Kwanini nashindwa kuwachukia Waarabu

Kwanini nashindwa kuwachukia Waarabu

Na wale wanaowaua waafrika weusi kule marekani ni wazungu pia. Muache jamaa atoe ushuhuda usipende kufafanisha.
Ni kweli ,jamaaa alikuja kutoa ushuhuda wake huyu mtu anakuja kumuponda,na sio kweli wale wanaojitoa muhanga wana malengo ya kuenda peponi ,yale mengine ni maslahi ya watu ,uislamu haujahalalisha kuuuwana.
 
Kwanini upalilie tangazo la kujikomba sana kwao Waarabu?

Eleza sababu zisizopungua 100, kwanini pamoja na kujipendekeza kote kwao bado tu wanatuona waafrika ni nyani [emoji848]

Sent from my CPH2185 using JamiiForums mobile app
Mkuu nadhani umechanganya kidogo
Hii dhana ya unyani imeletwa na somebody darwin kama sikukosea ambaye ni mzungu,
Kama kuna mwarabu anamwita mweusi nyani huuo atakuwa sio mwarabu mwislamu,
Si unajua wapo waarabu sio waislamu?
 
Habari wakuu
Mi nimzaliwa wa kwanza Kwa single mother(mkristo) ambaye alikua anafanya kazi za ndani Kwa wa'arabu(DSM). Mama yangu aliofanya kazi Kwa wale waarabu ikiwemo,kuwaanda watoto shule,kuwapikia familia na wafanyakazi,kusafisha nyumba na kuhakikisha usalama wa nyumba(wakisafiri).

Mama angu alianza kazi baada ya kuachika Kwa Mzee wangu wakati Mimi Nina miaka 4,shule ya msingi nilisoma kinondoni mpaka darasa la 3 ndipo waarabu kupitia kumuonea huruma mama'angu wakaamua kunisomesha wao private school kuanzia la nne kwenye shule mpya na Bora Yemen English medium(chang'ombe opposite na DUCE,2003) kuanzia la nne mpaka la Saba(2006) bila kulipia chochote na nilifaulu secondary kigamboni ila wakaendelea kunidhamini secondary private nilisoma shaaban Robert (form 1-4) mpaka nilipofaulu A level Tanga school.

Kipindi chote hiko mama'angu alikua akirudi kazini anarudi na misosi,wakitoa sadaka tunapewa,nguo za mitumba,nilikua na marafiki na connection Yao, sikujiona mpweke.

Mpaka Leo hii najitegemea ila msaada wao nikiuhitaji naupata,wale waarabu hawakujali kabila langu au nilipotokea. Nilicheza na watoto wao(mpaka Leo washkaji),nilitumia toys zao wakati mdogo,niliendesha magari Yao,tulialikwa harusi zao,walikuja misiba yetu na kadhalika.

Hata maramoja sikuwahi kujihisi kama wao watu tofauti na sisi na sijawahi kuona watu wanaoutumia utajiri wao kuwasaidia masikini kama wao. Nimekuja mkubwa hivi na Akili zangu ndio nagundua Ile familia ilisaidia,kusomesha,kutibia familia nyingi sana masikini. Ile familia ya kiarabu ilinifundisha UTU na kua HUMBLE sababu maisha haya yanapita tu.

Japo mama'angu kastafu kUfanya kazi ila hata Leo zile connection nilizopata Kwa kusoma zile shule tu walizonisaidia waarabu zinasaidia sana,Leo hii Nina marafiki matajiri(ambao ni marafiki kweli),marafiki walio nje ya Nchi(wana ni appreciate),marafiki walisoma sana,wenye nyadhifa mbali mbali sector binafsi na serikalini. Sipati picha ningesoma kayumba kama uwezo wa mama angu maana.
Hongera sana kwa kuleta ushuhuda huu hapa, wabaya watajifunza kuwa wema na tbia za wana choyo zinaweza kuwabadilisha tokana na story yako hiii
 
Point ni ile ile, duniani tupo wema na wabaya, mtu akija kukwambia waarabu, wazungu au waafrika ni wabaya basi kuna tatizo hapo, inawezekana huyo mtu ana tatizo au kikundi kidogo flani cha jamii flani kina tatizo so haimaanishi kuwa jamii ile yote iko vile
Point pia
 
Hao waliokufanyia hivyo ni asilimia ngapi ya waarabu waliopo duniani?

Yule aliyemnyea binadamu mwenzie mdomoni ni Mwarabu pia

Wale wanaojitoa mhanga kufa na watu wengine wakiamini watapata thawabu akhera pia ni waislam.

Dunia imejaa na maovu mengi, kwa uzi wa mleta mada naamini inaonyesha kuwa utu pia upo
 
Habari wakuu
Mi nimzaliwa wa kwanza Kwa single mother(mkristo) ambaye alikua anafanya kazi za ndani Kwa wa'arabu(DSM). Mama yangu aliofanya kazi Kwa wale waarabu ikiwemo,kuwaanda watoto shule,kuwapikia familia na wafanyakazi,kusafisha nyumba na kuhakikisha usalama wa nyumba(wakisafiri).

Mama angu alianza kazi baada ya kuachika Kwa Mzee wangu wakati Mimi Nina miaka 4,shule ya msingi nilisoma kinondoni mpaka darasa la 3 ndipo waarabu kupitia kumuonea huruma mama'angu wakaamua kunisomesha wao private school kuanzia la nne kwenye shule mpya na Bora Yemen English medium(chang'ombe opposite na DUCE,2003) kuanzia la nne mpaka la Saba(2006) bila kulipia chochote na nilifaulu secondary kigamboni ila wakaendelea kunidhamini secondary private nilisoma shaaban Robert (form 1-4) mpaka nilipofaulu A level Tanga school.

Kipindi chote hiko mama'angu alikua akirudi kazini anarudi na misosi,wakitoa sadaka tunapewa,nguo za mitumba,nilikua na marafiki na connection Yao, sikujiona mpweke.

Mpaka Leo hii najitegemea ila msaada wao nikiuhitaji naupata,wale waarabu hawakujali kabila langu au nilipotokea. Nilicheza na watoto wao(mpaka Leo washkaji),nilitumia toys zao wakati mdogo,niliendesha magari Yao,tulialikwa harusi zao,walikuja misiba yetu na kadhalika.

Hata maramoja sikuwahi kujihisi kama wao watu tofauti na sisi na sijawahi kuona watu wanaoutumia utajiri wao kuwasaidia masikini kama wao. Nimekuja mkubwa hivi na Akili zangu ndio nagundua Ile familia ilisaidia,kusomesha,kutibia familia nyingi sana masikini. Ile familia ya kiarabu ilinifundisha UTU na kua HUMBLE sababu maisha haya yanapita tu.

Japo mama'angu kastafu kUfanya kazi ila hata Leo zile connection nilizopata Kwa kusoma zile shule tu walizonisaidia waarabu zinasaidia sana,Leo hii Nina marafiki matajiri(ambao ni marafiki kweli),marafiki walio nje ya Nchi(wana ni appreciate),marafiki walisoma sana,wenye nyadhifa mbali mbali sector binafsi na serikalini. Sipati picha ningesoma kayumba kama uwezo wa mama angu maana.
Huu uzi una connection na uzi mwingine? Kama ndiyo ebu ziunge basi. Kama sivyo mm sijapata logic.
 
Point ni ile ile, duniani tupo wema na wabaya, mtu akija kukwambia waarabu, wazungu au waafrika ni wabaya basi kuna tatizo hapo, inawezekana huyo mtu ana tatizo au kikundi kidogo flani cha jamii flani kina tatizo so haimaanishi kuwa jamii ile yote iko vile
Wewe uko sahihi
 
Hao waliokufanyia hivyo ni asilimia ngapi ya waarabu waliopo duniani?

Yule aliyemnyea binadamu mwenzie mdomoni ni Mwarabu pia

Wale wanaojitoa mhanga kufa na watu wengine wakiamini watapata thawabu akhera pia ni waislam.
Wewe ni mpumbavu punguani... hilo neno WAISLAM limeingiaje hapa
 
Maisha yangu sijawahi kuona ubaya wa Waarabu. Niliokwisha kutana nao wanapenda urafiki na wanaongea real siyo kinafiki tofauti na wadosi.
 
Kufanya kwa hao wazungu haiwapi kibali Waarabu kuwanyanyasa watu weusi

Wote ni Wapumbavu tu, no matter ni Mwarabu au Wazungu...sioni sababu ya kuwaweka Wazungu kwny mada hii
 
Waarabu wa magomeni wenye nywele ngumu, pua pana na spread lips wamepanic sana kwenye mada hii [emoji23][emoji23]
 
Mshukuru Mwenyezi Mungu kwa yote uliyoyapata mpaka kifikia ulipo, wangekuwa wahindi ungeelewa kwanini waliitwa mapatel
 
Back
Top Bottom