Cheating is a long term mediated process. Imeanza akilini muda mrefu kabla haija manifest kwenye uhalisia.
Ni zaidi ya kitendo cha kumvulia mwingine nguo na kufanya naye kile kilichopaswa kutofautisha hadhi ya mwenzi wako na wengine.
Ni msururu wa uongo juu ya uongo uliokuwa ukisema na kuishi muda wote hadi kufikia kwenye tukio, msg na maongezi ya siri, mikutano ya siri, mawazo yako hasi kuelekea kwa mwenzio (ukweli ni kuwa watu huanza kuwashusha wenzi wao thamani au kuwatoa kasoro akilini mwao kabla ya kuanza kuangaza angaza macho kwingine).
Ni kukosa kwako ari ya kuishi viapo vya uaminifu ulivyotoa, ambalo linaashiria pia hali yako ya kiroho/kiakili ilivyo. Watu wanaoishi kiholela bila kuwa na mipaka au kutoheshimu mipaka waliyodai kujiwekea huwa na mvurugo nafsini mwao. You cannot have peace when you live a contradiction.
Either live an open polygamist/polyandrous life you believe in and not take unwilling victims in the process or live your vows to be faithful. It's the victims who help maintain the cheater's sanity by staying and trying to win them over.
Ni kukosa upendo na heshima kwa mwenzio na hivyo kujifikiria mwenyewe na mahitaji yako na kudharau ya mwenzio na kutojali madhara utakayomsababishia, kama unavyoona comments "ni tamaa zangu", "hawezi kuondoka", "nitakataa na atanisamehe", "nitakuwa msiri zaidi"
Ni ishara ya mtu immature asiye na uwezo wa kufanya maamuzi. Kama ndoa imekufa achana nayo acha kuishi uongo unamdanganya Nani!
Ni ishara ya mtu asiye na empathy yani haumii kwa kuumiza wengine, na hategemei kuwajibishwa.
Ni ishara ya mtu asiyejitambua, kama wanyama haja evolve beyond the physical, anaishi ili ale, anachagua mwenyewe anakula kwanza ndo ale au ale ndo atakula, imeisha hiyo.
Ndomaana mimi najiona mwenye bahati kuwa na mume wangu
wa kupuliza kwani amejua kufanya nyumba yetu kuwa kisiwa cha amani kwa kuishi ukweli wake!