Gazeti la Mwananchi la 31 Oktoba 2022 liliripoti habari ya kupatikana mwekezaji mpya wa kuendesha mabasi ya mwendokasi (DART), Kampuni ya Emirates National Group kutoka Falme za Kiarabu.
Taarifa ya serikali kupitia gazeti hilo ilisema kampuni hiyo ingeanza kazi Novemba 2022. Makubaliano ni kwamba; mwanzoni kampuni hiyo itaingiza mabasi 177, na ndani ya miezi 6 (kuanzia Nov 2022) itaingiza jumla ya mabasi 750. Pia, watarejesha mfumo wa malipo ya kadi pekee katika vituo vya mwendokasi.
Hata hivyo, hadi sasa wananchi hatuoni hayo mabasi mapya, hatuoni kuboreshwa kwa huduma ya usafiri wa mwendokasi na wala hatuwaoni watendaji wa Kampuni ya Emirates National Group kutoka Falme za Kiarabu.
Tatizo ni nini? Mbona wananchi hatuelezwi? Waarabu wamepatwa na nini? Kama wameshindwa hatuwezi kupata waarabu wengine wawekeze kwa kuzingatia waarabu wamefanikiwa sana katika sekta ya usafirishaji?
Information is power.
Soma DAR: DART kuondoa tiketi vituo vya Mwendokasi, malipo ya kadi kurejea