Kwanini mwandishi anamuhoji kocha wa kigeni kwa lugha ya kigeni bila kutafsiri na kufafanua wakati lugha ya taifa ni Kiswahili?

habdul64

Senior Member
Joined
Dec 24, 2014
Posts
153
Reaction score
67
Habari wanajamvi,

Naomba kuelezea kero yangu juu ya waandishi wa habari za michezo wa Bongo. Yaani mwandishi anamuhoji kocha wa kigeni kwa lugha ya kigeni tatizo ni kwamba hatafsiri na wala hafafanui walichozungumza wakati anajua wazi lugha ya taifa ya Bongo ni kiswahili.

Je, washibiki waliowengi wanafaidika kweli kujua makocha wao wanatoa maoni gani? Mi nadhani wajifunze kwa BBC Swahili bwana.
 
Kama ni Kiingereza hiyo pia ni lugha ya taifa ila haina waongeaji wengi. Kwa hiyo sema kwa faida ya wasio elewa kiingereza itafsiriwe kwa kiswahili na sio kwa sababu ya lugha ya taifa maana kiingereza pia ni lugha ya taifa.
 
Wengi wao washamba tu mkuu..

Nimewahi kufatilia soka la ufaransa,
Mchezaji mgeni asiyejuwa kifaransa,, anahojiwa kwa kifaransa,,halafu mkalimani anatafsiri.

Mfano under herera mchezaji wa PSG akihojiwa anahojiwa kwa kifaransa,,na mkalimani anatafsiri kwa kispaniola.

Hapa kwetu ushamba na ujuwaji unatusumbuwa...

Kuongea kingereza ndy utaonekana mwandishi mzuri,,mbobezi.
 
Kama ni Kiingereza hiyo pia ni lugha ya taifa ila haina waongeaji wengi. Kwa hiyo sema kwa faida ya wasio elewa kiingereza itafsiriwe kwa kiswahili na sio kwa sababu ya lugha ya taifa maana kiingereza pia ni lugha ya taifa.
Lugha ya taifa ni kiswahili mkuu ,,tusidanganyane..
 
Habari wanajamvi,

Naomba kuelezea kero yangu juu ya waandishi wa habari za michezo wa Bongo. Yaani mwandishi anamuhoji kocha wa kigeni kwa lugha ya kigeni tatizo ni kwamba hatafsiri na wala hafafanui walichozungumza wakati anajua wazi lugha ya taifa ya Bongo ni kiswahili.

Je, washibiki waliowengi wanafaidika kweli kujua makocha wao wanatoa maoni gani? Mi nadhani wajifunze kwa BBC Swahili bwana.
Kigeni ndio timu gani?
 
Kwa England mchezaji au kocha anahojiwa kwa kiingereza tu
Ni sheria ili upate kazi Uingereza lazima ujue lugha yao
 
Lugha ya taifa ni kiswahili mkuu ,,tusidanganyane..
Sikudanganyi ila Kiingereza pia ni lugha ya taifa pamoja na kiswahili ndugu. Mashuleni, vyuoni, mikataba ya kazi, magazeti,interview, mahakamani, matangazo n.k kote huko inatumika lugha ya kiswahili na kiingereza tu.

Sasa kwa nini sio kiswahili na kijerumani ndugu?
 
Kingereza sio lugha ya taifa..

Kwetu kiswahili ndy lugha ya taifa, inafatiwa na kingereza.

Huwezi kusema kingereza ni lugha ya taifa wakati 90% ya watu wako hawajuwi.

Tanzania tunachekwa hata na mijusi kwa sababu ya kutokujuwa kingereza,,

Bado unasema Tanzania kingereza ni lugha ya taifa .,

Tanzania sheria bado zinatafsiriwa kwa kingereza lakini lugha mama ni kiswahili.
 
Naku nukuu "Kingereza sio ya lugha ya taifa...
Kwetu kiswahili ndio lugha ya taifa inafatiwa na kingereza"

Sasa mara ukatae mara ukubali, huko kufatiwa ndio utaifa wenyewe ndugu. Unafikiri kwa nini baada ya kiswahili hakijafuatia kifaransa, kinyakyusa, kichaga au kichina?

Ni hivi kingereza tulirithi kwa wakoloni waingereza na tulikubaliana kingereza pia iwe lugha ya taifa.
Mashuleni , mavyuoni, mikataba , mahakamani, nterview, matangazo , magazetini, lugha rasmi zinazotumika ni kiswahili na kiingereza tu na huo ndio uthibitisho wa lugha za taifa ndugu.

Kukosa waongeaji wengi hiyo sio hoja.
 
Hakuna mahala mimekubali
Kwamba kingereza ni lugha ya taifa.

Nimesema kiswahili ndy lugha ya taifa..
Ikifatiwa na kingereza,,sababu sheria mbali mbali bado zipo ktk kingereza.

Ni lini umelisikia bunge au viongozi mbali mbali wakihutubia taifa kwa kingereza?
Lugha ya taifa ni ile ambayo utaweza kuizungumza bila kwenda shule..tena inazungumzwa na 99% wa watu wake.
Lugha ambayo inazungumzwa tu mitaani humu.

Hapa kwetu huwezi kujuwa kingereza kama hukwenda shule,
Na hata hao waliopitia shule pia hawajuwi kuongea..kifasaha zaidi ya actually,of course,,you know.

Sasa utasemaje ni lugha ya taifa..?
 
Kama ni Kiingereza hiyo pia ni lugha ya taifa ila haina waongeaji wengi. Kwa hiyo sema kwa faida ya wasio elewa kiingereza itafsiriwe kwa kiswahili na sio kwa sababu ya lugha ya taifa maana kiingereza pia ni lugha ya taifa.
Usichanganye Official Language na Lugha ya Taifa.Kiingereza sio Lugha ya Taifa Tanzania, ni official Language yaani yaani lugha iliyopitishwa kwa matumizi Rasmi.Lugha ya Taifa la Tanzania ni Kiswahili.Unaweza kunithibitishia sasa umeelewa na kuona utofauti??
 
Hakuna mahala mimekubali
Kwamba kingereza ni lugha ya taifa.

Nimesema kiswahili ndy lugha ya taifa..
Ikifatiwa na kingereza,,sababu sheria mbali mbali bado zipo ktk kingereza.

Ni lini umelisikia bunge au viongozi mbali mbali wakihutubia taifa kwa kingereza?
Lugha ya taifa ni ile ambayo utaweza kuizungumza bila kwenda shule..tena inazungumzwa na 99% wa watu wake.
Lugha ambayo inazungumzwa tu mitaani humu.

Hapa kwetu huwezi kujuwa kingereza kama hukwenda shule,
Na hata hao waliopitia shule pia hawajuwi kuongea..kifasaha zaidi ya actually,of course,,you know.

Sasa utasemaje ni lugha ya taifa..?
Duh...mbona mgumu kuelewa wewe? Rwanda wana lugha za taifa tatu , kinyarwanda, french na english, maana yake ni kwamba hizo ndio lugha zilizorasimishwa na haimaanishi kuwa wanyarwandwa wote wanazijua lugha zote kwa ufasaha.
Hapa hoja ni lugha kurasimishwa kuwa lugha ya taifa.Kama ina waongeaji wachache hilo ni suala lingine ndugu.

Kingereza kimerasimishwa kuwa lugha ya taifa ndio maana kinatumika mashuleni, vyuoni, mikataba, interview, n.k

Hoja ya kusema kwa kwa vile waongeaji wengi hawaongei kiufasaha basi hiyo sio lugha ya taifa hiyo ni hoja mfu. Nasisitiza tena hoja ni kurasimishwa, hivi lugha amabayo haijarasimishwa inaweza kutumika mashuleni, vyuoni?
 
Usichanganye Official Language na Lugha ya Taifa.Kiingereza sio Lugha ya Taifa Tanzania, ni official Language yaani yaani lugha iliyopitishwa kwa matumizi Rasmi.Lugha ya Taifa la Tanzania ni Kiswahili.Unaweza kunithibitishia sasa umeelewa na kuona utofauti??
Wewe ndio umejichanganya kabisa. National official language maana yake lugha rasmi ya taifa na ndio kusema lugha ya taifa. Tuna official national languages mbili Kiswahili na english. Yaani lugha rasmi za taifa. Yaani lugha zilizorasimishwa kwa mawasiliano iwe kazini, interview, mikataba, mashuleni ,vyuoni n.k ni kiswahili na english.

Hayo unayosema english ipo kwa matumizi rasmi tu, matumizi rasmi yapi?
 
Back
Top Bottom