Ayatollah na wadau wake walisema sababu ya kurusha makombora ni
1: Kisasi kwa kiongozi wa Hamas aliyeuwawa ndani ya ardhi yake na watu wanaodhaniwa ni waisrael.
2: Kuuwawa kwa kiongozi wa Hesbullah huko Lebanoni.
Ukiangalia sababu hizo zote hazina mashiko ukilinganisha sababu za mashambulizi ya kwanza baada ya kushambuliwa kwa ubalozi wake Syria. Ile ilijulikana ni ndege za Israel ndio zimelipua.
Kwa nini kakurupuka sasa.
1: Kiongozi wa Hamas aliuwawa na hakuna mtu aliyejitangaza kuhusika ikiwemo israel. Hata kama ni Israel ile ilikuwa ni misheni ya kijasusi qmbayo haikuacha nyayo nyuma. Huwezi kuitumia kama ushahidi kwa dunia nzima. Hawakuonyesha ushahidi usio nashaka kuwa Israel kahusika.
2: Hesbullah iko Lebanon . Ilitakiwa nchi ya Lebanon na Jeshi lake ndio lijibu au liiombe Iran iijibie kwa sababu ardhi yake ndio imeshambuliwa sio Iran. Kama Hezbullah ni tawi la Jeshi la Iran, Kiongozi wa Iran ameshasema Hesbullah wanajiweza wala hawahitaji msaada wa Iran. Hivyo wangewqacha Hesbullah wajibu au wawape hayo makombora wahusika.
Mtazamo wangu, Iran wamekurubuka, wamejibu kijadi sana.
Kama wanaushahidi wa kishushushu kuwa kiongozi wa hamas au Rais wao aliuwawa na Israel na hauwezi kutosha kusadikisha dunia, walipaswa na wao kujibu kishushushu. Iran ni moja ya nchi yenye Intelijensia kali sana. Walipaswa na wao kumuondoa Netanyahu kimyakimya bila kujitangaza. Kujibu hujuma kwa hujuma.
Kama wanawapenda sana Hezbullah (fimbo yao ya kuitesea Israel), walipaswa wapenyeze hayo makombora kwa Hesbullah au wayemen wajibu hukohuko, Maana kiongozi wa Hesbullah sio kiongozi wa Iran.