Kwanini Mwanajeshi akipigwa na Raia kwa Ugomvi Wao Kujitetea Kwake ni kwenda Kambini kuomba Msaada kwa Wenzake?

Kwanini Mwanajeshi akipigwa na Raia kwa Ugomvi Wao Kujitetea Kwake ni kwenda Kambini kuomba Msaada kwa Wenzake?

Hatakiwi kuomba msaada..yani raia mmoja tu anakushinda mpaka ukawautwa mbraza ako kikosini?

Inamaana kumbe wajeshi ni wachumba tu, watu wanaogopa uniform tu
Mkuu ni heshima tu ya jeshi, kuna raia mtaani wanapiga mkuu, acha kabisa usijichanganye. Niliwahi shuhudia mjeda mmoja alichezea sana kichapo kwa yule jamaa, ila sema kikosi kilichokuja kwakweli ule mtaa ulitulia mpaka leo [emoji23][emoji119]
 
Mkuu samahani umeshawahi kupewa Mkong'oto na Mwanajeshi / Wanajeshi?

Wasamehe.
Sijawai pata kadhia hiyo ya kupigwa na wanajeshi au mwanajeshi,ila nishapata mtihani na mwanajeshi aliyevaa kiria akiwa na gari yake barabarani, baada ya ajali ndogo tena chanzo akiwa ni yeye, kashuka tu kwa gari yake anaanza kunifokea, nikamuuliza tatizo nini!? Akasema nimemngonga na anataka gari zote ziende kambini,tena akaitaja hadi jina hiyo kambi, nikamwambia Mimi sipajui,mi ninachojua baada ya ajali traffic atapima na ndiyo tutajua Nani mwenye makosa na Bima zetu zitafanya kazi yake! Akasema unajifanya mjanjanja basi utaona, si akaanza kuitaa wenzie kutoka kambini, wenzie kufika wanaanza kwa Nini umesema gari lake bovu!? Nikasema hoja hapa ni ajali,Kama kuna Mtu mwenye sifa ya kupima ajali apime! Tulibishana sana,na kibaya zaidi hadi traffic waliogopa baada ya kuona wanajeshi wengi wamejaa alafu mi peke yangu nabishana nao, wao wanataka twende kambini kwao,mi nataka twende traffic! Tulibishana hadi kuna Mkubwa wao alikua anapita na Yuko na escort ya ma MP ndiyo akasimama, akauliza shida nini!? Baada kuelezea na akaangalia ajali yenyewe akaamrisha gari zote mbili kwanza zitoke barabarani ziwekwe pembeni alafu mazungumzo ndiyo yaendelee, baada ya kuziaachanisha gari zote mbili, na mabampa nayo yalikua yamebonyea yakarudi kwenye position yake na hakuna damage, Basi kila Mtu akaenda na safari zake! Lakini wale wanajeshi naamini walijiona ni Wajinga sana,na akili zao zilikua kwenye wizi tu wakutaka kuniibia pesa ya matengenezo hewa, bahati nzuri Mimi ajali zote huwa nawachia Watu wa Bima wa deal nazo,mi sina muda wakulipa Mtu barabarani kisa ajali wakati Nina bima!!
 
Inakuwaje Mtu uliyefunzwa vyema tena Kimedani/ Kivita ukiwa na Ugomvi wako na Raia kwa mfano mmegombania Mwanamke na akakuzidi Kete 'akambandua' na Wewe (Mwanajeshi) kuchezea Kichapo (Kipigo) utakachokifanya ni kwenda Kambini kuwachukua Wenzako ndiyo mje Kumchangia huyu Raia na Kumpiga?

Tafadhali King Kong III ukiwawakilisha Wajeda (Wanajeshi) Wenzako nakiomba uweke Neno lako hapa.
Ndivyo wanavyofundishwa kuusaka ushindi!

Ukimuona adui mmoja, unatakiwa kumpelekea nguvu ya "seksheni" ili kumdhibiti.

Adui seksheni moja hupelekewa nguvu ya "patuni".

Patuni ya adui hupelekewa moto wa "kombania".

Kombania ya adui hupelekewa nguvu ya "battalioni".

Battalioni ya adui hupelekewa nguvu ya "brugedi" nk nk.

Umoja na ushirikiano huleta ushindi ndivyo mafunzo yao yanavyoelekeza.

Lakini mkuu, ulishawahi kouna mjeda mtu mzima akifanya hayo?

Hizo mambo hufanywa na vijana damu moto wenye mihemko waliotoka "depot".

Keshapiga shabaha kulenga karatasi, anataka kuona bunduki lake linauaje!

Keshafunzwa kutumia kirungu, kutupia mtu pingu, kupiga judo nk nk, sasa anataka ayaone matokeo kwa vitendo.

Wanaitwa "trained soldiers" cheo cha pili cha askari toka ukuruta, wana hamu hata ya kuingia vitani wakayadhhirishe mafunzo yao.
 
Inakuwaje Mtu uliyefunzwa vyema tena Kimedani/ Kivita ukiwa na Ugomvi wako na Raia kwa mfano mmegombania Mwanamke na akakuzidi Kete 'akambandua' na Wewe (Mwanajeshi) kuchezea Kichapo (Kipigo) utakachokifanya ni kwenda Kambini kuwachukua Wenzako ndiyo mje Kumchangia huyu Raia na Kumpiga?

Tafadhali King Kong III ukiwawakilisha Wajeda (Wanajeshi) Wenzako nakiomba uweke Neno lako hapa.
hii sijui huwa kwanini
 
Kuna mmoja tulijipigia tena aalikua wawili na kavits kamgonga boda afu analeta kibass alipigwa vibaya hovyo
 
Mimi nishaga weka wazi, wanajeshi au askari yoyote yule akijileta zitapigwa na sitasarenda labda waniuwe ila kama sijafa nitamuuwa yeye. Hawa watu siwapendi [emoji35]
 
Chinga Yupo Kanenepa balaa nilikutana naye juzi anapiga story na Bodaboda maeneo ya Jambo Lee kapiga Sare zake Green Suruali na Shati la Light green.
Ninachompendea Afande Chinga ni Mtu wa Bata ila ana Maendeleo makubwa ya Kimaisha na ni Mtu Muwazi na Mshauri mzuri mno wa Kimaisha.

Mwambie Yule mwana Simba SC anayepiga Story katika Kijiwe cha Fundi Viatu Athumani Geti Dogo Lugalo akiwa na Mchezaji wa zamani wa Yanga SC na baadae Simba SC Shaaban Ramadhan namsalimia mno.
 
Wale special forces usije ukajaribu. Hata kama alikuwa mchovu ila akishapita kwenye yale mafunzo huwa wanakuwa hatari. Sema special forces huwa wastaarabu... tatizo lao kwenye mademu tu. Wanakuwaga dhaifu.
Duh!
 
Ninachompendea Afande Chinga ni Mtu wa Bata ila ana Maendeleo makubwa ya Kimaisha na ni Mtu Muwazi na Mshauri mzuri mno wa Kimaisha.

Mwambie Yule mwana Simba SC anayepiga Story katika Kijiwe cha Fundi Viatu Athumani Geti Dogo Lugalo akiwa na Mchezaji wa zamani wa Yanga SC na baadae Simba SC Shaaban Ramadhan namsalimia mno.

Yes jamaa ametoka mbali sana ,tangia yupo na mdogo wake wanakaa kwenye kichumba cha kawaida pale lugalo kabla ya kujengwa hizo flats ,amepiga hatua kubwa ,mtu wa kujichanganya na maneno mengi.

Hahahaa nitamsalimia.
 
Back
Top Bottom