Miongoni mwa maswali najiuliza kila uchwao ni kwanini Mungu aliitwa Mungu na sio jina lingine?,Ni nani alimpatia hilo jina? Na kama yupo alikuwa nani?
Kwanini Mungu hakummaliza shetani hukohuko kama kweli ni muharibifu? kiasi kwamba anatuletea tabu ambazo tunaamini yeye ni chanzo? na anashindwaje kumuangamiza hata sasa ili hali hakuna anachondwa?
Mungu anayo majina mengine mengi kulingana na lugha, tamaduni na kabila.. Hivyo Mungu hana jina MOJA
1. ADONAI-Mungu Mwenye Enzi Yote Mwanzo 15:2-8
2. EL – SHADAI-Mungu ututoshelezae/Mungu mtoshelezi
Mwanzo 17:1
3.EL-OHEENU- Bwana Mungu Wetu Zaburi 99:5,8,9
4. EL- GIBBOR- Mungu Mwenye Nguvu, Isaya 9:6-9
5. EL-OHEEKA- Bwana Mungu Wako Kut 20:2,5,7
6. EL-ELYON -Mungu Aliye Juu Sana Mwanzo 14:18
7. EL-OHIM- Muumbaji wa Milele Mwa 1:1
8. YEHOVA- SABAOTH Bwana wa Majeshi 1Samwel 1:3
9. JEHOVA TSIDKEMU -Bwana ni Haki Yetu Yeremia 23:6
10. JEHOVA RAPHA- Mungu Atuponyae,kutoka 15:26
11. JEHOVA MEKADDISHKEM- Mungu atutakasaye Kutoka 31:13
12. JEHOVA ROHI-Bwana Mchungaji Wangu Zaburi 23:1
13. JEHOVA JIREH- Mungu Atupaye /Atoaye Mwanzo 22:14
14. JEHOVA HOSEENU -Bwana Aliyetuumba Zaburi 95:6
15. JEHOVA NISSI- Bwana ni Beramu (Bendera)
yangu
Kutoka17:15
16. JEHOVA SHALOM -Bwana ni Amani, waamuzi 6:24
17. JEHOVA SHAMMAH -Bwana Yupo Hapa, Ezekiel 48:35
18.El-hai-Mungu aliyehai,Joshua 3:10,1 Samwel 17:26
19.El-elohe-israel-Mungu wa Israel, Mwanzoh 33:20
20.El-Olam-Mungu wa milele,Ufunuo 4:8,kutoka 3:14
Majina haya yapo katika Lugha za kiebrania
Shetani sio mwili ni roho na roho ikizaliwa haifi