Kwanini Mzee Jaji Warioba alirundikiwa vyeo vingi sana enzi ya Mwalimu Nyerere

Kwanini Mzee Jaji Warioba alirundikiwa vyeo vingi sana enzi ya Mwalimu Nyerere

Naomba kujuzwa alikua makamu wa Rais miaka ipi? Mbona sifahamu hili?
 
Hapana, hajawahi kuwa Jaji wa Tanzania. Ndo maana hana hata kesi moja aliyowahi sikiliza Tz. Kuna kesi fulani ya mambo ya uchaguzi alishitakiana na kama sio Lyatonga Mrema basi ni Steven Wasira
Warioba alishitakiana na Steven Masatu Wasira kwenye kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi Jimbo la Rorya, na siyo Lyatonga.

Japo sikumbuki hukumu za Jaji Warioba, ila huyu mwamba ni mwanasheria na aliteuliwa kuwa Jaji.

Whether amesikiliza kesi na au kutoa hukumu au la, haiondoi wala kupunguza ukweli kwamba alikuwa Jaji.
 
Mzee alipata kuwa
Jaji Mkuu
Makamu wa Rais
Waziri Mkuu
Mwanasheria Mkuu wa Serikali

Na badae Tena akaja kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Marekebisho ya Katiba

Hivi nauuliza huyu mzee ndio alikuwa msomi pekee na hadi Mwalimu kumpachika vyeo vyote hivyo kasoro uspika?

Nataka kuelewa kwanini walimpachika vyeo hivyo

Je, pension yake si itakuwa inasoma vzr sana kote kote analamba aliko hudumu.

Leo nilikuwa nae kwenye mkutano wa wahariri akifungua kongamano wadau wa habari na uchaguzi ndipo nikawaza aliwezaje kuwa kote kote huko na Ni kipind gani alihudumu.

Samahani mtoa mada. Naomba niende nje ya mada japo kwa muda.
Leo naona mzee kavaa koti. Hii kawaida yake. Sijamwona kwenye mwonekanao huu wa mavasi kwa muda mrefu sana.
 
Warioba alishitakiana na Steven Masatu Wasira kwenye kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi Jimbo la Rorya, na siyo Lyatonga.

Japo sikumbuki hukumu za Jaji Warioba, ila huyu mwamba ni mwanasheria na aliteuliwa kuwa Jaji.

Whether amesikiliza kesi na au kutoa hukumu au la, haiondoi wala kupunguza ukweli kwamba alikuwa Jaji.
Nakubaliana na wewe kuwa kutosikiliza kesi hakuondoi Ujaji wa Jaji husika. Sikuwa na kumbukumbu nzuri juu ya hii kesi ya uchaguzi ndio maana nikasema aliwahi kuwa na kesi ya uchaguzi na mmoja kati ya hao Mrema na Wasira.

Ila nakukatalia wazi kabisa kuwa Jaji Warioba hajawahi kuteuliwa na raisi yoyote Tanzania hii kuwa Jaji wa Mahakama Kuu au hata Mahakama ya Rufaa.

Hajawahi kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania.
 
Duh sawa ,Sasa alihudumu kwa Muda gani ktk ofc zote
Kwani alikuwa navyo wakati mmoja? Mnaulizaga masuali gani hayo? Kumbuka nafasi ya waziri mkuu enzi zake ilikuwa nafasi moja na Makamu wa Rais, iliitwa Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais. Wakati huo Rais wa Serekale ya Zanzibar akiwa Makamu wa Pili wa Rais.
 
Mzee alipata kuwa
Jaji Mkuu
Makamu wa Rais
Waziri Mkuu
Mwanasheria Mkuu wa Serikali

Na badae Tena akaja kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Marekebisho ya Katiba

Hivi nauuliza huyu mzee ndio alikuwa msomi pekee na hadi Mwalimu kumpachika vyeo vyote hivyo kasoro uspika?

Nataka kuelewa kwanini walimpachika vyeo hivyo

Je, pension yake si itakuwa inasoma vzr sana kote kote analamba aliko hudumu.

Leo nilikuwa nae kwenye mkutano wa wahariri akifungua kongamano wadau wa habari na uchaguzi ndipo nikawaza aliwezaje kuwa kote kote huko na Ni kipind gani alihudumu.

Mwongo mkubwa wewe; nadhani una ajenda yako binafsi hapa.

Wakati wa Nyerere Warioba alianza kama mwanasheria wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaama kabla ya kuwa mwanasheria wa Serikali (ambayo ni nafasi ya kawaida kwenye kundi la wanasheria wengi wa serikali). Nyerere alimteua kuwa mwanasheria mkuu wa Serikali kutokana na mapendekezo ya Jullie Manning aliyekuwa waziri wa wa kwanza wa kike kuongoza wizara; Julie Manning na Waryoba walikuwa cream ya kwanza ya wanasheria wa kitanganyika kutunukiwa digrii za sheria kutoka Dar es Salaam University College of London.

Wakati akiwa Mwqansheria mkuu ndipo alipoteuliwa kuwa Waziri wa Sheria kuziba nafasi iliyokuwa imeachwa na Julie Manning; ambayo ndiyo nafasi ya mwisho kubwa kwa waryoba kushika wakati wa utawala wa Nyerere.

Sesa wewe hivyo vyeo vya Jaji Mkuu, Makamu wa rais, waziri Mkuu sijui unevitoa wapi wakati inajulikana kuwa Mawazir wakuu wakati wa Nyerere walikuwa ni Kawawa, Msuya na Sokoine tu, Makamu wa raius nao walikuwa ni Krume, Jumbe na Mwinyi tu.

Ningekuwa modereta, ningekuwa nafuta hizi thread zinazonazishwa zikiwa zinasadidia kusambza habari za uwongo badala ya kuelimisha jamii.
 
Alikuwa jaji wa International tribunal inayodeal na Marine Conflicts huko ujerumani
Marekebisho na kwako Jaji Warioba hajawahi kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania. Alikuwa Jaji wa moja wapo ya nchi za jumuiya ya madola, (imenitoka kidogo). Hajawahi kuwa Jaji ndani ya Mahakama ya Tanzania.

Ukiuliza kama hilo linawezekana jibu ni ndio linawezekana.

Mbali na elimu pia Jaji Warioba na Mzee Butiku wana nasaba ya karibu na Mwalimu Nyerere.
 
Back
Top Bottom