Kwanini Mzee Jaji Warioba alirundikiwa vyeo vingi sana enzi ya Mwalimu Nyerere

Kwanini Mzee Jaji Warioba alirundikiwa vyeo vingi sana enzi ya Mwalimu Nyerere

Marekebisho na kwako Jaji Warioba hajawahi kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania. Alikuwa Jaji wa moja wapo ya nchi za jumuiya ya madola, (imenitoka kidogo). Hajawahi kuwa Jaji ndani ya Mahakama ya Tanzania.

Ukiuliza kama hilo linawezekana jibu ni ndio linawezekana.

Mbali na elimu pia Jaji Warioba na Mzee Butiku wana nasaba ya karibu na Mwalimu Nyerere.
Sasa nchi moja ya jumuiya ya madola s Ni Tanzania
 
Mzee alipata kuwa
Jaji Mkuu
Makamu wa Rais
Waziri Mkuu
Mwanasheria Mkuu wa Serikali

Na badae Tena akaja kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Marekebisho ya Katiba

Hivi nauuliza huyu mzee ndio alikuwa msomi pekee na hadi Mwalimu kumpachika vyeo vyote hivyo kasoro uspika?

Nataka kuelewa kwanini walimpachika vyeo hivyo

Je, pension yake si itakuwa inasoma vzr sana kote kote analamba aliko hudumu.

Leo nilikuwa nae kwenye mkutano wa wahariri akifungua kongamano wadau wa habari na uchaguzi ndipo nikawaza aliwezaje kuwa kote kote huko na Ni kipind gani alihudumu.

Katika uongozi wa Nyerere Joseph Sinde Warioba alikuwa Waziri wa Sheria na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Vyeo vingine kama Waziri Mkuu, Makamu wa Rais alivipata wakati wa Mwinyi.

Wakati wa Mkapa aliongoza tume ya kupambana na rushwa.

Wakati wa Kikwete aliongoza tume ya katiba.

Warioba alipata kuwa jaji katika mahakama ya kimataifa ya bahari.

Kote huko aliaminiwa kwa sababu Warioba ni mtu meticulous kwenye sheria na msomi mzuri, kati ya wasomi wa kwanza wa sheria Tanzania. Hii ndiyo batch ya kina Balozi Joshua Opanga na Samuel Sitta, wanafunzi waliogoma hapo UDSM.

Walikuwapo waliomtangulia na kumfundisha kina Julie Manning, lakini kwenye kipindi ambacho Warioba anashika madaraka wao walikuwa wakubwa sana kiumri washastaafu.
 
Unafahamu maana ya kurundikwa?

Kwa muktadha wa swali lako juu ya Jaji Joseph Sinde Warioba, inamaanisha kupachikwa vyeo vingi kwa wakati mmoja.

Unachopaswa kujua ni kuwa, Mzee Sinde alitumikia nafasi hizo kwa nyakati tofauti tofauti kipindi cha utumishi wake.

Mathalani,
.Kuanzia mwaka 1976-1985 ndiyo alikuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali
.Mwaka 1985 mpaka 1990 ndipo alikuwa Waziri Mkuu kipindi cha Hayati Mzee Mwinyi.
.Mwenyekiti wa tume ya Katiba mwaka 2012.

Hajawahi kuwa Jaji Mkuu kama ulivyoainisha hapo juu.

Hakuna kipindi ambacho aliwahi kuwa na vyeo viwili kwa wakati mmoja. Ukiachana na vile vya lazima kama kuwa Mbunge ili uweze kuwa waziri, nk.

Na si yeye tu, viongozi wengi wa Tanzania wamepitia katika nyakati tofauti tofauti za uongozi, na kuwa na vyeo tofauti tofauti katika nyakati za utumishi wao.
Na umakamu wa rais alikuwa kipindi gani kwa ujumla Ni Kwamba ukanda pia ulimbeba sna
 
Hivyo vyeo sio kuhudumu kwa pamoja. Ni nyakati tofauti tofauti. Pia uadirifu wake ndio ilikuwa kigezo cha yeye kuwa ktk utumishi wa aina hiyo kwa nyakati tofauti.

NB;-Tanzania hatuna bahati. Edward Sokoine ilikuwa kipenzi cha Nyerere na Watanzania pia. Angeisogeza Tz. Bahati mbaya ndio vile. Ikaja kwa JPM bahati mbaya nae ndio ikawa vile
 
Na umakamu wa rais alikuwa kipindi gani kwa ujumla Ni Kwamba ukunda pia ulimbeba sna

wakati wa utawala wa chama kimoja KATIBA ilikuwa inaelekeza kwamba Raisi wa Jamhuri akitokea Zanzibar, Waziri Mkuu atalazimika kutoka upande wa Tanzania Bara[Tanganyika], na pia atatambulika kama Makamu wa kwanza wa Raisi. Ndio maana Mzee Warioba, Mzee Malecela, na Mzee Msuya, wanatambulika kama Makamu wa Kwanza wa Raisi wastaafu.
 
kipindi huko nyuma vyeo vya Waziri wa Sheria, na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, vilikuwa vimeunganishwa. Nakumbuka Joseph Warioba, na Damian Lubuva, waliwahi kushika nafasi ya Waziri wa Sheria, na Mwanasheria Mkuu wa Serikali. suala la Warioba kuitwa Jaji ni kwasababu alihudumu ktk tribunal ya kimataifa ktk masuala ya sheria za maji na bahari. wako baadhi ya wanasheria wanaamini Warioba hapaswi kuitwa Jaji kwasababu hakuwahi kuhudumu ktk mahakama ya Tanzania.
 
Mzee alipata kuwa
Jaji Mkuu
Makamu wa Rais
Waziri Mkuu
Mwanasheria Mkuu wa Serikali

Na badae Tena akaja kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Marekebisho ya Katiba

Hivi nauuliza huyu mzee ndio alikuwa msomi pekee na hadi Mwalimu kumpachika vyeo vyote hivyo kasoro uspika?

Nataka kuelewa kwanini walimpachika vyeo hivyo

Je, pension yake si itakuwa inasoma vzr sana kote kote analamba aliko hudumu.

Leo nilikuwa nae kwenye mkutano wa wahariri akifungua kongamano wadau wa habari na uchaguzi ndipo nikawaza aliwezaje kuwa kote kote huko na Ni kipind gani alihudumu.

Mpaka utangulize neno ''mzee''? Hili ni Magufuli aliwakaririsha wabongo na wengi wameiga. Just say Jaji Warioba watu wataelewa.
 
Na umakamu wa rais alikuwa kipindi gani kwa ujumla Ni Kwamba ukanda pia ulimbeba sna
Wewe unaonekana ni hawa wa shule za kata? Maswali unayouliza haya-make sense hata kidogo. Kwa mfano unasema alilundikiwa vyeo wakati siyo. Tena unahoji pension yake itakuwa kubwa eti kwa sababu alifanya kazi sehemu mbali mbali (yaani una-asume kila cheo kina pension yake). Unasema alibebwa na ukanda, wakati huyu ni mmoja ya wasomi wa kweli wa Tanzania.
 
Hivyo vyeo sio kuhudumu kwa pamoja. Ni nyakati tofauti tofauti. Pia uadirifu wake ndio ilikuwa kigezo cha yeye kuwa ktk utumishi wa aina hiyo kwa nyakati tofauti.

NB;-Tanzania hatuna bahati. Edward Sokoine ilikuwa kipenzi cha Nyerere na Watanzania pia. Angeisogeza Tz. Bahati mbaya ndio vile. Ikaja kwa JPM bahati mbaya nae ndio ikawa vile
Tuna sikitika snaa
 
Wewe unaonekana ni hawa wa shule za kata? Maswali unayouliza haya-make sense hata kidogo. Kwa mfano unasema alilundikiwa vyeo wakati siyo. Tena unahoji pension yake itakuwa kubwa eti kwa sababu alifanya kazi sehemu mbali mbali (yaani una-asume kila cheo kina pension yake). Unasema alibebwa na ukanda, wakati huyu ni mmoja ya wasomi wa kweli wa Tanzania.
Sasa nikuulize swla la kitoto sna ,je Ni cheo kipi kwa SAS ndio inamlipa pensions Kama alikuwa na byeo karibia vyote muhumi kupewa pension
 
Joseph Sinde Warioba (born September 3, 1940) served as Prime Minister of Tanzania from 1985 to 1990. Furthermore, he served concurrently as the country's Vice President. He has also served as a judge on the East African Court of Justice, and as chairman of the Tanzanian Constitutional Review Commission.

Following his tenure as prime minister, Warioba served as a judge on the Hamburg, Germany-based International Tribunal for the Law of the Sea from 1996 to 1999. Furthermore, in 1996, President Benjamin Mkapa appointed him as chairman of the Presidential Commission Against Government Corruption, better known as the Warioba Commission.

Warioba was chosen to lead the Commonwealth Observer Group in the April 2007 Nigerian elections.[1] He gave a positive assessment of the elections, deeming them to be progress while also saying that there were irregularities.[2]

Following President Jakaya Kikwete's announcement for a referendum for Tanzania's constitution in 2014, he appointed Warioba as the Chairperson of the Constitutional Review Commission (CRC).

Warioba was appointed in November 2016 by the President of Tanzania John Magufuli as the Chancellor of Sokoine University of Agriculture in Morogoro, Tanzania.

SOURCE: WIKIPAEDIA.
 
Nyerere na Warioba ni wazaliwa wa Mkoa wa Mara.

Pia hili ni jibu la ni kwanini wajeda wengi wanatokea Mkoa wa Mara.

Hata Bongo Movie sehemu ya mjeda ni lazima usikie lafudhi ya Kanda Maalaum ya Tarime na Rorya.
 
Back
Top Bottom