1. Kristo ni mrithi wa hili jina
Waebrania 1:1-4
Imeandikwa hivi:
“Mungu, ambaye alisema zamani na baba zetu katika manabii kwa sehemu nyingi na kwa njia nyingi, mwisho wa siku hizi amesema na sisi katika Mwana, aliyemweka kuwa mrithi wa yote, tena kwa yeye aliufanya ulimwengu. Yeye kwa kuwa ni mng'ao wa utukufu wake na chapa ya nafsi yake, akivichukua vyote kwa amri ya uweza wake, akiisha kufanya utakaso wa dhambi, aliketi mkono wa kuume wa Ukuu huko juu; amefanyika bora kupita malaika, kwa kadiri jina alilolirithi lilivyo tukufu kuliko lao.”
Kwa mistari hii ya mwanzo ya waraka wa waebrania tunaona ya kuwa Yesu Kristoamewekwa na Mungu Baba yake “kuwa mrithi wa yote”. Na katika mambo aliyopewa kuyarithi ni pamoja na JINA HILI LA YESU – NDIYO maana imeandikwa “amefanyika bora kupita malaika, kwa kadiri jina alilolirithi lilivyo tukufu kuliko lao” (waebrania 1:4)
Kwa hiyo ni wazi kwamba huyu mwana wa Mungu alipewa jina hili la Yesu kwa kuwa yeye MRITHI WA YOTE ya Baba yetu mungu aliye mbinguni
................................
...............................................
........................................................
Unaweza ukawa unajiuliza inakuwaje jambo hili. Lakini kabla ya kuendelea kusita, nadhani utakubaliana na mimi ya kuwa mtu hawezi kurithi kitu chake, bali anarithi kitu kisicho chake. Pia, mtu hawezi kurithi Jina Lake, bali anarithi jina lisili lake. Kwa hiyo biblia inapotuambia ya kuwa Baba amempa Mwana wake urithi wa Jina lake, ina maana ya kuwa hapo mwanzo jina la Yesu lilikuwa ni la Mungu Baba hadi alipoamua kumpa jina hilo motto wake kama sehemu ya urithi wake! Ndiyo maana yesu Kristo alisema, “
Kwa maneno mengine alitaka tujue ya kuwa jina la Yesu Kristo si “jina lake mwenyewe.” Lingekuwa “jina lake mwenyewe” angepokelewa, lakini kwa kuwa jina la Yesu Kristo alilokuja nalo ulimwenguni ni “jina la Baba yake” hawakumpokea.
Nadhani sasa unaweza ukaelewa kwa nini ina hili la Yesu Kristo linaitwa ni jina lipitalo majianyote mbinguni, duniani na hata chini ya nchi (wafilii 2:9-10). Jina la Yesu Kristo ni jina lipitalo kila jina kwa kuwa ndilo jina la Mungu Baba pia. Mungu Baba angekuwa na jina jingine kuliko hili, biblia isingesema hata mbinguni jina la Yesu Kristo liko juu ya majina yote.