Kwanini Mwanza Wanauza magari bei rahisi kuliko Dar es Salaam?

Kwanini Mwanza Wanauza magari bei rahisi kuliko Dar es Salaam?

Leo ndo nimepata somo
Nimewahi ulizia probox succeed yenye manual transmission
Aseeeeeh huwezi amini...........
Niliambiwa sh mil 22
Huyo jamaa nilimwambia acha matani kazini yaan probox unaniuzia mil 22 je harrier utaniuzia bei gan....

Jamaa hakujibu tena
Ni wazi Dar uuni umezidi watu wnataka pesa kupitia mitaji ya watu wengine

Ilinibidi nihairishe kununua gari kwanza
 
DSM maiisha magumu, na matapeli wengi

Wengi wanataka kutatua shida zao ndani ya muda mfupi
Wenye pesa ni wengi ukilinganisha na sehemu zingine zote za nchi yetu, kwa hiyo demand ya vitu Dar ni kubwa kuliko sehemu zingine na hivyo kupelekea bei za vitu kuwa juu!
 
Habari za asubuhi wakuu.

Kwa muda kidogo nimekua nikifanya utafiti mdogo wa madalali wauzaji wa magari instagram na social media nyingine.

Kuna kitu nimegundua nikaona nijadiliane nipate majibu sahihi.

Nimeona madalali wa mwanza wanauza gari kwa bei rahisi sana ukilinganisha na wa Dar es Salaam (kwa gari zenye specificationa sawa)

Mfano
Toyota crown
Mwanza nakuta nyingi average milion 8 (zinaanza 7m mpaka 10m hivi) ila dar es salaam average milion 11 (zinaanzia 10m mpaka 13m).

Toyota mark x
Mwanza around 5.5m mpaka 7m, ila Dar es salaam around 8m mpaka 11m

Toyota kluger
Mwanza 9m mpaka 14m.. ila Dar es salaam 14 mpaka 18

Toyota harrier tako la nyani
Mwanza 14m mpaka 18m
Dar 16 - 22m

Sasa ndugu zangu naomba kujua sababu ya utofauti huu mkubwa wa bei! Je madalali wa Dar ni kwamba wanapiga cha juu kingi au watu wa mwanza wana pesa sana ndio sababu wanauza bei ndogo?

Maana nimeshawishika kidogo kununua harrier kwa hawa jamaa wa Mwanza maana bei zao kitonga sana.

Nawasilisha
NGOSHAs inasemekana huwa hawajui depreciation ya mali, wao hawajali hasa kama wanataka hela ya haraka kutoa mahari ama kuoa mwanamke mweupe wa kichagga.
 
Kinachofanya mwanza mandinga yawe bei pow
1.Dalali anakuambia bei husika then anakuomba umuandalie kiposho then n boss anampa kiposho xo akiuza gari unakuta faidaa kapata labda laki 5 kwa pande zotee tofaut na dar mfano Jacktan safari uwa anawek a bei nzuri

2. Demand ya magar mwanza ni ndogoo pia madalali hawana mitaji ya kununua gari used na wapo wachache wenye mitaji km Aisam magari .n. k
 
Dar uswahili mwingi , matapeli , msinunue magari dar utatapeliwa , Wana njaa sana , ukienda dar kununua gari watakuzungusha week Moja bila ya kuona gari ,
 
Madalali wa dar bei zao zinazidi hadi bei za showroom.
Hii Subaru showroom unaipata kwa 19M
IMG_20231223_103020.jpg
 
Back
Top Bottom