Akotia
JF-Expert Member
- Dec 16, 2016
- 528
- 1,241
Habari wakuu,
Mi nimzaliwa wa kwanza Kwa single mother(Mkristo) ambaye alikua anafanya kazi za ndani Kwa wa'arabu(DSM). Mama yangu aliofanya kazi Kwa wale waarabu ikiwemo, kuwaanda watoto shule, kuwapikia familia na wafanyakazi, kusafisha nyumba na kuhakikisha usalama wa nyumba(wakisafiri).
Mama angu alianza kazi baada ya kuachika Kwa Mzee wangu wakati Mimi Nina miaka 4,shule ya msingi nilisoma kinondoni mpaka darasa la 3 ndipo Waarabu kupitia kumuonea huruma mama'angu wakaamua kunisomesha wao private school kuanzia la nne kwenye shule mpya na Bora Yemen English medium(chang'ombe opposite na DUCE,2003) kuanzia la nne mpaka la Saba(2006) bila kulipia chochote na nilifaulu secondary kigamboni ila wakaendelea kunidhamini secondary private nilisoma shaaban Robert (form 1-4) mpaka nilipofaulu A level Tanga school.
Kipindi chote hiko mama'angu alikua akirudi kazini anarudi na misosi,wakitoa sadaka tunapewa,nguo za mitumba, nilikua na marafiki na connection yao, sikujiona mpweke.
Mpaka leo hii najitegemea ila msaada wao nikiuhitaji naupata,wale waarabu hawakujali kabila langu au nilipotokea. Nilicheza na watoto wao(mpaka Leo washkaji), nilitumia toys zao wakati mdogo, niliendesha magari Yao,tulialikwa harusi zao, walikuja misiba yetu na kadhalika.
Hata maramoja sikuwahi kujihisi kama wao watu tofauti na sisi na sijawahi kuona watu wanaoutumia utajiri wao kuwasaidia masikini kama wao. Nimekuja mkubwa hivi na Akili zangu ndio nagundua Ile familia ilisaidia, kusomesha, kutibia familia nyingi sana masikini. Ile familia ya kiarabu ilinifundisha UTU na kua HUMBLE sababu maisha haya yanapita tu.
Japo mama'angu kastafu kUfanya kazi ila hata leo zile connection nilizopata Kwa kusoma zile shule tu walizonisaidia waarabu zinasaidia sana, leo hii Nina marafiki matajiri (ambao ni marafiki kweli), marafiki walio nje ya Nchi (wana ni appreciate), marafiki walisoma sana,wenye nyadhifa mbali mbali sector binafsi na serikalini. Sipati picha ningesoma kayumba kama uwezo wa mama angu maana.