Kwanini mwanaume anayeamua kuwa na single mother anajitengenezea sintofahamu siku za baadae

Kujifariji kwingi,,
Halafu kamwandiko ka kilokole kalikochanganyika na ufeminist ndani yake, Halafu kanaact kamsela wakati tone inakaumbua kuwa ni kadem kenye mindset ya women can be superior to men.
We suria wa watu amka kwenye huo usingizi umbadilishe mwanao pampaz ohoo..
 
Hawawezi kuficha hisia zao kwa wanaume waliozaa nao. Maana ndie chaguo lake. Wewe unatumika kutatua mgogoro wao.
Na kama kazaa na Wanaume wawili au watatu tofauti,hisia zao zinakuwa kwa hao wote?
 
Uzi mzuri sana hapa wanaume wenzagu kuna cha kujifunza...
 
With all due respect, unawapotosha umma. Haya unayoyaandika ni mawazo na experience yako binafsi sio ya watu wote na lazima iheshimiwe. Lakini, nyuma yake naona kama kuna chuki kubwa kwa mwanamke mwenye mtoto asiye na mume. Naomba nikuhakikishie kuwa wapo single mothers tofauti kabisa, kabisa na haya uyasemayo. Labda ungeangalia upande huo pia.

Kingine, umesema a woman is only loyal to her feelings. Sawa, but who isn't?? Haya wewe uko loyal kwa hizo hisia zako kuwa wanawake single mothers wako namna fulani. Unapoamua kuwa na mtu fulani kimapenzi, you're being loyal to your feelings too. Unapoamua kuwa huhitaji tena uhusiano, again, you are being loyal to yourself. Kwa hili, endapo nimekosea, naomba unieleweshe
 
With all due respect, unawapotosha umma. Haya unayoyaandika ni mawazo na experience yako binafsi sio ya watu wote na lazima iheshimiwe.
Kupotosha maana yake ni kuwa naandika vitu ambavyo havipo kabisa katika jamii. Sasa je ni kweli haya ninayoyaongea ni mambo nayatunga kutoka kichwani mwangu,yaani nasemea uongo kitu ambacho kipo?
Lakini, nyuma yake naona kama kuna chuki kubwa kwa mwanamke mwenye mtoto asiye na mume. Naomba nikuhakikishie kuwa wapo single mothers tofauti kabisa, kabisa na haya uyasemayo. Labda ungeangalia upande huo pia.
Kusema nina chuki ni matumizi mabaya ya misamiati. Nadhani ungesema ninakemea mfululizo labda ingekuwa sahihi. Kusema nipo motivated na chuki tu hiyo si ukweli. Nachukiaje kitu chenye madhara sasa?

Ni kweli wapo ambao wapo tofauti ila sasa turudi katika msingi wa hoja, mwanamke kujizalisha watoto bila taratibu rasmi ya kuwa mke halali wa mtu ni jambo zuri kwako?

Kanuni ni kwamba usizae na mwanaume yoyote yule ambaye si mume wako wa ndoa,na usijiruhusu kuwa katika maamuzi ya kuzaa na mwanaume ambaye hajawahi kuja kwenu kukuposa na kufuata taratibu kukuchukua kama mke halali.

Unazaa na mtu nje ya mfumo wa ndoa halafu unataka utambulike kama mwanamke ambaye anaishi ndani ya mfumo halali wa kijamii?

Hii inakuwaje ni sawa kwako? So mtoto wako wa kike utamruhusu akujie hapo nyumbani akiwa na mimba na haujui baba wa mtoto ni nani?🤔
Kingine, umesema a woman is only loyal to her feelings. Sawa, but who isn't??
Men aren't. Wanaume hatuna hisia bali tuna mantiki kwenye mahusiano. Wanaume wengi wanaoteseka na mahusiano au kuanguka kimahusiano ni kwasababu ya kutumia hisia (feelings) badala ya mantiki(logic).

Okay,tuchambue why ni tatizo. Mwanamke tokea anaumbwa mwanzo wa kale tukijifunza katika vitabu vitakatifu,anaelekezwa kuwa tamaa yake iwe kwa mwanaume na si kinyume chake.

Kwasasa wanawake wameweka tamaa kwa aina fulani ya wanaume sababu ya material possession zao yaani Mali. Hapo tu ndipo wanawake wa sasa mnapokwenda chaka. Kitendo cha kuweka tamaa ya mali ina maana mwanaume yoyote atakae mzidi dau mwanaume wako then utahamishia hisia kwake.

Ndio maana kirahisisha mambo nikasema mwanamke yupo loyal kwa hisia zake tu. Na kwa kusema hivyo ntakuwa nimemaanisha kuwa anatamaa ya vitu. Wanawake wa sasa hawana tamaa ya mwanaume kama mwanaume yaani hawezi kuipa dunia na vitu vyake mgongo amfuate mwanaume wake hiyo haipo tena, mimi binafsi nimefuta.
Haya wewe uko loyal kwa hizo hisia zako kuwa wanawake single mothers wako namna fulani.
Sio swala la mimi kuwa loyal ni swala la mimi kuwa logical.

Wewe nikuulize swali, una mtoto wako wa kiume hapo,umemsomesha kwa taabu sana hadi kafika hatua nzuri ya kuwa na kanzi nzuri,akapata mali na utajiri, ukafika muda wa kuoa,akakukelea mwanamke wa miaka 29 na kumtambulisha kama mkweo, ana watoto watatu wa baba tofauti,kila mtoto na baba yake, anataka kumuoa,na hao watoto anataka wawe warithi wake yaani wawe sehemu ya warithi wa mali zake kwenye mgao pamoja na mama yao?

Halafu kuwe na mwanamke mwingine binti wa miaka 24 ambaye hajazaa tena ni mwadilifu tu ana adabu na ni mzuri. Pia ana mahusiano na mtoto wako.

Anakuja kukuomba ushauri mama kuwa anawapenda wote ila anatakiwa kumchagua m'moja, anategemea ushauri wako kufanya maamuzi ya mwisho na utakae mpendekeza atamchukua na kumuoa?

Wewe kama mama unatapendekeza yupi,yule mwenye watoto watatu ndie awe mkweo au huyu asie na watoto?
Unapoamua kuwa na mtu fulani kimapenzi, you're being loyal to your feelings too.
Again wanaume hatutumii huu mfumo wa hisia kwenye maamuzi,huu ni mfumo wenu wanawake. Sisi tukipenda ni logical thinking process sio emotional feeling process.
Unapoamua kuwa huhitaji tena uhusiano, again, you are being loyal to yourself. Kwa hili, endapo nimekosea, naomba unieleweshe
Kuwa loyal to yourself haimaanishi kukana mwingine. Wanaume loyalty kwetu ni kujitoa kwa mwanamke na watoto wetu wawe na maisha mazuri ndipo sisi tunapata kuridhika. Loyalty kwa mwanamke inakwenda na anachotaka based na hisia zake zinamuelekeza wapi.

Mfano, Kijana na binti wanaohitimu chuo,baada ya kumaliza tu na kuingia mtaani mara nyingi mabinti huwa wanabadilika na kuanza mfumo mpya wa maisha na kukana mahusiano waliyotoka nayo chuo na sababu watakupa kabisa ila ni za kibinafsi.

Mpe kijana kazi ya mshahara wa milioni 5 kwenda juu kitu cha kwanza atawaza ni kuoa halafu ndio maisha yaendelee. That's loyalty ya kiume ilivyo kwa wanawake. Mwanamke mpe kazi ya mshahara wa milioni 5,tavunja mahusiano yake ya sasa na kutaka kuishi mwenyewe huku akitafuta kulala na wanaume wenye hela na status ya juu akiamini atakamata m'moja maana ndio anaona ni hadhi yake.

So loyalty ya mwanamke kwa mwanaume ni very questionable kwasababu wanawake ni hypergamous.
 
Kwahiyo ukimwongezea mtoto unakuwa umejiongeza kwenye orodha ya Wanaume ambao yeye anakuwa na hisia nao?
Wewe ndio unakuwa na faida maana umepata shamba la bwerere la kuoteshea mbegu zako
Na kuvuna bila tabu yoyote ile bila kudaiwa gharama za kulinunua shamba hilo..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…