Kwanini nchi za Magharibi zinaisaidia Ukraine silaha bila kificho lakini huzishutumu nchi zingine zinazoisaidia Urusi?

Jugado

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2021
Posts
1,446
Reaction score
3,184
Kama kichwa cha thread kinavyoonesha, sishabikii vita ila inaonekana nchi za Magharibi na Marekani ni tishio sana kila anaemsaidia Urusi hufanya hivyo kisiri siri!. West hujiona wapo sahihi kwa Kila kitu na wanataka mtazamo/maadili yao uwe mtazamo wa dunia yote.

Hivi dunia haiwezi kuwepo bila vita Kila kona? Huyu anapigana na yule hawa wanapigana wenyewe Kwa wenyewe ili mradi tafrani.
 
Marekani na washirika wake ndiyo chanzo cha vurugu na fujo zote Duniani. Kwa ufupi tu Marekani, Israel na baadhi ya nchi za Magharibi mf. Uingereza; ndiyo chanzo kikuu cha vita, vurugu, na fujo zote zinazotokea hapa Duniani.

Na ndiyo maana yanatambulika pia kama Mataifa ya uovu (Evil Nations). Hayo Mataifa yanapenda muda wote Dunia iwe katika vita, mauaji, vurugu, ushetani, shida, taabu, na mateso tele kwa raia.
 
Ni kama vile mwanaume na mwanamke dunia hii ,sehemu yoyote mwanamke huplay kama yeye ndio victim na dunia nzima itarevolve arround her ila kwa mwanaume huonekana ni strong and no one takes his side..
 
Marekani na washirika wake ndiyo chanzo cha vurugu na fujo zote Duniani. Kwa ufupi tu Marekani, Israel na baadhi ya nchi za Magharibi mf. Uingereza; ndiyo chanzo kikuu cha vita, vurugu, na fujo zote zinazotokea hapa Duniani.

Na ndiyo maana yanatambulika pia kama Mataifa ya uovu (Evil Nations). Hayo Mataifa yanapenda muda wote Dunia iwe katika vita, mauaji, vurugu, ushetani, shida, taabu, na mateso tele kwa raia.
Sio kweli umekaririshwa au mahaba...
 
Kama kichwa cha thread kinavyoonesha, sishabikii vita ila inaonekana nchi za Magharibi na Marekani ni tishio sana kila anaemsaidia Urusi hufanya hivyo kisiri siri!. West hujiona wapo sahihi kwa Kila kitu na wanataka mtazamo/maadili yao uwe mtazamo wa dunia yote.

Hivi dunia haiwezi kuwepo bila vita Kila kona? Huyu anapigana na yule hawa wanapigana wenyewe Kwa wenyewe ili mradi tafrani.
Urusi ndie aliyeanzisha vita vya kichokozi visivyo na mashiko kwa kuivamia Ukraine na kuteka maeneo ya Ukraine na kufanya uharibifu na ukatili mkubwa sasa uliona watu anasaidiwa mvamizi kumpiga mwasithiriwa
 
Kama kichwa cha thread kinavyoonesha, sishabikii vita ila inaonekana nchi za Magharibi na Marekani ni tishio sana kila anaemsaidia Urusi hufanya hivyo kisiri siri!. West hujiona wapo sahihi kwa Kila kitu na wanataka mtazamo/maadili yao uwe mtazamo wa dunia yote.

Hivi dunia haiwezi kuwepo bila vita Kila kona? Huyu anapigana na yule hawa wanapigana wenyewe Kwa wenyewe ili mradi tafrani.
Hakuna msaada hapo, ni biashara.
 
Urusi ndio kavamia Ukraine na nchi nyingi za dunia zinakubaliana huo ni uvamizi haramu.
 
Marekani na washirika wake ndiyo chanzo cha vurugu na fujo zote Duniani. Kwa ufupi tu Marekani, Israel na baadhi ya nchi za Magharibi mf. Uingereza; ndiyo chanzo kikuu cha vita, vurugu, na fujo zote zinazotokea hapa Duniani.

Na ndiyo maana yanatambulika pia kama Mataifa ya uovu (Evil Nations). Hayo Mataifa yanapenda muda wote Dunia iwe katika vita, mauaji, vurugu, ushetani, shida, taabu, na mateso tele kwa raia.
Umeandika kishabiki sana ndugu yangu.
Siyo kweli kwamba vita vyote vinavyotokea duniani huanzishwa na nchi za magharibi, hizo ni chuki zako tu.
Vipi vile vikundi vyenye misimamo mikali ya kidini kama vile Alshabab, Boko Haram, Is, nk ?
 
Urusi ndio mvamizi

Time za kagera war mataifa mengi yaliisaidia Tanzania silaha kwa sababu ndio iliyovamiwa
Yepi na yepi? Wewe ukiambiwa Urusi anasaidiwa silaha na NK, Iran na SA, CN utaamini? That theory never holds kwani hukumbuki US kuvamia Iraq, Libya nani na nani waliwasaidia silaha wale mataifa hayo?
 
RUSSIA ni existential threat kwa himaya ya magharibi inayoongozwa na US.
 
Kama kichwa cha thread kinavyoonesha, sishabikii vita ila inaonekana nchi za Magharibi na Marekani ni tishio sana kila anaemsaidia Urusi hufanya hivyo kisiri siri!. West hujiona wapo sahihi kwa Kila kitu na wanataka mtazamo/maadili yao uwe mtazamo wa dunia yote.

Hivi dunia haiwezi kuwepo bila vita Kila kona? Huyu anapigana na yule hawa wanapigana wenyewe Kwa wenyewe ili mradi tafrani.
Hizo nchi zinaisaidia Ukraine kwa uwazi kabisa kwa sababu ni jambo jema. Wanaisaidia Ukraine ili imwondoe mvamizi nchini mwake.

Ukiisaidia Urusi maana yake unaisaidia iendelee na uvamizi wake.

Kama jirani yako akivamiwa na jambazi, unayemsaidia huyo jirani kwani utafanya kwa kificho? Lakini ukiamua kulisaidia jambazi, unadhani utafanya kwa uwazi?

Mambo yote mabaya hufanywa kwa kificho, bali mambo mema hufanywa kwa uwazi, na utataka hata watu wengine watambue ulichokifanya.
 
Marekani na washirika wake ndiyo chanzo cha vurugu na fujo zote Duniani. Kwa ufupi tu Marekani, Israel na baadhi ya nchi za Magharibi mf. Uingereza; ndiyo chanzo kikuu cha vita, vurugu, na fujo zote zinazotokea hapa Duniani.

Na ndiyo maana yanatambulika pia kama Mataifa ya uovu (Evil Nations). Hayo Mataifa yanapenda muda wote Dunia iwe katika vita, mauaji, vurugu, ushetani, shida, taabu, na mateso tele kwa raia.
Hadithi za vijiweni.
 
RUSSIA ni existential threat kwa himaya ya magharibi inayoongozwa na US.
Urusi mpaka inapewa msaada wa kifedha toka nchi za Magharibi halafu iwe tishio? Urusi ana nini cha pekee zaidi ya makombora ya nuklia?

Maiaka ya 1990 mpaka 2000, mageuzi ya kiuchumi ya Urusi yalifadhiliwa na nchi za Magharibi, huenda hata hujui.

Uchumi wa Russia, licha ya kuwa na idadi kubwa ya watu, ni mdogo kuliko hata wa South Korea.

United States: $20.89 trillion

China: $14.72 trillion

Japan: $5.06 trillion

Germany: $3.85 trillion

United Kingdom: $2.67 trillion

India: $2.66 trillion

France: $2.63 trillion

Italy: $1.89 trillion

Canada: $1.64 trillion

South Korea: $1.63 trillion

Russia: $1.48 trillion

Brazil: $1.44 trillion

Australia: $1.32 trillion

Uchumi wa Russia ni mdogo mara 14 ya ule wa USA. Hata ukijumlisha uchumi wa Russia, China na India, bado haufikii ule wa US.
 
Hizo nchi zinaisaidia Ukraine kwa uwazi kabisa kwa sababu ni jambo jema. Wanaisaidia Ukraine ili imwondoe mvamizi nchini mwake.

Ukiisaidia Urusi maana yake unaisaidia iendelee na uvamizi wake.

Kama jirani yako akivamiwa na jambazi, unayemsaidia huyo jirani kwani utafanya kwa kificho? Lakini ukiamua kulisaidia jambazi, unadhani utafanya kwa uwazi?

Mambo yote mabaya hufanywa kwa kificho, bali mambo mema hufanywa kwa uwazi, na utataka hata watu wengine watambue ulichokifanya.
Hiyo principle inge apply pande zote ingeeleweka. US alipoivamia Iraq, Bush aliiambia dunia kwamba "you are either with us or against us".
 
Back
Top Bottom