Kongole kwa kutoa madini ila wangeacha alphabet za kiarabu ingekuwa unyama sana.
Yah!! Ingekuwa unyama ila sidhani kama kingeendelea kama kilivyoendelea sasa. Muarabu
Kongole kwa kutoa madini ila wangeacha alphabet za kiarabu ingekuwa unyama sana.
Asante sana mkuu. Unyama ungekuwa mwingi sana kaka. Ila tatizo kiswahili kisingekuwa kikubwa na hadhi kama iliyokuwa nayo leo. Na lunga nyingi za kaliba ya kiswahili mara zote zillishia kupotea.
Unajua lunga ni sauti za nasibu. Lakini kuitanua lugha na kuikuza si nasibu tena. Ni suala linalohitaji utashi wa kisiasa, madaraka na bajeti. Ndipo lugha inapopata hadhi na kuwa jabali. Pia kuitanua lugha inahitaji utaalamu na usimamizi. Najaribu kusema haya ili tuelewe safari kilikotoka kiswahili na kilivyofika hapa.
Post yangu ya kwanza, nimejaribu kumpa picha ya Kiswahili mtoa mada, ili aone hadhi ya leo ya kiswahili ni juhudi za jana za mkoloni, lakini ameamua kushupaza shingo. Hadhi ya kiswahili ndio ilimpa wazo la kudhani kiswahili chaweza kuwa lugha ya kimataifa. Credit ya hadhi hiyo ni ya mkoloni.
Tuachane na hilo, tuje kwanini mkoloni aliamuwa kubadili kiswahili toka herufi za kiarabu. Mkoloni alikuwa na plani yake mkononi na maono yake kichwani. Wakoloni wa kimisionari walitafuta lugha ambayo ingewafaa kueneza habari njema za Yesu. (na kweli, concept ya lugha iliwalipa sana. Kazi waliyoipiga ndani ya muda mfupi utadhani walifika Tanzania miaka 3,000 iliyopita). Waliona kutumia kiingereza ingewachukua muda sana. Au kilatini ndiyo mambo yangekwama kabisaaaa. Tukumbuke kwenye habari njema enzi hizo Kilatini ndiyo ilikuwa habari ya mjini kati. Waliona Kiswahili kina ubantu mwingi na kubwa zaidi hakina asili ya jamii yoyote ya Kitanzania. Lugha yenye asili ya jamii fulani ingesababisha upinzani wakati wa kueneza habari njema kwa jamii nyingine. (Pata picha ya hiyo vita, wachaga wameletewa injili kwa kihaya.......mi sipati hiyo picha). Kiswahili kikaonekana ndiyo lugha pekee inayokidhi vigezo vikubwa. Mambo mengine ya kiswahili mkoloni wa kimisheni aliona ni madogo madogo na yanarekebishika. Utaalamu wanao, madaraka ya mkoloni ni yao, fungu wanalo.....basi wamisheni wakaingia mzigoni kwa mara ya pili. Nasema mara ya pili sababu mzigo ulishaanza. Mzigo wa mara ya kwanza ulikuwa ni utafiti huo nilioelezea hapo juu. Utafiti wa kujua ni lugha ipi itawafaa.
Basi wakakichukua kiswahili. Kwanza wakaona kiswahili kwa upande wa maandishi, alfabeti za kiarabu hazifai. Kulingana na scope yao na mahusiano ya kibantu na kiarabu, waliona haiwezekani. Pia nadhani hawakuwa na utaalamu mwingi wa hizo arabic alfabeti japokuwa pia walitoa sababu za kifonetiki na muundo. Ndio maana hata kwenye alfabeti za kirumi hawakutumia Q na X kwenye kuunda maandishi ya kiswahili.
Mkoloni alikisimamia na kukitanua sana kiswahili. Kazi mojawapo ya Baraza la kiswahili la mkoloni ilikuwa ni kuunda misamiati na istilahi. Nadhani kiswahili ndiyo lugha iliyotanuka zaidi katika fani za sayansi na ujuzi mwingine ukilinganisha na lugha nyingine za barani Afrika. Ni uzembe wetu tu hatukuweza kukiendeleza kiswahili baada ya kuachiwa usukani. Kuna istilahi nyingi sana za kisayansi zimeshapotea na zinaendelea kupotea . Kwa scope ya mkoloni kiswahili kingekuwa ni lugha inayotumika kufundishia mpaka chuo kikuu. Pamoja na dini, mkoloni pia alihitaji nguvukazi yenye weledi.
Kuna watu wanasema kiswahili hakifai kufundishia elimu ya juu sababu hakijitoshelezi kwa misamiati na istilahi. Huo ni uongo mkubwa. Neno kama barakoa lilikuwa limeshapotea kama siyo Uviko kuja kulihuisha tena. Neno kama mpinimwendo=crank shaft halipo tena. Na kuna mengi mengine ya nyanja anuwai tukisema tuanze kuyakusanya hapa jamvini tuta-terminology za kila tasnia.
Istilahi zipo nyingi sana ila wenye nafasi ya kutoa maamuzi kuhusu kiswahili nao hawajui kiswahili. Tatizo la nchi zetu hizi, ukiwa kiongozi basi unajihisi unajua kila kitu. Na sisi hata kiongozi akiongea shombo hupigiwa makofi na vifijo. Kiswahili ni kipana kinahitaji utashi wa kisiasa na kimamlaka kiwe lugha ya Afrika. Mandeleo yote ya kiswahili leo hayakuja kwa nasibu, ni juhudi za watawala wa kikoloni. Tena kiswahili kimerudi nyuma sanasana baada ya mkoloni kuondoka.