Kwanini nchi haina Kitengo cha Intelijensia ya Uchumi?

Kwanini nchi haina Kitengo cha Intelijensia ya Uchumi?

Tena ilitakiwa kuwa active kama ile ya police kwenye kunusa njama za kigaidi kwenye maeneo ambayo wapinzani wanakusudia kufanya mikutano. Hapa tungekuwa tunanusa hadi upungufu wa dola miaka hata sitini mbele na kujiwekea akiba.

Bei ya mafuta na tozo zisizojulikana mwelekeo wake zisingekuwa za kushtukiza kama ilivyo sasa. Wategemea nyongeza ya mishahara pia tungekuwa tunapewa hali ya miaka hata 20 huko mbele kama ipo au la
Tumaineli alitoa hizi forecast mapema sana, kiashirio kuwa hicho kitengo kipo. Tatizo letu kama kawaida ni hayo haya pewi kipaumbele na Wanasiasa. Nchi yetu the dominant system ni politics kama ilivyo nchi nyingi za mrengo wa kushoto. Nadhani tulikosea tangu mwanzo kwakua ideology yetu ilikuwa siasa kushika hatamu badala ya uchumi kushika hatamu...

Kila kitu hakitokei ki miujiza ni conceptualization kwanza inayounda mfumo, kwahiyo mfumo mzima upo anchored kwenye siasa ndiyo sababu unaona Kuna protection ya hali ya juu kwenye siasa kuliko ilivyo kwenye uchumi....

Training pia ya hao imeegemea zaidi kwenye siasa. Katika sekta ambayo training yake ni very poor ni uchumi, wachumi wetu wengi sana hawajawa trained effectively na consistently, hii ni weakness ya Idara ya uchumi the so called "The University" kwa hiyo miguu na mikono ya kiutendaji Kwa maana ya serikali, haiwezi kufanya kazi vizuri kama kichwa hakifikiri sawasawa
 
Uleule ujuaji wa kishamba! Mkishaangalia series za Kimarekani basi mnajiona na nyie ni majasusi! Nenda TISS kawaulize kama kitengo hiki hakipo?

Ninyi ndiyo bado mnaamini kuwa MOSSAD, CIA, MI6 ndiyo mashirika bora ya kijasusi! Nenda kawaulize wenye taaluma yao wakwambie ukweli!
Hata kama kipo basi kimeonyesha udhaifu wake katika hili. Usimshambulie bila sababu, he has a point
 
Muundo wa Serikali ulivyo ni wazi hatuna kitengo kinachoratibu na kusimamia intelijensia ya uchumi.

Kama mipango yetu ingeongozwa na intelijensia ya uchumi maana yake sera zetu zingeeleweka hadi ngazi ya mtaa ila kwa sasa hata mawaziri hakuna ajuaye tuna threat na opportunity gani kisekta.

Kwanini kitengo hiki kisiundwe ndani ya wizara mpya ya mipango kikichukua majasusi kutoka vyombo vya dola, vyuoni, taasisi binafsi na wizara ya fedha! Kitengo hiki kikiwepo hata mwanasheria mkuu wa serikali hataruhusiwa kwenda kuingia mikataba ya DP world coz watakuwa wanafanya uchambuzi wa kila sekta, kuainisha intervention za kisekta pamoja na kucontrol kiu ya mwanasiasa.

Hiki kitengo ni muhimu sana kwa ulinzi wa uchumi wetu lakini pia kitatusaidia kuwabaini wanaotuhujum na kuwaweka wazi au kuwadhibiti.

Intelijensia ya jinai siyo kipaombele cha Dunia tena; Dunia inalindwa zaidi na economic power. Leo tunapoona kila dili likifeli means hatuna jicho la majasusi wenye business mind. Tuna majasusi wa jinai ambao ni consumers wa public funds kuliko kuimarisha vyanzo vya mkwamuo wa kiuchumi.

Let us invest kwenye ujasusi wa kiuchumi
Kwa ccm hii ya akina mzee wasira uchumi si kipaumbele.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Uko nje ya mada. Hiyo FIU inaangalia money laundering siyo economic Intelligence. Tasks za Economic Intelligence ni kama; search for, find, and collect information, and present information on the economic field for strategic interests in the national, regional and international spheres that are needed as input for determining policies and decision making in the context of national defense and security development
Nje ya mada?. Mkuu moja ya jukumu ni hili hapa
 

Attachments

Kwa ccm uchumi si kipaumbele
Hata kama ni chama changu, huo ndiyo ukweli...Lakini si kosa lake ni kosa la mwanzilishi...Maana huko nyuma ilikuwa Siasa ni Kilimo, mara Azimio la Musoma, mara Azimio la Arusha, yote hayo ni yalijengwa kisiasa zaidi kuliko kiuchumi. Hadi Leo ndiyo sababu mara utasikia BBT humo ndani ni siasa zaidi kuliko uchumi, sijui Kilimo Kwanza huelewi hata ni sera, Azimio au tamko, which means ni siasa zaidi...Watu wanalenga kupata political acknowledgments zaidi kuliko economic gains
 
Nakubaliana na hoja kwamba kuna kitengo labda kinachofanana na hiki ila nadhani ufanisi wake siyo mzuri kutokana na haya yanayotokea kwenye jamii. Kujua mtu ameweka kiasi gani kwenye akaunti yake nakumfuatilia hiyo siyo kazi ya wataalam wa intelijensia ya uchumi hiyo ni kazi ya intelijensia ya jinai kuhusa kama kuna kiatarishi au biashara vya utakatishaji fedha.

Ninaposema intelijensia ya uchumi ninazungumzia mfumo mzima wa biashara NCHINI; kwa zaidi ya wiki mbili sasa kuna changamoto ya kuvuka mpaka wa TUNDUMA; ukisoma mwananchi online namna viongozi wa jeshi la polisi na TRA wanavyosagiana kunguni utabaini tunalo tatizo la maono mapana kibiashara. Polisi wanasema wanaongoza magari kwa utaratibu mzuri ila wanadai mkuu wa TRA katika kituo hicho amezidi kuwa mpole.

At this level; unaamini lango kubwa kama TUNDUMA linalopitisha asilimia kubwa ya mzigo kutoka bandari yetu lipo mikono salama? Polisi wanakiri kwamba scaner za mizigo zinasumbua (tunainhiza fedha kiasi gani hadi tushindwe kutengeneza scaner?)

Lakini pia wataalam wetu wa ujasusi wa kibiashara wameshindwa kabisa kutowapa mwanya washindani wetu kama Mombasa na Beira katika sekta biashara?

Nitatoa mfano wa pili; leo Tanzania ni nchi ya kukamata lakini uchumi wake unajengwa na mabepari wakiwemo wawekezaji. Tumeona namna mabepari wanavyotunyonya katika madini na rasilimali nyingine kupitia mikataba. Haya yanafanyika majasusi wa kiuchumi wakiwa wapi? Kwanini tusiamie sasa kutumia zaidi mbinu za kibepari kuliko mbinu za kijamaa?

So, hoja hapa ni kuamsha watu waanze kujadili na kufungamanisha ujasusi wa kiuchumi na sheria zetu, katiba na sera za nchi. Ujasusi wa kiuchumi siyo siyo siri Duniani ni uwezo wa kubagain na kufanya robbing. That's y makampuni yote makubwa ushinda kesi wanapotuhumiwa kwa rushwa, wizi au udanganyifu .....wameandaa wataalam wanaoweka misingi imara yakisheria kulinda maslahi yake.

Mzee Magufuli alipoona intelijensia ya uchumi imefeli aliamua kutumia intelijensia ya jinai akafanikiwa kiasi kukabiliana na MABEBERU lakini akafeli kwa kiasi kikubwa kwa sababu MABEBERU walielekea kuisaka haki mahakamani.

Hawa watu wanapaswa kuwepo kila sekta ya wapewe meno yakudhibiti nguvu za wanasiasa; wanapaswa kuwepo waimarishe mifumo ya urasimu ya nchi yetu.......nchi inaishiwa urasimu na hivyo mikataba yakupita hatua tano kwa mwaka tunataka isainiwe over night ....badala tuwe na mipango ya muda mrefu sisi tunawaza leo na uchaguzi.

Tujadili eneo hili litasaidie kuimarisha taasisi zetu kuelekea katiba mpya
 
Sekta na takwimu! Cz anakuja kiongoz kutolea ufafanuzi jambo ambalo si sekta yake by professional na kitakwimu kila mmoja huja na takwimu yake!!
chukua takwimu na taarrifa za kiintelijesia za kisekta husika na hizo mara zote ndizo sahihi.

achana na taarrifa za kiintelijesia za simba kutolewa na yanga ama za za ACT kutolewa na CHAUMA.
Taarrifa sahihi, taasisi sahihi.
 
Nchi ina vitengo vingi sana hii... sema tatizo labda ina watu wasiojua kuzitendea haki hizo nafasi.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
chukua takwimu na taarrifa za kiintelijesia za kisekta husika na hizo mara zote ndizo sahihi.

achana na taarrifa za kiintelijesia za simba kutolewa na yanga ama za za ACT kutolewa na CHAUMA.
Taarrifa sahihi, taasisi sahihi.
Hakuna wa kumuamini iwe taasis wala kiongoz!! Taasis hiz mfano tuliambiwa gas ya mtwara inakwenda kumaliza tatizo la umeme, kiko wap 🤣🤣🤣? Amken dunia ishabadilika watanzania wameamka, nendeni na wakat uongo uongo na ujanja ujanja havitowasaidia!!
 
Angalia Mbarali, mwaka jana wamezuia wananchi kulima. Mwaka huu kwenye kampeni Kinana ameona hasira ya wananchi ametangaza mkakati wa kufuta maamuzi ya awali

Maana yake hakukuwa na utafiti kuhusu madhara bali waliishauri kujifurahisha tu
 
Ipo na inafanya kazi vizuri sana labda tu haifanyi kulingana na ambavyo ungependa wewe.

Hiyo idara ipo kila sector, mathalani katika bajeti ya serikali kuu lakini pia hata katika halmashauri intelijensia huashiria watakusanya kiasi gani katika mwaka wa fedha husika.

Lakini pia mfumuko wa bei, Bei ya mafuta, thamani ya sarafu na dola, hali ya hewani, ukiaji wa uchumi, njaa, ukame na hali za maisha ya watu na makazi intelijensia huonyesha ishara ya kukua, kuzorota au kuhatarisha hali za kisekta na hivyo tahadhari ya jumla katika sekta husika hutolewa.
Futa huu ujinga. Yaani halimashauri kuproject watapata mapato gani ndo intelligencia? Hivi kizazi hivi kinaenda wapi kwa akili za hovyo namna hii?
 
sikulazimishi.
bas sawa shupaza shingo vivyo hivyo, hujui kitu, unaeleweshwa unaleta kiburi,kaa ivoivo sasa ebo!😳
Kama kipo performance yake ni poor. Dowans, mikataba mibovu, Richmond, escrow, hicho kitengo kinafanya nini
 
Bring more substantial evidence. Acheni basi porojo zisizokuwa na ushahidi.
Substantial evidence gani wakati mambo ya kifisadi yako wazi kabisa. Inchi inaingia mikataba mibovu tunapata hasara, baadaye inavunjwa tunashitakiwa tunashindwa kesi tunalipishwa billions hasara nyingine tatizo mmeshiba to the level hamuoni umuhimu wa kupigania inchi zaidi ya matumbo yenu
 
Back
Top Bottom