Kwanini nchi nyingi za Afrika wanatumia lugha za wakoloni kama lugha za taifa, hivi hawaoni aibu?

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2013
Posts
38,920
Reaction score
44,970
Kutumia lugha ya mkoloni kwa shughuli mbali mbali hasa zisizoepukika kwa sasa, mfano masomo ya sayansi, sioni kama ni shida sana.

Shida yangu ni lugha ya mkoloni kufanywa kuwa ndio lugha ya taifa na inatumika mtaani hadi na wauza nyanya, ambao wangezweza kutumia lugha yao wenyewe kwenye masuala kama hayo.

Niwapongeze Kenya kwa kukifanya kiswahili kuwa lugha ya taifa lao, sina hakika juu ya Uganda,DRC kama wanampango juu ya kufanya kiswahili lugha ya mataifa yao. Bila kuisahau mikoa ya kaskazini magharibi mwa Tz, ya Rwanda na Burundi.

Hebu oneni hata aibu jamani, seriously..
 
Kwa asili yetu ki Africa kutokana na kuwa na ethnic groups ambazo zilikuwa (zipo) very diverse ilifaa kupata lugha moja ya kuunganisha watu.

Kwakuwa imagine sasa nchi ina zaidi ya ethnic groups 200+ na kila mtu aongee lugha yake hapo pasingekalika. Hata kuleta umoja wa kitaifa isingekuwa rahisi.
 
Hicho ulichokiongea hapo umekiongea kirahisi sana na umesahau kama ni kitu cha kimchakato. Umesahau kama katika jamii yako anaeongea lugha hiyo unayoita ya mkoloni ndio anaonekana mstaarabu aliyestaarabika kuliko anaengea lugha ya asili? By the way, kwani sisi lugha yetu ya asili ni kiswahili au vilugha vyetu kama kimakonde, kijita, kichaga na kadharika? Kwahiyo na sisi tuone aibu sio?
 
Kutumia lugha ya mkoloni kwa shughuli mbali mbali hasa zisizoepukika kwa sasa, mfano masomo ya sayansi, sioni kama ni shida sana.

Shida yangu ni lugha ya mkoloni kufanywa kuwa ndio lugha ya taifa na inatumika mtaani hadi na wauza nyanya, ambao wangezweza kutumia lugha yao wenyewe kwenye masuala kama hayo.

Niwapongeze Kenya kwa kukifanya kiswahili kuwa lugha ya taifa lao, sina hakika juu ya Uganda,DRC kama wanampango juu ya kufanya kiswahili lugha ya mataifa yao. Bila kuisahau mikoa ya kaskazini magharibi mwa Tz, ya Rwanda na Burundi.

Hebu oneni hata aibu jamani, seriously..

Colonial legacy ni zaidi ya lugha...tunaona kuanzia kiuchumi, kisiasa na mpaka kijamii..
Wakoloni mpaka kutupatia uhuru, tayari walishapata njia mbadala ya kututawala..
..ukitaka kujua madhara yalivyo makubwa..uzi wako umemalizia kwa kiingereza,Jina lako lenyewe halijakaa kimatumbi..,[emoji2][emoji2]

Sent from my SM-A405FN using JamiiForums mobile app
 
Kutumia lugha ya mkoloni kwa shughuli mbali mbali hasa zisizoepukika kwa sasa, mfano masomo ya sayansi, sioni kama ni shida sana.

Shida yangu ni lugha ya mkoloni kufanywa kuwa ndio lugha ya taifa na inatumika mtaani hadi na wauza nyanya, ambao wangezweza kutumia lugha yao wenyewe kwenye masuala kama hayo.

Niwapongeze Kenya kwa kukifanya kiswahili kuwa lugha ya taifa lao, sina hakika juu ya Uganda,DRC kama wanampango juu ya kufanya kiswahili lugha ya mataifa yao. Bila kuisahau mikoa ya kaskazini magharibi mwa Tz, ya Rwanda na Burundi.

Hebu oneni hata aibu jamani, seriously..
Rwanda na Birundi ni mikoa ya kaskazini mwa Tanzania ! Da ngoja waje.
Mbona umeisahau malawi ? Mkoa wa kusini mwa Tanzania.
 
Kutumia lugha ya mkoloni kwa shughuli mbali mbali hasa zisizoepukika kwa sasa, mfano masomo ya sayansi, sioni kama ni shida sana.

Shida yangu ni lugha ya mkoloni kufanywa kuwa ndio lugha ya taifa na inatumika mtaani hadi na wauza nyanya, ambao wangezweza kutumia lugha yao wenyewe kwenye masuala kama hayo.

Niwapongeze Kenya kwa kukifanya kiswahili kuwa lugha ya taifa lao, sina hakika juu ya Uganda,DRC kama wanampango juu ya kufanya kiswahili lugha ya mataifa yao. Bila kuisahau mikoa ya kaskazini magharibi mwa Tz, ya Rwanda na Burundi.

Hebu oneni hata aibu jamani, seriously..
Umesahau kuwa kiswahili kina asili ya uarabuni
 
Mkuu.. kuna kipindi tulikuwa tunatafuta soko la matunda katika ma supermarkt hapa DAR likiwepo tunda letu pendwa lililobeba Biashara yetu strawberry [emoji526] .. mkuu huko masupermarkt wamejaa wahindi na wazungu mkuu.. kama haujui KINGE- ung’eng’e mkuu hata wa kuzugia haufanyi biashara .. tukubali tukatae kuna umuhimu wa kujifunza hii lugha hata kama haitakuwa lugha yetu ya taifa MKUU
 
Tunawekana sawa tu. Hata kiswahili chenyewe aliyekirasimisha ni mkoloni. Yeye ndiyo alikitoa kwenye alphabeti za kiarabu na kukileta kwenye a, e, i, o,u na konsonati. Yeye ndiye alikinyambua na kutengenezea aina saba za maneno.....sijui nomino, vidamshi, vihangaya etc. Mkoloni alikopy kutoka kiingereza "seven parts of speech". Na alihakikisha makosa yaliyotokea kwenye kiinngereza, hayajirudii kwenye kiswahili. Mojawapo ya kosa kubwa la Engish waliloepuka ni neno kuandikwa tofauti na kutamkwa tofauti. Mfano, unaandika 'road' unatamka 'rod'. Huu ujinga waliufuta kwenye kiswahili. Ndiyo maana mzungu akija leo unaweza ukamuandikia kiswahili akakisoma utadhani anajua kitu. Wakoloni walikipanga kiswahili bana. Wale wa lingua nadhani tunaelewana.
Ni moja ya lugha zinazofundishika kiundani. Luhga nyingi ukiondoa ya malkia na baadhi ya luhga za ulaya, ukianza kujifunza unaanza na irabu kama siyo consonati then unaanza kutiririka na maneno. Huwezi kuzama deep kama kiswahili mpaka kwenye ma-adjustebo na ma-molankoyi huko.
Mkoloni ndiyo alikiunda kiswahili ili kifundishike. Na alianza kukifundisha upya. Na kwa wamatumbi ilikuwa ni lugha mpya. Kwenye kuandika ndiyo walianza kujifunza upya kabisaaaa, kama wameletewa kichina. Kumbuka kiswahili cha mwanzo kwenye maandishi kilitumia alphabeti za kiarabu.
Na kwa taarifa tu, wajumbe wa baraza la kiswahili kutoka Congo. Walijitoa kwenye baraza la kiswahili la Afrika mashariki na kati baada ya Shaban Robert kuchaguliwa kuwa mjumbe wa baraza la kiswahili. Na huo ndio ulikuwa mwanzo wa kiswahili kulegalega fasi ya Congo. Ikumbukwe kuwa baraza la kiswahili enzi za mkoloni lilikuwa na wazungu watupu, hasa makasisi wa kimisionari. Wawakilishi wa kutoka Congo hawakuamini kama mtu mweusi anaweza kuwa mtaalamu wa kiswahili, hivyo walipinga uteuzi wa Shaban Robert na wakajitoa.
Mafather wa kimissionari ndio waliandika hizi kamusi zote za kiswahili. Kiufupi wao ndio walizitunga. Na kiswahili kilitengenezwa, kilisimamiwa na mkoloni mpaka kikakaza na kikasimama. Mkoloni alikuwa anaenda kufuta mpaka lahaja zote na kubaki na moko. Toka Lamu mpaka Kampala kiswahili ni lahaja moja tu, sikumbuki alichagua lahaja ipi, ila alitaka akomae na lahaja moja tu. Na mkoloni angeweza coz alishaweza.
Kwakusema hayo basi, itoshe kusema 'ajabu ya mvita kuota mvinde'. Hichi kiswhili tunachojipigia upatu leo.....ni zao halali la mkoloni. Na nachelea kusema mnyonge myongeni laki credit zake tumpe.

Wakatabahu
Infopaedia.
 
Umuhimu unaouna wewe kutokana na life style ya ukoloni ulizaliwa ukaikuta.Mtafute Mrusi,Mu Germany au Mchina umweleze hivyo kama atakuelewa.
 
Nadhani hakuna aliyebisha juu ya uliyoyaandika. Sasa nenda uingereza halafu zungumza kiswahili, maana kwa maelezo yako wao ndio wamekitunga. Halafu tupe mrejesho.

Mkuu mataifa yote hayo uliyoyataja yanatumia kingereza mkuu .. sema sio lugha ya kufundishia mashuleni..
 
Kumbuka tukienda kuomba misaada kwa wakoloni lazima tutumie lugha za wakoloni.
Hapa ndipo penye shida! Na kwa kutotilia umuhimu wa lugha ya kikoloni huenda tulipigwa kwenye mikataba feki ya raslimali zetu.
 
Back
Top Bottom