Kwanini Mwalimu Nyerere, pamoja kupewa PhD 23, tuzo lukuki, usomi na weledi vyake hakuwahi wala kupenda kuitwa daktari? Je, aliogopa au hakujua?

Katunukiwa na vyoo siyo vyuo. Ametunukiwa au amenunua toka kwenye degree mills kama akina Gwajima na Njaa Kaya?
Mkuu hizo ni hisia zako, sina unasaba na stivu na wala hatufahamiani kabisaa ili kwa hili hujaonesha tofauti ya usomi wako na influence ya Stivu, wewe umeonyesha kijicho tu!

Mkuu Gwajima ana watu ambao wameguswa na umaamuma wake!! Toka hadharani utunonyeshe watu 500 tu walioguswa na usomi wako??

Mkuu pambana na hali yako, usiwapange wala kuwapangia watu!
 
Soma uzi vizuri utaelewa. Kama influence ni big deal basi Nyerere angeitwa daktari. Anyways, hawa wenu ni madoktari.
 
Mwalimu hakuwa ni mtu wa kujikweza kweza na pia alikuwa anajiamini sana na aliletwa na Mungu kwa ajili ya kuwaongoza watu wake waliochaguliwa na Mungu 🙏

The Chosen people of Tanganyika !
Na akawatunzia mali zao zote zilizokuwa Ardhini na Baharini ili wakishapata Elimu ya hizo mali zao waje wazitoe huko ziliko hata kwa kushirikiana na aliowaitaga mabeberu lakini iwe ni kwa faida ya vizazi na vizazi vya watu wake aliowapenda sana wa Tanganyika na baadaye Tanzania 🇹🇿 😳🙄🙄🙄🙄 !
 
Hakuwa na viini vya kujitweza kama hawa wengine, yeye aliamini katika usawa zaidi, hawa wa sasa wanaamini katika kuheshimiwa, kuogopwa, kunyenyekewa na tabia zingine zinazofanana na hizo
 
NChi za wenzetu ukisikia mtu ni PhD holder basi ujue ni elimu imelala kweli kweli sio kama huku kwenu mnakuta sijui Dr Samia sijui dkt nani halafu ukimfanyia assessment huyo Dr unaona kabisa hana cognitive reasoning, matokeo yake akikutana na situations zinazo unveil her or his low cognitive skills anaishia kuwa mbogo.
 
 
Na ww pia umekosa wazo la kuanzisha thread. Kwani ukiitwa Dr na usiitwe Dr itakuwa umepata au umekosa nn? Tujaribu kujadili au kuanzisha thread za maana zenye impact kwa issues za kitaifa. Mfano kikwete kuiba gesi mtwara.
 
Stiv nimemtumia kama mfano tu. Weka wote walio pewa za burebure wamazo ita za heshima
 
Alijua ni ulimbukeni na misifa TU, Sasa Kila mtu anajiita dokta! Kaa darasani Iuone moto wake! Halafu yanachekelea sana!
 
Validation za watu kama Mwashambwa Lucas
 
Angekubali kuitwa Daktari, sasa hivi bongo imgeizidi Sauzi Afrika kimaendeleo, ila kitendo cha kukazania kujiita Mwalimu kasababisha nchi iwe kama majengo ya shule za msingi vijijini
 
Watanzania tunapenda kujikweza. Si jambo la ajabu kusikia mtu akijitambulisha mimi naitwa Mr So and D
So.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…