KERO Kwanini N-CARD hawana App inayowezesha abiria kutop-up balance bila kupanga foleni?

KERO Kwanini N-CARD hawana App inayowezesha abiria kutop-up balance bila kupanga foleni?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Wakazi wa Kigamboni kwa muda mrefu tumekuwa tukitumia Vivuko vipya ambavyo ni vya Azam maarufu kama SeaTax kazi yao ni nzuri, lakini kuna hii Kampuni N-CARD ambayo imekuwa ikihudumia upande wa hizi card zinazotumika kukata ticket ili uweze kuvuka.

Kinachonishangaza kwa kipindi cha digital transiformation na hasa ukizingatia wakazi asilimia kubwa ya Kigamboni pia ni wanafunzi wa vyuo vikuu, lakini cha ajabu kumekuwa na kero ya upangaji foleni kwa ajili ya kutop-up balance kwenye card.

Nashindwa kuelewa ni nini kinaendelea mpaka App yao ambayo huko nyuma ilikuwepo wakaifunga na kusababisha abiria walazimike kupanga foleni kuwekewa balance badala ya kutumia application kutop-up balance.

Yani karne hii kweli mtu unachelewa kazini kwa kupanga foleni ili ujaze salio kwenye card?

N-CARD mnafeli wapi? Hii ni kero sana.

Ufafanuzi wa Selcom soma hapa ~ Selcom: Unaweza kuweka salio kwenye N-CARD yako kwa kutumia Selcom Pesa
 
Back
Top Bottom