Kwanini nchi haina Kitengo cha Intelijensia ya Uchumi?

Futa huu ujinga. Yaani halimashauri kuproject watapata mapato gani ndo intelligencia? Hivi kizazi hivi kinaenda wapi kwa akili za hovyo namna hii?
hiyo ni intejensia, unachofikiri wew ni kitu kingine kabisa,

skiza, hata ukitaka kufungua biashara yako Lazima utumie intelijensia ya kiuchumi kujua utapata faida au hasara katika eneo husika.
Lazima uwe na intelijensia kujua kuna wateja au hukuna, wanahitaji bidhaa hii au ile.

unaelekezwa, unashupaza shingo akati hujui kitu.
kaa ivoivo ivo na mitusi na ujinga wako
 
My friend nchi yetu hakuna kitu inachokosa, Intellijensia ya uchumi tunayo iliyosheheni wataalam wabobezi!.

Tatizo tulilonalo maamzi mengi yanategemea msukumo wa kisiasa ambapo manyang'ani na wabinafsi walioshikiria hatamu ushauri wa kitaalam hufunikwa na kufanya yale yanayowanufaisha wao tu na kupelekea haya unayoyaona yanayotutia aibu!.
 
Angalia Mbarali, mwaka jana wamezuia wananchi kulima. Mwaka huu kwenye kampeni Kinana ameona hasira ya wananchi ametangaza mkakati wa kufuta maamuzi ya awali

Maana yake hakukuwa na utafiti kuhusu madhara bali waliishauri kujifurahisha tu
Kinana Hana jinsi kwakua asipofanta hivyo wanapoteza kura. Tatizo siyo Kinana, Bali mfumo mzima wa nchi na siasa zetu.
 
Kuna watanzania wengi sana wamefilisika kwasababu ya kushindwa kulindwa katika biashara zao na huo ufilisi unafanywa na mafia wachache ambao wanataka kuhodhi utajiri wa nchi hii. Mtu anayedharau intelijensia ya uchumi hajui hata huo uchumi unaathirika vipi locally na globally
 
Hii kazi ya afisa mdogo kabisa aliyesomea certificate ya marketing and sales ndiyo unaita intelijensia?

Nahama nchi. Vijana mna dharau sana.
 
Hii kazi ya afisa mdogo kabisa aliyesomea certificate ya marketing and sales ndiyo unaita intelijensia?

Nahama nchi. Vijana mna dharau sana.
intelijensia inaonyesha unanyapia nyapia wanafunzi sio tu wa certificate ya marketing hadi wa shule ya msingi, utaozea jela, shauli yako, acha tamaa

intelijensia inaonyesha una pia una muda mrefu hujafanya ibada na bado utaendelea kukwepa ibada kwa kipindi kirefu kijacho tunafatilia na kuweka mtego ili ufanye ibada
 
Pumbavu
 
Wapi wewe ,? , Intelijensia ya uvccm labda
 
Vilaza hawa ,hamna wanachojua kwenye issues za uchumi .
Inapoteza muda tu
 
Intelijensia ya uchumi ni kitengo ambacho inabidi kuwe kama mboni ya jicho la taifa ,
Unafikiri nchi zilizoendelea zimefika pale kimiujiza ?
Wana watu na vitengo nyeti vya uchambuzi na intelligence ya uchumi na kutengeneza mikakati ya kuwezesha maendeleo ya kila sekta katika nchi ,kwa wenzetu hawa watu ndio final say kuhusu sera za kiuchumi .
Hapa mataaahira wasio na upeo wala weledi wowote wanafanya maamuzi yanayo affect uchumi na maendeleo ya mwananchi negatively kila siku , yet tupo tu na tunaona kawaida .
Taifa la maiti Tanzania
 
Huwezi kuwa na kitengo cha Financial and economics intelligence Halafu kila siku tunaingia mikataba ya kimangungo inayofilisi nchi ,tunaingia mikataba ya kipuuz at the end tunalipa mabilioni ya pesa kama fidia kwa kuvunja mikataba hiyo ,pesa ambazo zingeweza kutumika kuendeleza nchi .
Tunashindwa kutengeneza sekta komavu za kiuchumi ambazo zinaweza kuwa engine ya ukuaji wa uchumi wa mwananchi halafu mtu anasema kuna kitengo ya intelijensia ya uchumi , labda intelijensia ya kushibisha matumbo yenu
 
Nchi hii haina hata clear vision ,tunataka nini ,kwa nini ,na tunaweza fanikisha vipi .
Hizo visions zote za kiuchumi huwa zinatengenezwa na hao watu .
 
Hiki kitengo ni kipana sana na muhimu ,kwa nchi za wenzetu wanatengeneza mpaka majasusi na mapandikizi huko kwenye mataasisi makubwa nje ya nchi kwenda kuiba utaalamu na technology ili itumike kufaidisha taifa .
Wanaenda mbali hata kuunda na kutekeleza mbinu za kufanya makampuni yanayomilikiwa na wazawa yakue na kutanuka zaidi hadi nje ya nchi na hivyo kukuza pato la taifa .
Hizo zote ni kazi za Economics intelligence .
Hadi mbinu za rafu dhidi ya washindani wa taifa letu katika sekta flani zinaweza tengenezwa ili kuwashinda ,mfano sisi na Kenya katika sekta ya bandari , hawa jamaa wanaweza tengeneza mbinu hata za kuhujumu sekta ya bandari Kenya huku yetu tukizidi kuikuza zaidi ili mwisho wa siku kuwa dorminant kwenye hiyo sekta then tunapata mapato zaidi hata ambayo mshindani wetu Kenya alikuwa anayapata
 
Ukiachana masuala ya intelegensia ya uchumi. watu wanafanya Mambo ya ovyo kule maofisini... Watu wanapiga pesa.., rushwa ipo nje nje. Watu wanawachomeka ndugu zao. Ukipelekwa central police kama pochi yako inasoma kesi hamna hata kama ushahidi upo. Mtaani wauza Ganda Wana protection ya washikaji zao mapolisi. Hata akichomeshwa siku mbili yupo mtaani tena anaendelea na biashara zake. Vijana wako hoi bin taabani.., ajira hamna, hamna uwezeshwaji wala mkakati wowote wa kuwasaidia vijana zaidi ya porojo na propaganda tu. Hii pia hainekani kama ni threat dhidi ya uhai na usalama na wa taifa au tishio dhidi usalama wa taifa ni pale tu inapotaka kupinduliwa serikali ya CCM. TISS wanafanya kazi gani...! kama hivi vitu watu wanavifanya bila uoga. Au ni ile informer wa TISS mwenyewe kwenye kila taasisi anajilikana, washikaji wakitaka kupiga bingwa wanamwendea na kumkatia kidogo...!
Kutokuwepo kwa haki na usawa, ukandamizaji na utawala mbovu nao ichukuliwe kama threat dhidi ya usalama na uhai wa Taifa(Ni mtazamo Tu...!)
 
Kwanza anawajua fsb au kgb muulize hivyo😂😂😂
 
Kama kipo basi akipo active kwenye maswala nyeti ya taifa,ilikuaje tukarudishiwa chenji ya rada au wanyama wanatoroshwa wengine wakiwa hai!,madini n,k
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…