Kwanini nchi haina Kitengo cha Intelijensia ya Uchumi?

Tumaineli alitoa hizi forecast mapema sana, kiashirio kuwa hicho kitengo kipo. Tatizo letu kama kawaida ni hayo haya pewi kipaumbele na Wanasiasa. Nchi yetu the dominant system ni politics kama ilivyo nchi nyingi za mrengo wa kushoto. Nadhani tulikosea tangu mwanzo kwakua ideology yetu ilikuwa siasa kushika hatamu badala ya uchumi kushika hatamu...

Kila kitu hakitokei ki miujiza ni conceptualization kwanza inayounda mfumo, kwahiyo mfumo mzima upo anchored kwenye siasa ndiyo sababu unaona Kuna protection ya hali ya juu kwenye siasa kuliko ilivyo kwenye uchumi....

Training pia ya hao imeegemea zaidi kwenye siasa. Katika sekta ambayo training yake ni very poor ni uchumi, wachumi wetu wengi sana hawajawa trained effectively na consistently, hii ni weakness ya Idara ya uchumi the so called "The University" kwa hiyo miguu na mikono ya kiutendaji Kwa maana ya serikali, haiwezi kufanya kazi vizuri kama kichwa hakifikiri sawasawa
 
Hata kama kipo basi kimeonyesha udhaifu wake katika hili. Usimshambulie bila sababu, he has a point
 
Kwa ccm hii ya akina mzee wasira uchumi si kipaumbele.
 
Reactions: Ame
Nje ya mada?. Mkuu moja ya jukumu ni hili hapa
 

Attachments

Kwa ccm uchumi si kipaumbele
Hata kama ni chama changu, huo ndiyo ukweli...Lakini si kosa lake ni kosa la mwanzilishi...Maana huko nyuma ilikuwa Siasa ni Kilimo, mara Azimio la Musoma, mara Azimio la Arusha, yote hayo ni yalijengwa kisiasa zaidi kuliko kiuchumi. Hadi Leo ndiyo sababu mara utasikia BBT humo ndani ni siasa zaidi kuliko uchumi, sijui Kilimo Kwanza huelewi hata ni sera, Azimio au tamko, which means ni siasa zaidi...Watu wanalenga kupata political acknowledgments zaidi kuliko economic gains
 
Nakubaliana na hoja kwamba kuna kitengo labda kinachofanana na hiki ila nadhani ufanisi wake siyo mzuri kutokana na haya yanayotokea kwenye jamii. Kujua mtu ameweka kiasi gani kwenye akaunti yake nakumfuatilia hiyo siyo kazi ya wataalam wa intelijensia ya uchumi hiyo ni kazi ya intelijensia ya jinai kuhusa kama kuna kiatarishi au biashara vya utakatishaji fedha.

Ninaposema intelijensia ya uchumi ninazungumzia mfumo mzima wa biashara NCHINI; kwa zaidi ya wiki mbili sasa kuna changamoto ya kuvuka mpaka wa TUNDUMA; ukisoma mwananchi online namna viongozi wa jeshi la polisi na TRA wanavyosagiana kunguni utabaini tunalo tatizo la maono mapana kibiashara. Polisi wanasema wanaongoza magari kwa utaratibu mzuri ila wanadai mkuu wa TRA katika kituo hicho amezidi kuwa mpole.

At this level; unaamini lango kubwa kama TUNDUMA linalopitisha asilimia kubwa ya mzigo kutoka bandari yetu lipo mikono salama? Polisi wanakiri kwamba scaner za mizigo zinasumbua (tunainhiza fedha kiasi gani hadi tushindwe kutengeneza scaner?)

Lakini pia wataalam wetu wa ujasusi wa kibiashara wameshindwa kabisa kutowapa mwanya washindani wetu kama Mombasa na Beira katika sekta biashara?

Nitatoa mfano wa pili; leo Tanzania ni nchi ya kukamata lakini uchumi wake unajengwa na mabepari wakiwemo wawekezaji. Tumeona namna mabepari wanavyotunyonya katika madini na rasilimali nyingine kupitia mikataba. Haya yanafanyika majasusi wa kiuchumi wakiwa wapi? Kwanini tusiamie sasa kutumia zaidi mbinu za kibepari kuliko mbinu za kijamaa?

So, hoja hapa ni kuamsha watu waanze kujadili na kufungamanisha ujasusi wa kiuchumi na sheria zetu, katiba na sera za nchi. Ujasusi wa kiuchumi siyo siyo siri Duniani ni uwezo wa kubagain na kufanya robbing. That's y makampuni yote makubwa ushinda kesi wanapotuhumiwa kwa rushwa, wizi au udanganyifu .....wameandaa wataalam wanaoweka misingi imara yakisheria kulinda maslahi yake.

Mzee Magufuli alipoona intelijensia ya uchumi imefeli aliamua kutumia intelijensia ya jinai akafanikiwa kiasi kukabiliana na MABEBERU lakini akafeli kwa kiasi kikubwa kwa sababu MABEBERU walielekea kuisaka haki mahakamani.

Hawa watu wanapaswa kuwepo kila sekta ya wapewe meno yakudhibiti nguvu za wanasiasa; wanapaswa kuwepo waimarishe mifumo ya urasimu ya nchi yetu.......nchi inaishiwa urasimu na hivyo mikataba yakupita hatua tano kwa mwaka tunataka isainiwe over night ....badala tuwe na mipango ya muda mrefu sisi tunawaza leo na uchaguzi.

Tujadili eneo hili litasaidie kuimarisha taasisi zetu kuelekea katiba mpya
 
utofauti uko upande gani kwa mfano?
kisekta, kisera au kitakwimu?
Sekta na takwimu! Cz anakuja kiongoz kutolea ufafanuzi jambo ambalo si sekta yake by professional na kitakwimu kila mmoja huja na takwimu yake!!
 
Sekta na takwimu! Cz anakuja kiongoz kutolea ufafanuzi jambo ambalo si sekta yake by professional na kitakwimu kila mmoja huja na takwimu yake!!
chukua takwimu na taarrifa za kiintelijesia za kisekta husika na hizo mara zote ndizo sahihi.

achana na taarrifa za kiintelijesia za simba kutolewa na yanga ama za za ACT kutolewa na CHAUMA.
Taarrifa sahihi, taasisi sahihi.
 
Nchi ina vitengo vingi sana hii... sema tatizo labda ina watu wasiojua kuzitendea haki hizo nafasi.
 
Reactions: Ame
chukua takwimu na taarrifa za kiintelijesia za kisekta husika na hizo mara zote ndizo sahihi.

achana na taarrifa za kiintelijesia za simba kutolewa na yanga ama za za ACT kutolewa na CHAUMA.
Taarrifa sahihi, taasisi sahihi.
Hakuna wa kumuamini iwe taasis wala kiongoz!! Taasis hiz mfano tuliambiwa gas ya mtwara inakwenda kumaliza tatizo la umeme, kiko wap 🤣🤣🤣? Amken dunia ishabadilika watanzania wameamka, nendeni na wakat uongo uongo na ujanja ujanja havitowasaidia!!
 
Angalia Mbarali, mwaka jana wamezuia wananchi kulima. Mwaka huu kwenye kampeni Kinana ameona hasira ya wananchi ametangaza mkakati wa kufuta maamuzi ya awali

Maana yake hakukuwa na utafiti kuhusu madhara bali waliishauri kujifurahisha tu
 
Futa huu ujinga. Yaani halimashauri kuproject watapata mapato gani ndo intelligencia? Hivi kizazi hivi kinaenda wapi kwa akili za hovyo namna hii?
 
sikulazimishi.
bas sawa shupaza shingo vivyo hivyo, hujui kitu, unaeleweshwa unaleta kiburi,kaa ivoivo sasa ebo!😳
Kama kipo performance yake ni poor. Dowans, mikataba mibovu, Richmond, escrow, hicho kitengo kinafanya nini
 
Bring more substantial evidence. Acheni basi porojo zisizokuwa na ushahidi.
Substantial evidence gani wakati mambo ya kifisadi yako wazi kabisa. Inchi inaingia mikataba mibovu tunapata hasara, baadaye inavunjwa tunashitakiwa tunashindwa kesi tunalipishwa billions hasara nyingine tatizo mmeshiba to the level hamuoni umuhimu wa kupigania inchi zaidi ya matumbo yenu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…