano. Biblia imekuwapo tangu karne ya kwanza kabla hata Waroma hawajakubali Ukristo. Sasa iweje Wakatoliki ndio waliandika Biblia?
 
Kwa hiyo ukiwa sehemu peupe unamwona Mungu?
Jibu ni ndiyo, iwapo maana ya ^peupe^ ni nuruni katika mantiki ya Biblia.

Dhambi zetu ndizo zinatufarakanisha na Mungu.

Hii ni kusema kwamba dhambi ni kama ukuta unaomzuia binadamu asimwone Muumbaji wake.

Wewe binafsi umeshamwona mara ngapi, maana mie ninachojua mwanadamu hawezi kumwona Mungu akaishi.
Kuna kumwona Mungu kwa muktadha wa Adamu na Hawa ile kitambo kabla ya anguko, na kumwona Mungu kwa muktadha wangu na wako leo baada ya janga la dhambi.

Unadhani kwa nini baadhi ya watu hawadhani Mungu yupo? Kwa nini hawamwoni?

Sababu mojawapo ni kwamba akili zao zimedidimiza na kufukia mstari unaotenganisha mema na mabaya.

Kwao wema ni ubaya na ubaya ni wema; kwao watu hao, Mungu ni Shetani na Shetani ni Mungu.

Watu na namna hiyo, uwepo wa Mungu ni fumbo zito mno wasilolimudu na lenye mateso makali, ambalo wao huona ahueni kulitupilia mbali badala ya kulitafakari japo kwa sekunde.
 
Jibu ni ndiyo, iwapo maana ya ^peupe^ ni nuruni katika mantiki ya Biblia.

Dhambi zetu ndizo zinatufarakanisha na Mungu..
Tatizo la binadamu ni kwamba mambo yaliyo rahisi sana tunaamua kuyafanya yaonekane kuwa magumu sana, na yaliyo magumu tunayachukulia kirahisi sana!
 
Naombeni jibu
Anakuona fureshi ila Kwa vile umejificha lazima akuite. Pia Kuna nafasi alimpa aitawale, alivyochungulia akamuona mtu mwingine so ilibidi amuite. Na hata Adam mwenyewe alimwambia nilijificha maana nili uchi.
 
Katika Mwanzo 3:9, Mungu anamwita Adamu, "Uko wapi?", baada ya Adamu na Hawa kula tunda lililokatazwa na kujificha. Swali hili lina tafsiri nyingi, na hakuna jibu moja linalokubalika kwa ujumla. Baadhi ya tafsiri ni pamoja na:

Mungu anaonyesha huzuni na tamaa: Mungu hakuwa akimuuliza Adamu kwa hasira au kumtafuta kimwili. Badala yake, alikuwa anaonyesha huzuni na tamaa kwa mabadiliko yaliyotokea kwa Adamu kutokana na dhambi. Swali lilikuwa ni la kiroho zaidi.

Mungu anafunua aibu ya Adamu: Adamu na Hawa walificha uchi wao baada ya kula tunda, wakionyesha aibu yao baada kufanya dhambi. Swali la Mungu linawafanya wakabiliane na aibu yao na kutambua hali yao ya dhambi.

Mungu anaanza mazungumzo: Swali linafungua njia ya mazungumzo kati ya Mungu na Adamu kuhusu kile kilichotokea. Hii inampa Adamu nafasi ya kuelezea matendo yake na kumwomba Mungu msamaha.

Jaribu kupitia Waebrania 4:13: "Hakuna kiumbe kilichofichwa machoni pake; vitu vyote viko wazi na vyake."
 
Adamu alijificha alijua ameshaharibu uhusiano mzuri ilikuwepo ukaaribika.

Ni sawa na mtoto wako akitenda kosa asikie unamwita
 
Waislamu walijua juu ya Admu kutokana na masimulizi ya Musa, ambayo aliandika karibu miaka 2000 kabla Quran haijatokezwa. Sasa kama Musa alieleza juu ya Adamu na Hawa, na Quran ikaeleza juu ya Adamu mwingine tofauti, maana yake ni kwamba kuna Adamu ambaye Musa haukuongea juu yake. Sidhani kama huo ndio msimamo rasmi wa Uislamu, na kama ndio basi kuna tatizo kubwa sana katika imani ya Kiislamu - kupunguza urefu na uzito wa yale ambayo Musa alifununuliwa na Mwenyezi Mungu
 
Waislamu walijua juu ya Admu kutokana na masimulizi ya Musa, ambayo aliandika karibu miaka 2000 kabla Quran haijatokezwa. Sasa kama Musa alieleza juu ya Adamu na Hawa, na Quran ikaeleza juu ya Adamu mwingine tofauti, maana yake ni kwamba kuna Adamu ambaye Musa haukuongea juu yake. Sidhani kama huo ndio msimamo rasmi wa Uislamu, na kama ndio basi kuna tatizo kubwa sana katika imani ya Kiislamu - kupunguza urefu na uzito wa yale ambayo Musa alifununuliwa na Mwenyezi Mungu
Fata link hiyo chini, niliandika haya kuhusu Adam:

https://www.jamiiforums.com/threads...enye-biblia-hakuna-hawa-kwenye-quran.2014179/
 
Haifunguki

1717520119102.png
 
Hapana. Ni kinyume chake. Ukijificha, wewe ndiwe huwezi kumwona Mungu.

Mungu alimwita Adamu ili kumzindua arudi katika utimamu wake wa akili, ajue kwamba hitaji lake ni Mungu na si kinginecho, ama awe nuruni au gizani...
Congrats
 
Back
Top Bottom